Ulijisikiaje baada ya kugundua unaenda kuwa mzazi kwa Mara ya kwanza?

Ulijisikiaje baada ya kugundua unaenda kuwa mzazi kwa Mara ya kwanza?

Kwanza kabla sijajifungua nilikua nawaza Sana na kumuomba Mungu nijifungue Salama.Nilikua nawaza Ile picha ya Leba je nitatoka Salama.Mungu ni mwema nakumbuka mtoto wangu wa Kwanza nilienda kujifungulia nyumbani.

Mungu alinijalia nikajifungua salama.Mama yangu ndo mtu wa Kwanza kuingia Leba na kuanza kumfuta.Ni mkunga mama lakini wakati napush hakuweza kukaa pale mpaka aliposikia sauti ya kichanga ndo akaingia.
Nilipompigia simu mume wangu kwamba nimejifungua salama Kesho yake Tu mapema Sana alipanda gari kuja home.Ni furaha kwakweli kuwa mzazi.

Changamoto sasa za kulea mtoto mchanga.Mtoto analia usiku mpaka na Mimi nalia.Nashukuru Mungu mama alinipa support kubwa Sana plus wadongo zangu.
Furaha hua inakua kubwa zaidi ukipata mume anaejali watoto.Aisee huyu mume wangu anajua kujali watoto mpaka basi.Kwangu hiyo ni furaha kubwa Sana.Dah Leo nimeandika Sana.
 
Back
Top Bottom