Ukweli usemwe: Aliyeharibu nchi hii ni Mwalimu Nyerere kwa kushindwa kuwapa Watanzania Elimu

Ukweli usemwe: Aliyeharibu nchi hii ni Mwalimu Nyerere kwa kushindwa kuwapa Watanzania Elimu

Kwahiyo ulitaka Nyerere afanye kila kitu?

Ili wewe na baba yako mbaki kupanda juu ya meza kunywa konyagi na kucheza amapiano tu??

Kwasababu naona ulitaka matatizo yote ya Tanzania ni Nyerere tu alitakiwa kuwa ameyamaliza.
Ndugu yangu Elimu ndio msingi muhimu wa kujenga taifa.

Katika kauli mbiu yake kuhusu maadui watatu wa taifa ilikuwaje akashindwa kuweka mikakati ya maana katika kufuta ujinga?

Hapa tunaongea reality. Nyerere ali fail kuwapatia watanzania elimu.
 
Ndugu yangu unabahati sana kusoma.
Kipindi chake hiyo elimu ilikuwa bahati haikuwa haki ya mwananchi.

Nasema hivi mpaka anaondoka kuna mikoa mingi tu ilikuwa haina hata shule moja ya sekondari.

Je, sababu ilikuwa ni nini?
Maendeleo kwa ujumla yalikuwa chini sana, kutoka Dar mpaka Tanga ilikuwa safari ya usiku kucha, leo hii ni chini ya masaa matatu.
 
Lowassa walijenga shule za kata Kila kata akiwa kama nani?
Huyo Nyeterebunayemsema alijenga ofisi za Chama na viwanja vya mpira je, yeye hakuwà na waziri mkuu?
Shule za kata zilikengwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete na sio E. N. Lowassa.
Kama kule Rais alijenga lakini huku waziri mkuu kajenga! Rekebisha hapo kwanza vinginevyo andiko lako lifutwe.
Kosa langu ni nini? Kosa langu kusema ukweli? Lowassa ndiye aliyezunguka nchi nzima kupiga kelele kuhusu shule za kata. Alizomewa na wabunge lakini alikomaa.

Ndio maana shule za kata zikaitwa shule za Lowassa.
 
Mwl alifeli pia kwa kukitukuza kiswahili na kukipromote kuwa lugha ya taifa .
Tunetengeneza taifa ambalo lipo isolated sana na dunia. Watu wanahitaji akina mkandara kutafsiriwa cnn english news.
Angeweka kingereza ndio lugha ya taifa milembe ingekuwa imejaa machizi wengi sana tanzania na yeye anakili akajua machizi niwangekuwa wengi
 
Kosa langu ni nini? Kosa langu kusema ukweli? Lowassa ndiye aliyezunguka nchi nzima kupiga kelele kuhusu shule za kata. Alizomewa na wabunge lakini alikomaa.

Ndio maana shule za kata zikaitwa shule za Lowassa.
Mbona hakupigania uhuru kazi yake ni kujioshea kwa kila mtu
 
Je, Mwalimu Nyerere kitu gani kilimshinda kujenga shule za msingi kila kijiji kwa miaka yote hiyo 24 badala yake akajenga ofsi za chama kila kijiji?

Je, kitu gani Mwalimu Nyerere kilimshinda kwa miaka 24 kujenga vyuo vya ufundi kila wilaya badala yake alijenga viwanja vya mpira wa miguu?

Lowassa aliweza kujenga shule za secondary kila kata. Je, Mwalimu Nyerere kitu gani kilimshinda kwa miaka 24 kujenga Shule hizo?
Ukimtuhumu Hayati Mwl. Julius K. Nyerere hutakuwa umemtendea haki, alijenga shule nyingi tu na hata watoto wake wote walisoma kwenye shule za umma, kwa hilo ytu ujue alikuwa visionery kila kijiji kulikuwa na shule kwa wakati wake ila huenda hujui, aliyevuruga elimu ya nchi anajulikana.
 
