Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Ok!! nashukuru sana kiongozi
 
Mkuu una madini,, ni biashara ipi hyo ilikua na ilikuaje tupe madini kdogo
 
Embu itolee ufafanuzi hyo sentensi"Biashara yako iwe chini ya kampuni"[emoji106]
 
Mkuu una madini,, ni biashara ipi hyo ilikua na ilikuaje tupe madini kdogo
Biashara ya kununua mazao ya chakula ya msimu na kuuza. Ile ambayo kuna jamaa kakushawishi uanze sijui uende Mtwara sijui wapi Kusini uko.

Ile biashara inataka uwe na elimu kubwa na uzoefu wa mazingira na mazao husika. Ukiwa nje unaona ni mahindi tu, ukiingia field unakutana na mahindi yana namba sijui H30 na ngapi, mara punje ina pumba nyingi mara inatoa kiini kikubwa mara imepinda katikati hivyo gunia halina uzito sana.
Hujaja kwenye mpunga uko utakutana na mbegu zaidi ya nane na huwezi zijua kichwakichwa.

In short tuseme ni biashara ambayo unatakiwa uwe mtu wa kijijini kukekule, sio umetoka Kigamboni wajomba zako wanauza CD na mitumba eti unakurupuka kuuza mpunga. Utaijulia wapi kalima wangu, Zambia, salo, mbawa mbili na India?
Mpaka unakuja kujua mchezo umechoma mtaji tiyari. Ukija kuujua serikali inazuia mazao kuuzwa nje, msimu unaofuata serikali inanunua michele kutoka Pakistan bei inashuka sokoni.

Nilikaa hata msimu haukuisha nikala kona. Kila niliyekutana naye kachoka. Wenye faida ni wanaonunua na kuweka store. Sasa wewe na 10M yako ukiiweka store then ukafanye nini. Nikatimua mbio
 
Kiufupi biashara yoyote yenye mahusiano na kilimo sio lelemama unatakiwa uwe na roho ya mamba.
 
Alikuwa anapigwa lakini hakuchunguza kabla ya kukata tamaa.

Au huenda kipimo cha kuuzia kilikuwa kikubwa tofauti na kipimo sahihi wanachopima wenzake
 
Uvumilivu

Biashara yoyote inahtaji uvumilivu,unaweza ukahisi hamna wateja eneo ulilofungua biashara lakini si kweli wateja wapo na ni hao hao unaowaona wanapita nnje ya biashara yako.

TABIA ZA WATEJA

Wateja wana tabia ya kusikiliziana,anataka aone nani anakuja dukani kwako ndio na yeye aje, Usijali wala usikate tamaaa...

endelea na Promo utawaona mmoja mmoja anakuja.

"Chelewa kufunga Wahi kufungua" Huu ni moja ya Uchawi namba 1 kwa biashara Mpya.

Amini nakwambia kuna biashara unapatia location,mtaji na kila kitu ukiona wateja hawaji jua kuna eneo unakosea usikimbulie kuifunga na kubadlisha.

Usiuze bidhaa 1 dukani kwako hata kama n huduma,usitoe moja toa na zngine za kuvuta wateja.

Binafsi naweza fungua Barber Shop ya kunyoa mtu 20,000 lakini katka branding zangu matangazo na sticker ntaongezea

VIFURUSHI NA VOCHA ZINAPATIKANA

watu watakua wanakuja nunua vocha na vifurushi,wale wateja wasikiliziaji watajua wenzao wanaingia kunyolewa kumbe mtu kafata vocha,akija kunyoa siku ananyolewa vizuri Ana NASA.

Mengi ya kuandika,ila kama mtaji unao usiruhusu biashara ikushinde.
 
Asante kwa Madini Mkuu.
 
M
Mkuu wewe unafanya biashara gan na umetoa kais gan? Au umeandika tii ili watu waingie mkenge?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…