Ukweli usemwe: Aliyeharibu nchi hii ni Mwalimu Nyerere kwa kushindwa kuwapa Watanzania Elimu

Ukweli usemwe: Aliyeharibu nchi hii ni Mwalimu Nyerere kwa kushindwa kuwapa Watanzania Elimu

Tulikuwa tunakwenda vizuri mpaka yule mshenzi nduli Amini alipotuvamia ile 1978 Taifa likaingia vitani kwenye vita vya Kagera ndio sasa tukaharibikiwa.
Kaka mkuu shikamoo, umeeleza vizuriiiii, ila hapa mwisho umechanganya, pamoja na vita kuwa ni gharama lakini pia ukombozi wa nchi za kusini mwa afrika nalo limechangia pakubwa na inawezekana ni kuzidi hata hiyo vita yenyewe, tulitakiwa kufunga mkanda miezi 18 tu ila yaliyofuata sasa, na hata vita yenyewe kiuhalisia tungeweza kuiepuka kama tungetaka sema kutumwa nako ni shida
 
Nawasalimu wanaJF.
Leo nimeamua niseme ukweli kuhusu nchi yetu hii ya Tanzania.

Katika miaka 24 ya utawala wa Mwalimu Nyerere, alitangaza maadui wakubwa wa watatu wa watanzania:-
1. UJINGA
2. UMASKINI
3. MARADHI

Mwalimu Nyerere hakuwa visionary leader alikuwa mwanaharakati, badala ya kujenga nchi na kuwapatia elimu watanzania alikuwa na misemo tu, kuongea majukwaani tu bila vitendo.

Je, Mwalimu Nyerere kitu gani kilimshinda kujenga shule za msingi kila kijiji kwa miaka yote hiyo 24 badala yake akajenga ofsi za chama kila kijiji?

Je, kitu gani Mwalimu Nyerere kilimshinda kwa miaka 24 kujenga vyuo vya ufundi kila wilaya badala yake alijenga viwanja vya mpira wa miguu?

Lowassa aliweza kujenga shule za secondary kila kata. Je, Mwalimu Nyerere kitu gani kilimshinda kwa miaka 24 kujenga Shule hizo?

Tunaweza kutafuta mchawi wa taifa letu. But kusema kweli Nyerere alitukosea sana watanzania.

Nadhani Mwalimu Nyerere alikuwa na mentality za utawala wa kifalme ambao hauna malengo.

Tunaona mataifa mengi yaliyowekeza kwenye elimu alivyopiga hatua.

Yeye Mwalimu Nyerere hakuwa na nia kabisa ya watanzania wengi kupata elimu. Wakati wa Mwalimu Nyerere kusoma ilikuwa ni bahati na siyo haki ya Mtanzania.

Taifa lisilokuwa na elimu haliwezi kujiendesha vizuri, litabaki kuwa ombaomba tu.

Sisi kama Taifa ni lazima tujue tulipoangukia, tukainuke na kusonga mbele. Bado hatujachelewa.

Tanzania tupo na vijiji na mitaa isiyozidi 20,000. Kwani alishindwa nini kuchukua kila kijiji vijana 10 na kuwapeleka kusoma nchi za nje? Vijana 10 kila kijiji maana yake ni watanzania 200,000 tu.

Yaani angechukuwa wanawake 5 na wanaume 5.
But uwezo alikuwa nao wa kufanya hivyo.

Nitaendelea kueleza machungu yangu haya kwenye uzi huu ili tujue wapi tulipoangukia tukainuke na kusonga mbele...
Okay alifanya makosa its bad! So since that time imeshindikana kuweka mamb saw hatua kwa hatua? Au kosa lake halibadilishiki? Au inabid tumlaum milele!!
 