Usipende laumu kitu fanya kitu wangapi wamefungua ngo's na wanasaidia watu
 
Ukimtuhumu Hayati Mwl. Julius K. Nyerere hutakuwa umemtendea haki, alijenga shule nyingi tu na hata watoto wake wote walisoma kwenye shule za umma, kwa hilo ytu ujue alikuwa visionery kila kijiji kulikuwa na shule kwa wakati wake ila huenda hujui, aliyevuruga elimu ya nchi anajulikana.
Dah!! Sijajua mzee wewe umekulia mkoa gani.

Kijijini kwetu kulikuwa na shule mbili za msingi kwenye kata ambayo ilikuwa na vijiji saba. Tena shule hizo zilijengwa na wakoloni.

Shule ya sekondari ilikuwa moja mkoa wote.

Tell me my friend.
 
Dah!! Sijajua mzee wewe umekulia mkoa gani.

Kijijini kwetu kulikuwa na shule mbili za msingi kwenye kata ambayo ilikuwa na vijiji saba. Tena shule hizo zilijengwa na wakoloni.

Shule ya sekondari ilikuwa moja mkoa wote.

Tell me my friend.
Wilayani kwangu kulikuwa na shule kila kijiji ambazo zilijengwa kwa uhamasishwaji kwa wananchi kuchangia nguvu zao kufyatua na kuchoma matofari na serikali ilileta vifaa vya ujenzi na walimu, that is how he did
 
Nyerere kaiumiza sana Tanzania, hakuna alichokifanya kikawa na mafanikio.

Aliliamini sana kanisa katoliki, ndilo lililompotosha?

Nyerere aliiweka imani yake kwa kanisa katoliki kwanza kuliko chochote, ni kama kondoo mwengine yeyote, hakuweza kuona mbali na kujiongoza mwenyewe zaidi ya kuongozwa na wachungaji wake. Inaitwa "blind faith".
Punguza mavi hayo kichwani mwako wewe bibi

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Wilayani kwangu kulikuwa na shule kila kijiji ambazo zilijengwa kwa uhamasishwaji kwa wananchi kuchangia nguvu zao na serikali ilileta vifaa na walimu, that is how he did
Wilaya gani mkuu.
 
Wilaya gani mkuu.
Tafuta wilaya kongwe zote Tanzania utaona sehemu ambazo wananchi walihamasika kujenga mashule ya msingi kila kijiji na sekondari kila kata mwishoni mwa 70s na mwanzoni mwa 80s
 
Tafuta wilaya kongwe zote Tanzania utaona sehemu ambazo wananchi walihamasika kujenga mashule ya msingi kila kijiji na sekondari kila kata mwishoni mwa mwa 70s na mwanzoni mwa 80s
Mzee umeshindwa kutaja jina la wilaya! Nini unaogopa?
 
Huyu huyu Nyerere alilea Dini yake ya ukatoliki kwa kukandamiza madhehebu mengine ya kikristu, mpaka wakatoliki wanajiona wana steki kubwa kufanya uamuzi zaidi ya dini zingine kuhusu serikali, kimya kimya alikua ana promote ukatoliki serikalini kwa kuwapa vyeo mbali mbali na huku nje anaonyesha iko sawa kwa wote, Nyerere alikua Mdini wa chini chini.
Ningeshangaa sana usingekuja na hizi lawama na chuki yako kwa Kanisa Katoliki.Unaleta chuki zako kwa Kanisa Katoliki kwa kujifanya unayatetea madhehebu mengine ya Kikristu kumbe deep down unachuki kubwa na Ukristo na unatamani hata hii Nchi ingekuwa ni ya Ki Islam tu.Tuzoee tu,kanisa Katoliki lipo na huwezi kulifuta na hayo makanisa mengine yataendelea kuwepo na jifunze kuishi kwa uhalisia huu.
 
