Sipendi sana kuingilia mada za machawa siku hizi, ila nimona wewe nikujibu.
Kiuhalisia, huyo P Funk ana afadhali kuliko hao WCB.
PF hamiliki Album za wasanii ila anamiliki BEATS. Na ndio maana hujawahi kusikia Msanii analalamika.
Na kiukweli, wasanii wa zamani walipata pesa mnoooo.
Hakuna Msanii ambaye hakupata pesa. Kuna wasanii mpaka walikuwa wanatembea na pesa kwenye but I za gari.
Tatizo kubwa ukiwa msanii WCB ujue Ni Kama unafanya kazi ambayo Ni COMMISSION BASED.
Inatakiwa ufanye kazi halafu, iqe Shows, ngoma mitandaoni au endorsement kila kinachopatikana unakatwa 60% unapewa 40% kwa mkataba wa miaka 10.
Maana yake, unafonzea kila kitu. Miaka 10 kisanii hutakuwa na jipya tena.
Na baada ya kutoka hutakuwa unamiliki nyimbo yoyote Wala digital platform zako.
Kuna vitu watu huwa wanakubali kwasababu ya shida tu.