Matatizo ya Waafrika kwa Asilimia 60 yanafanana ndio maana Africa karibia yote tu inafanana, acha kupoteza muda kum single out Nyerere.
Yoda ni kweli waafrika tuna matatizo yanayofanana katika maendeleo yetu na nadhani tatizo si viongozi wetu bali kuna watu waliyojipa mamlaka ya kuongoza dunia, hao ndiyo wanaotufanya sisi waafrika tuwe jinsi tulivyo. Viongozi wetu mara nyingi huwa wanapata shinikizo kutoka huko juu, ukiwa kiongozi wa kweli wa kutaka kuwaletea watu wako maendeleo na kutengana na wakoloni basi utafnayiwa figisu na hatimaye wanaweza kukuondoa.
Na ni kweli kuwa wanaharakati wengi wa bara la Afrika walishindwa kutoboa na kuzifanya nchi zao zijitegemee kiuchumi kutokana na wao kutokuwa wabobezi katika msuala ya uendeshaji wa nchi na kujikuta wanakumbatia misimamo ambayo ipo kinyume na wakoloni au ile ambayo inafuatwa na mahasimu wa hao wakoloni.
 
Niseme japo kwa kifupi kuhusu lawama zako kwa mwalimu hayati JK Nyerere juu ya elimu ya Tanzania.

Mwalimu alipokea nchi toka kwa wakoloni ikiwa na kundi dogo sana la wasomi, na kundi jingine dogo la wanaojua kusoma na kuandika tofauti na majirani zetu.

Kazi ya kwanza ilikuwa ni kupunguza kundi la wasiojua kusoma na kuandika ambalo lilikuwa kubwa zaidi.

Akawa na kazi ya pili ya kuwasomesha vijana watakaosaidia katika idara nyeti kama madaktari na wahandisi. Kumbuka nafasi tunapopata uhuru zilikuwa zimeshikwa zaidi na wageni japo na wenyeji kidogo walikuwepo.

Haikuwa kazi rahisi kwa uchumi wa wakati huo kutoa elimu ya juu kwa watu wengi. Lakini alipambana kujenga shule za msingi,sekondari na chuo kikuu ili kuongeza idadi ya wasomi.

Alitumia wasomi wa idara mbalimbali kama walimu katika maeneo yao. Kwa mfano walimu mahali popote walipo walitakiwa kufundisha si tu wanafunzi, bali hata watu wazima katika eneo hilo japo wajue kusoma na kuandika.

Aliandika vitabu vya elimu ya watu wazima kwa mkono wake na wadau wengine, vikiwa na taaluma mbalumbali kama upishi, ufundi nk.

Kama haitoshi, ili kukuza kwa haraka elimu kwa wananchi, alianzisha mpango wa UPE (universal primary education), mpango ambao umerudiwa na Rais Magufuli. Mpango huu ndiyo ulioipa Tanzania sifa ya kuwa na wananchi wengi wanaojua Kusoma na Kuandika katika bara la Afrika mwishoni mwa miaka ya 70 hadi mwanzoni mwa miaka ya 80.

Kifupi mwalimu alipambana sana kuiinua Tanzania. Kumbuka haikuwa rahisi kutokana na mabeberu kuwakandamiza waafrika kupunguza kundi la wasomi wasijeleta upinzani wanapotaka kutunyonya.

Kama unaweza kujifunza, jifunze kwanini viwanda vya vyetu vilijengwa kisha vilikufa kwa haraka sana. Moja ya sababu ilikuwa ni kukosa vipuli na nguvu kazi (wataalam) kutokana na wazungu kugoma kuendeleza wataalamu wetu na kutuuzia vipuli.

Kama siyo juhudi zake Nyerere, tungekuwa na maisha kama ya Kenya. Sipati picha ingekuwaje.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
Mimi nimeishi kipindi Nyerere akiwa mtawala. Ndugu labda wewe umebahatika kukukulia katika jamii iliyopata kipaumbele hicho.

Nyerere aliitawala Tanzania miaka 24. Ni mikoa michache tu ilikuwa na shule za sekondari. Yaani miaka 24 akishindwa kujenga shule za sekondari kila kata!!!? Alishindwa kujenga shule za msingi kila kijiji?

Mikoa kama Kigoma, Lukwa nk shule za msingi na Sekondari hazikuwepo.

Mikoa iliyobahatika kuwa na shule ni Kilimanjaro na kagera. Kwingine kote ilikuwa giza nene.

Hebu niambie ni nini kilshinda kujenga vyuo vya ufundi stadi kila mkoa lakini aliweza kujenga viwanja vikubwa vya mpira?
 
Sasa huyo mbunge aliechaguliwa na hajui chochote kuhusu nchi si kachaguliwa na watu kama wewe mnaoijua nchi ama alijichagua mwenyewe?