Mwalimu tumlaumu kwa jambo moja tu.
Katiba.
Mwalimu alikuwa na kila uwezo wa kuhakikisha anaacha katiba bora kwa ustawi wa Taifa,lakini pamoja na yeye kutambua ubovu wa katiba,hakufanya jambo lolote kutoa huo ubovu.
 
Nawasalimu wanaJF.
Leo nimeamua niseme ukweli kuhusu nchi yetu hii ya Tanzania.

Katika miaka 24 ya utawala wa Mwalimu Nyerere, alitangaza maadui wakubwa wa watatu wa watanzania:-
1. UJINGA
2. UMASKINI
3. MARADHI

Mwalimu Nyerere hakuwa visionary leader alikuwa mwanaharakati, badala ya kujenga nchi na kuwapatia elimu watanzania alikuwa na misemo tu, kuongea majukwaani tu bila vitendo.

Je, Mwalimu Nyerere kitu gani kilimshinda kujenga shule za msingi kila kijiji kwa miaka yote hiyo 24 badala yake akajenga ofsi za chama kila kijiji?

Je, kitu gani Mwalimu Nyerere kilimshinda kwa miaka 24 kujenga vyuo vya ufundi kila wilaya badala yake alijenga viwanja vya mpira wa miguu?

Lowassa aliweza kujenga shule za secondary kila kata. Je, Mwalimu Nyerere kitu gani kilimshinda kwa miaka 24 kujenga Shule hizo?

Tunaweza kutafuta mchawi wa taifa letu. But kusema kweli Nyerere alitukosea sana watanzania.

Nadhani Mwalimu Nyerere alikuwa na mentality za utawala wa kifalme ambao hauna malengo.

Tunaona mataifa mengi yaliyowekeza kwenye elimu alivyopiga hatua.

Yeye Mwalimu Nyerere hakuwa na nia kabisa ya watanzania wengi kupata elimu. Wakati wa Mwalimu Nyerere kusoma ilikuwa ni bahati na siyo haki ya Mtanzania.

Taifa lisilokuwa na elimu haliwezi kujiendesha vizuri, litabaki kuwa ombaomba tu.

Sisi kama Taifa ni lazima tujue tulipoangukia, tukainuke na kusonga mbele. Bado hatujachelewa.

Tanzania tupo na vijiji na mitaa isiyozidi 20,000. Kwani alishindwa nini kuchukua kila kijiji vijana 10 na kuwapeleka kusoma nchi za nje? Vijana 10 kila kijiji maana yake ni watanzania 200,000 tu.

Yaani angechukuwa wanawake 5 na wanaume 5.
But uwezo alikuwa nao wa kufanya hivyo.

Nitaendelea kueleza machungu yangu haya kwenye uzi huu ili tujue wapi tulipoangukia tukainuke na kusonga mbele...
Hio iko wazi kabisa dingilai ndo alizamisha hii meli mazima!

Baba yangu mzazi (mzaliwa wa 1961) alikuwa kinara darasani lakini hakuchaguliwa kwenda sekondari (around 1975 hivi) wakachaguliwa wengine 7 ambao walikuwa watoto wa waalimu na watu wengine mashuhuri hapo kijijini. Nilimuhoji kwa uchungu akanijibu "hakukuwa na shule za kutosha hivyo nafasi zilikuwa chache sana". Maisha yalienda akajiajiri akufungua kampuni 1991. Mwalimu aliekuwa akimtuma buchani (mbali, uelekeo wa kupanda mlima) kununua nyama huku wenzake darasani wanangoja kuanza mtihani (alifanya hivyo mara nyingi sana) alimleta mwanae (aliefaulu kwenda sekondari) ofisini kwa baba yangu kumuombea kazi na kwa upendo tu mzee alimuajiri classmate wake. Hii maisha bana, anyway ni machungu tu natoa.

Nirudi kwenye mada, ADUI alikuwa mmoja tu nae ni UJINGA! maradhi na umasikini ni matokeo ya UJINGA.
Nawasilisha hoja mheshimiwa mwenye uzi.
 
Back
Top Bottom