Ulipokea vipi Msiba wa Hayati Magufuli?

Ulipokea vipi Msiba wa Hayati Magufuli?

Dah, tofauti kabisa na mimi. Baada ya kukagua mabweni ya Kurasini baada ya Daraja la Ubungo, Stendi ya Mbezi na Soko la Kisutu kuna jamaa alinipigia na kunismbia "game is over" Kwa hiyo sikusubiri date 17, nikaanza shangwe.
 
Siku hiyo kabla haijatangazwa japo nilikuwa na uhakika Jiwe hayupo..
Nilienda kwenye min supermarket moja mkoa flan jioni nikamkuta mmiliki..

Katika story nikamwambia unajua Jiwe kakata moto.. Mmiliki kidogo anitoe na mawe... Eti ondoka na habari zako za kichochezi.. Unataka biashara yangu nisumbuliwe..

Jamaa akaomba kabisa story za Jiwe nisimwambie kwa uoga wa kushughulikiwa akisema sitaki matatizo .. Polisi ilikuwa inadaka watu..

Usiku napata habari.. Sikufurahi kwa kuwa ni binadamu mwenzetu ila kelele nje... Kuna Grocery majirani walitoka wengine vifua wazi walipiga pombe zikaisha.. Na mimi nilijumuika nao.

Kesho yake naenda kwenye minsupermarket sikumkuta mmiliki ila nilimpigia simu... Kumbe yeye alizima bar kwa furaha.. Anadai alikuwa na uoga sana wa maisha kipindi cha Jiwe hasa kuwekewa mizengwe katika biashara au ukionekana unasupport upinzani..
 
Mbona huulizinwa MKAPA ambazo ulikuwa wa ghafla?
Wa huyu tuliambiwa na Waziri Mkuu kwamba yuko fiti anafanya shughuuli kama kawaida! mnamtaka aende Kariakoo mmuone huko?
Daah hii ni wiki Moja mbaya sana!
Jpm alikuwa kipenzi cha Watu na wala hii haina ubishi
 
Alikuwa ni kiongozi mbaya kupindukia. Japo alikuwa muuaji na katili, kiasi cha kila mpenda haki kupendelea kutokuwa na kiongozi wa namna ile, lakini nilisikitika kupokea taarifa za kifo chake. Ni jambo jema mwovu aendelee kuishi, ajutie uovu wake au abadilike na kuuchukia uovu wake wa kale. Nilipoisikia habari ile, nilishtuka, nikaamka. Nilikaa kimya kwa dakika, nikajawa na simanzi. Maana kwa kweli pamoja na kuwaaumiza watu wengi, haikuwahi kutokea akilini mwangu kufikiria kuwa, aheri afe. Ningependelea aondoke kwenye uongozi lakini siyo kufa. Lakini basi kwa kuwa ilitokea, mapenzi ya Bwana yalitimia kwa kipimo cha hekima yake Mungu.

Vyovyote iwavyo, kifo chake ni fundisho kubwa kwetu tulio hai. Cha kujiuliza, sisi tunafanya nini tofauti na uovu wake? Tunafanya nini sambamba na mazuri yake, hata kama yakiwa machache? Kuna wengine ni fundisho kubwa kwao mara mbili zaidi maana wakati wa utawala wake, walitenda uovu mwingi wakiamini yupo wa kuwalinda kwenye uovu wao.

Wapo waliomkufuru Mungu, hata wakamwita Magufuli ni Mungu, wengine wakasema ni zaidi ya Yesu, na wengine wakasema eti Mungu amshukuru Magufuli. Na wote sasa hivi wamebakia kama kondoo wasio na mchungaji.

Hii ilikuwa ni kufuru kubwa. Mbaya zaidi hata marehemu mwenyewe hakuwakemea. Mwalimu Nyerere alipopambwa kupita kiasi, alimaka na kusema, 'mmeniita mchongameno nimenyamaza, mmeniita Haambiliki nimenyamaza, lakini hili la Musa, kuniita Musa, hapana, sitaki kusikia'. Yaani Mwalimu aliona kuwa yeye hafanani wala kumkaribia kwa chochote nabii Musa aliyewaongoza wana wa Israel toka utumwani Misri. Nabii Musa alikuwa mwanadamu, lakini mwalimu aliona bado Nabii Musa ni mkubwa mno kuweza kufananishwa naye. Marehemu alilinganishwa na Mungu, yeye akakaa kimya. Lilikuwa kosa kubwa.

Kifo chake ni fundisho kwetu kuwa Mungu hana ushirika na mwanadamu yeyote katika Umungu wake. Tunafundishwa kuwa Mungu hana mwanzo wala mwisho. Kifo hiki kilitufundisha kuwa hata uwe na nini, wewe bado ni mwanadamu, unafanana na wanadamu wenzako katika kuzaliwa na kufa.

Tuendelee kuomba, Mungu atujalie hekima ya kujifunza kupitia kifo hiki, na wala kifo hiki kisitufanye kuzidi kumkosea yeye Mungu au wanadamu wenzetu.
Ujumbe mzito na comment bora kabisa kwenye uzi huu. Asante Mkuu kwa kuturejesha kwenye neno la Mungu.
 
nimepitia uzi nimegundua kumbe jiwe alikuwa hapendwi na walevi,kila mtu nilikuwa grocery nikapigiwa simu!!!

 kweli Tz inawatu wa ajabu aisee!!!,,haya tuendeleeni kunywa beer na umasikini wetu japo humu Jf kila mtu ana noti tu hatakama anaishi kwa shemeji yake
 
Mi naishi karibu na kituo cha polisi... Sikuamini nilivyoona polisi wakifurahia... Mi nilijiunga nao kwenye kibanda umiza cha polisi mwenzao kuwaunga mkono walinzi wa raia na mali zetu.... Ofkozi kwa kupiga gambe
Mtani nimepata simu ya wakili wangu kwaheri [emoji23] [emoji1545][emoji1544][emoji1550]
 
Back
Top Bottom