Yani watu hamtaki ku accept failures zenu, mnafanya blame shifting.
Anachaguliwa na wajinga walio wengi kwenye jamii.

Wachache wenye uelewa wanashindwa nguvu na majority ya wasio na uelewa.
 
Nawasalimu wanaJF.
Leo nimeamua niseme ukweli kuhusu nchi yetu hii ya Tanzania.

Katika miaka 24 ya utawala wa Mwalimu Nyerere, alitangaza maadui wakubwa wa watatu wa watanzania:-
1. UJINGA
2. UMASKINI
3. MARADHI

Mwalimu Nyerere hakuwa visionary leader alikuwa mwanaharakati, badala ya kujenga nchi na kuwapatia elimu watanzania alikuwa na misemo tu, kuongea majukwaani tu bila vitendo.

Je, Mwalimu Nyerere kitu gani kilimshinda kujenga shule za msingi kila kijiji kwa miaka yote hiyo 24 badala yake akajenga ofsi za chama kila kijiji?

Je, kitu gani Mwalimu Nyerere kilimshinda kwa miaka 24 kujenga vyuo vya ufundi kila wilaya badala yake alijenga viwanja vya mpira wa miguu?

Lowassa aliweza kujenga shule za secondary kila kata. Je, Mwalimu Nyerere kitu gani kilimshinda kwa miaka 24 kujenga Shule hizo?

Tunaweza kutafuta mchawi wa taifa letu. But kusema kweli Nyerere alitukosea sana watanzania.

Nadhani Mwalimu Nyerere alikuwa na mentality za utawala wa kifalme ambao hauna malengo.

Tunaona mataifa mengi yaliyowekeza kwenye elimu alivyopiga hatua.

Yeye Mwalimu Nyerere hakuwa na nia kabisa ya watanzania wengi kupata elimu. Wakati wa Mwalimu Nyerere kusoma ilikuwa ni bahati na siyo haki ya Mtanzania.

Taifa lisilokuwa na elimu haliwezi kujiendesha vizuri, litabaki kuwa ombaomba tu.

Sisi kama Taifa ni lazima tujue tulipoangukia, tukainuke na kusonga mbele. Bado hatujachelewa.

Tanzania tupo na vijiji na mitaa isiyozidi 20,000. Kwani alishindwa nini kuchukua kila kijiji vijana 10 na kuwapeleka kusoma nchi za nje? Vijana 10 kila kijiji maana yake ni watanzania 200,000 tu.

Yaani angechukuwa wanawake 5 na wanaume 5.
But uwezo alikuwa nao wa kufanya hivyo.

Nitaendelea kueleza machungu yangu haya kwenye uzi huu ili tujue wapi tulipoangukia tukainuke na kusonga mbele...
Ivi mchongameno yeye alisoma?
 
Tusikae kimya sasa kusubiri miaka 10 ijayo Rais wetu aandike Kitabu cha kujutia kuingia mkataba huu mbovu wa Bandari, tumkosoe mapema ili akija kuandika kitabu hicho aseme nilishauriwa ila nilikataa Ushauri"-Baba Paroko wetu leo 27/08/2023
 
Umesahau wachaga walikua na nchi yao na uongozi wao, umesahau huko Mbeya, Iringa na Usukumani kulikua ni falme/kingdom zinazojiendesha
Mbona haya mambo yapo hadi leo na bado serikali inaendesha mambo yake bila tatizo.
 
alichokosea ni kuwa alijua hii katiba siyo ila akatuachia hivyo hivyo hayo mengine unamuonea!
angebadili katiba na kuweka sheria kali kwa viongozi wa umma wala tusingekuwa hapa!
Mzee Mchonga alijifanya Mungu mtu na aliamini ktk uungu wake,
 
