Uliambiwa nini ukiwa Mtoto lakini baada ya kukua ukagundua ni Uongo?

Leta muhindi huo nikutengenezee njia ya kwenda mbeya hahahhaha....kumbe babu anaula muhindi wangu wote lohhh !!
 
Nilidanganywa kuwa watoto hununuliwa dukan
Kumbe loh!!!
 
Nilikua napendaga kukwangua sufuria la ukoko nikadanganywa kama hujashiba ukijitwisha kichwani sufuria ukazunguka nyumba Mara kumi sufuria linajaa wali, basi nikaaminigi ni kweli ila sikuwahi kujaribu kwa sbb ya aibu ntaonekana mlafi!
 
Eti ukikutana na Alibino njiani jitemee mate kifuani usipojitemea ukiwa mkubwa na wewe kama ni mwanamke utapata mtoto albino au kama ni mwanamme mkeo utakaemuoa atazaa mtoto albino
 
Et rud kavae viatu ndan nakusubir APA APA ukiingia tu ndan kutoka nje mama hayupo nalia had nacnzia apoapo
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] nimejikuta nacheka mwenyewe maana hii mbinu naitumia kila wkt kumtoroka mwanangu
 
Hii tabia mama alikuwa anaenda shamba nalilia kumfuata akaniambia ataniletea bagia.
Nikarudi kwa furaha.

Alivorudi ile kumdai tuu aseee
Alivokurupuka
Shamba kuna viazi na mihogo mimi hizo bagia ntapata wapi??


Nyingine

Eti ukiona kimondo usiseme kesho utaokota hela.

Niliwahi kuona kama sita hivi kesho yake nilishinda mtaani kama chokola, nilichoambulia ni bakora za uzurulaji na
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…