Ulipokea vipi Msiba wa Hayati Magufuli?

Hukumu ya Mungu siku zote ni ya haki. Huwezi kutumia mabilioni ya kodi zetu kuandaa uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu kisha ukatumia mabilioni mengine kuvuruga chaguzi hizo tena kwa kumwaga damu halafu Mungu akuache kuendelea kupumua, never !!!!!
 
Watoto wa juzi mna tabu sana, hivi wakati wa msiba wa Mchonga ulikuwa na umri gani? Huu msiba wa Jiwe ambao majority tulishangilia huo ulikuwa msiba au ilikuwa sherehe?
 

Jamaa alikuwa anapendwa watu mpaka walikuwa wanaivamia njia kama hakuwa na mpango wa kusimama liwalo na liwe lakini asimame wamuone tu.

Raisi wa watu
Hata yule mwovu anapendwa sana na watu wa aina yake au wasiomjua vyema kuwa ni mwaribifu mkuu
 
Maajabu hata sisi ughaibuni tulipata taarifa(zisizo rasmi) kuanzia tarehe 9 lakini ikawa ukiuliza wengine wanaingizwa mkenge na wanasiasa(akina Kassim Majaliwa) kwamba mwehu bado yuko hai na Corona anaikabili kwa ndimu, vitunguu na tangawizi [emoji38][emoji38].
 
Aisee acha tu, ilikuwa kama ndoto nafungua tv naona kwenye screen kuna kapicha kamheshimiwa halafu mara taarifa ya mama inaletwa akitaalifu umma duh nilishituka sana.
 
Reactions: nao
Poleni sana.Mngekunywa diazepam tabs.
Acha tu. hadi sasa tunaumia tu.. tulikuwa tumeanza kuchimbiwa mitaro ya kuletewa maji hadi sasa hatujui lini yatafika huku kwetu. Barabara ay Lami tunaziona kwa macho kwa wenzetu tu.
 
Reactions: nao
Acha tu. hadi sasa tunaumia tu.. tulikuwa tumeanza kuchimbiwa mitaro ya kuletewa maji hadi sasa hatujui lini yatafika huku kwetu. Barabara ay Lami tunaziona kwa macho kwa wenzetu tu.
Poleni aisee!Undeni tawi jipya la machawa.Hakika mtafikiwa na mizigo yenu mizito itatuliwa.
 
Sherehe kubwa sana, tulikunywa na kula nyama choma kwa fujo, kama wiki zima.
 
Mixed feelings indeed.

Mwenyenzi Mungu amrehemu..
 
Mkuu watu kuwa wengi kwenye msiba haimaanishi alipendwa. Wengine walikwenda kushuhudia ikiwa Shetani naye hufa
Angalia video sio ya msiba alikuwa hai bado anapita tu njiani kwenye mishemishe zake. Baada ya ving’ora kukatiza wananchi walipoona akuwa na mpango wa kusimama wakavamia barabara kitemi gari lake binafsi ikabidi msafara wote usimame.

Halafu video imerokediwa na bystander tu aliekuwepo kwenye eneo. Unaona upendo wa wazi kutoka kwa wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…