Tusikae kimya sasa kusubiri miaka 10 ijayo Rais wetu aandike Kitabu cha kujutia kuingia mkataba huu mbovu wa Bandari, tumkosoe mapema ili akija kuandika kitabu hicho aseme nilishauriwa ila nilikataa Ushauri"-Baba Paroko wetu leo 27/08/2023
Hamna Cha kubadili ktk hiyo mikataba watu washakula mirungula
 
huyo nyerere hafai hata kuitwa baba wataifa maana hakuingia msituni kupigania nchi.matatizo tuliyo nayo ya ujinga na umasikini chanzo niyeye ,alipoona watu wanaanza kujanjaruka akaamua kung"atuka,, we fikiria ukivaa saa nzuri unaulizwa, redio kwa mjumbe wa nyumba kumi, tv anayo yeye tu kwako.katika utawala wake alitumia ili umtawale mtu mnyime uhulu , elimu,na nguvu ya pesa kama alivyofanya kupora mali za watu kipindi hicho kila aliemshauri alionekana adui,mf kama kambona,nyerere alikuwa shujaa wawatu ambao akili zao zimelala ,namlaumu sana huyu mzee angekuwa kalibu ni.alijiona mungu mtu,msomi n.k, wakupewa heshima ni kina kinjekitile ngwale sio yeye.kipindi anachukua nchi alikuta uchumi uko imara na pesa inathaman chakushangaza nchi ikafirisika ikiwa mikononi mwake
 
Nataka nikuongezee jambo hapa.
Kuna mtu mmoja aliitwa Oscar Kambona. Huyu aliweza kutendewa mambo ya ajabu sana na Mwalimu.

Kambona alipendekeza vyama vingi since independence. Bado Nyerere alikataa. Baada Nyerere aliweza kuwakamata ndugu zake Oscar Kambona na kuwafunga.

Kambona alikuwa Muumini wa kanisa la Anglican na alisomeshwa na viongozi wa Angican masuala ya Sheria huko Uingereza.

Inakuwaje vichwa kama hivi unaamua kuvipoteza kwa matakwa yako Binafsi. Kambona angesikilizwa hakika leo tungekuwa na katiba nzuri na nchi ya wasomi.
Kambona aliishiwa kuitwa Malaya na kuikimbia nchi...
 
Ukiachana na hilo. Pia yeye ndio chanzo cha mifumo mibovu miwili
1. Mfumo mbovu sana wa uongozi (ccm, katiba mbovu ya 1977)
Katiba ya mwaka 1977 haikuandikwa na Julius, taja walioandika hiyo katiba kisha tuone wao na wewe nani anauelewa mpana kwenye masuala ya katiba, kisha tujue kama unajua unachotuhumu!

2. Mfumo mbovu sana wa kiuchumi
Nenda kwenye trends, cheki ni sarafu gani ilikuwa na nguvu enzi hizo, cheki sarafu hiyo againsta Tzs, kisha tufananishe na baada ya mwaka 1984.

Moja ya indicators za ukuaji wa uchumi, ni matumizi ya nishati ya umeme. Julius alijengwa plant ya 205MW enzi zake, miaka ya hivi karibuni, tena tukiwa na gesi, tunajenga plant za 60MW, 45MW, 100MW, unaonaje hapo, tunasonga mbele au tumegeuza kichwa kubadili mbele yetu?
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Ccm from now and on bado hawana vision leader since Nyerere to SSH .
 
Hii mada niliona niipite tu kwakuwa kuanzia mtoa mada na wachangiaji wengi bado wako kwenye "Kati ya pesa na elimu, kipi bora" debate mode ki-primary zaidi.

Pamoja na wao kujisahaulisha UHALISIA lakini pia ni kana kwamba wamegoma kutumia uwezo wao wa kufikiri AU wanafikiri based on what they have seen already.

Ukiwapanga kwa UPIGAJI kazi uliotukuka katika nchi hii, wenye uzalendo na uwajibikaji, dhamira safi ya kuisogeza nchi mbele, basi listi itakuwa
1. JKN
2. JKN
3. JKN
4. JKN
5. Sokoine
6. Sokoine
7. JPM
8. JPM
9. JPM
10. BWM
JPM iliyeingia mitini na trillion 1.5 yule alikua jambazi sugu
 
Nawasalimu wanaJF.
Leo nimeamua niseme ukweli kuhusu nchi yetu hii ya Tanzania.

Katika miaka 24 ya utawala wa Mwalimu Nyerere, alitangaza maadui wakubwa wa watatu wa watanzania:-
1. UJINGA
2. UMASKINI
3. MARADHI

Mwalimu Nyerere hakuwa visionary leader alikuwa mwanaharakati, badala ya kujenga nchi na kuwapatia elimu watanzania alikuwa na misemo tu, kuongea majukwaani tu bila vitendo.

Je, Mwalimu Nyerere kitu gani kilimshinda kujenga shule za msingi kila kijiji kwa miaka yote hiyo 24 badala yake akajenga ofsi za chama kila kijiji?

Je, kitu gani Mwalimu Nyerere kilimshinda kwa miaka 24 kujenga vyuo vya ufundi kila wilaya badala yake alijenga viwanja vya mpira wa miguu?

Lowassa aliweza kujenga shule za secondary kila kata. Je, Mwalimu Nyerere kitu gani kilimshinda kwa miaka 24 kujenga Shule hizo?

Tunaweza kutafuta mchawi wa taifa letu. But kusema kweli Nyerere alitukosea sana watanzania.

Nadhani Mwalimu Nyerere alikuwa na mentality za utawala wa kifalme ambao hauna malengo.

Tunaona mataifa mengi yaliyowekeza kwenye elimu alivyopiga hatua.

Yeye Mwalimu Nyerere hakuwa na nia kabisa ya watanzania wengi kupata elimu. Wakati wa Mwalimu Nyerere kusoma ilikuwa ni bahati na siyo haki ya Mtanzania.

Taifa lisilokuwa na elimu haliwezi kujiendesha vizuri, litabaki kuwa ombaomba tu.

Sisi kama Taifa ni lazima tujue tulipoangukia, tukainuke na kusonga mbele. Bado hatujachelewa.

Tanzania tupo na vijiji na mitaa isiyozidi 20,000. Kwani alishindwa nini kuchukua kila kijiji vijana 10 na kuwapeleka kusoma nchi za nje? Vijana 10 kila kijiji maana yake ni watanzania 200,000 tu.

Yaani angechukuwa wanawake 5 na wanaume 5.
But uwezo alikuwa nao wa kufanya hivyo.

Nitaendelea kueleza machungu yangu haya kwenye uzi huu ili tujue wapi tulipoangukia tukainuke na kusonga mbele...
Kwani Rome, Dubai Tokyo, New York nk no zimejengwa siku moja?
Utawala wake ukiwa na umri wa 15 nchi iliingia vitani, vita ina gharama zake kuiendesha.
Mwanzo wa kuweka msingi/misingi una gharama zake Mwl alipambana na kuweka misingi kwa taifa.

62-24=38, hii miaka 38 warithi wake mmefanya nini ili kusawazisha hayo unayolalamikia?
Kwenye utawala wa mwl amepigana vita dhidi ya Uganda ninyi warithi wake ni vita ipi mmepigana?

Mwl amewasomesha akina BWM, JK, Edo Jasusi mbobevu A.k.a Maembe ili waje kulijenga taifa hao hao aliowasomesha wakaona hawatafanya ufisadi wao Mwl akiwa hai wakaamua kumleftisha,
Wakafanya ufisadi wa kutisha, Richmond na Dowans ,Ascrow, Meremeta nk nk wakabinafsisha mashirika ya umma kwa bei ya kutupa, viwanda wakaviua halafu unamlau mwl?
Mwl alisema tusomeshe kwanza vijana wetu ndipo gesi na madini yetu tuchimbe,
Mzazi watoto wako umewasomesha kwa kujifunga mkanda, wamemaliza masomo yao badala ya kuiendeleza familia na rasilimali za familia watoto hao hao wanangeuka wahujumu wa rasilimali za familia, hao hao wanamuua mzee wao ili wawe huru,
Hapo mzee ana kosa gani?
Hivi kati ya JK Senior na JK Junior nani aliye lihujumu hili taifa kwa ufisadi wa kutisha?
Au una chuki zako binafsi na mwl?
Mwl angefanya kila kitu?
Mwinyi Senior, Mkapa na huyo mnafiki wa Msg wao unasemaje juu yao?
Msitutoe kwenye ## Mkataba wa DP World na TPA hauna maslahi na taifa letu.
 
Msingi wa taifa ni muhimu mno.
Kama taifa limejengwa katika misingi ya kuongea tu. Utekelezaji zero, taifa hilo litakuwa chini ya utumwa kwa miaka yote.

Nyerere alikuwa na nafasi kubwa mno ya kujenga taifa imara. Alikuwa na nafasi ya kuwapatia elimu watanzania.

Sijui kwanini alishindwa.
 
Back
Top Bottom