Ulitumia mbinu gani kumfanya Mtoto wako aache kulala chumbani kwako?

Ulitumia mbinu gani kumfanya Mtoto wako aache kulala chumbani kwako?

mimi nakuelewa, tatizo baadhi ya wachangiaji hapa wanapotosha kwa kuwa hawana watoto/hawana experience. Mzazi hawezi kulala usingizi wakati mtoto yupo mlangoni kwake analia
Mimi ni mzazi nimekaza kwa wote and wanaodopt within a month.....
Nlifanya mistake mtoto wa kwanza took a painful lesson & waliobaki hawajanisumbua, separate them when young inakua sio ishu.
 
Hebu naomba mnisaidie hapa jaman ili niweze kuwahamisha hawa Watoto chumbani kwangu (Miaka 4&2). Imekuwa vita ya muda mrefu sana hawataki kulala kwenye Chumba chao, wanalazimisha kuendelea kulala kwangu

Hata nikisubiri walale halafu niwahamishe wakishtuka kwenye zoezi la kuhamishwa mtanange unaanza upya, walalia kama ndio wanakufa siku hiyo 😀 😀 😀 😀😀😀

Wenzangu mlifanyaje kwenye hili?
Lala nao chumbani kwao kisha watotoroke
 
Kuna jamaa na mkewe wana watoto watano lakin jamaa na mkewe wanakula peke yao sebuleni na watoto wanalia jikoni na mfanyakaz na wakimaliza kula ni kulala

Yaan jamaa hakai sebuleni na watoto,afu kuanzia wa miaka 2 na wengine wanalala na beki 3
 
mimi wakwangu mmoja anamiaka 6 na mwingine anamiaka 3,, nijuzi tu wameanza kulala chumba chao napo ni baada ya huyu mkubwa kushangaza,, kaamka asubuh kaenda kufanya usafi chumba kingine halafu anatuambia leo nawahama nahamia kwenye chumba changu mimi na mdogo wangu,, hvo nakushauri hata hao wako waache ikifika muda wenyewe watahama.
We jamaa yani mtoto wa miaka 6 unalala nae kitanda kimoja?
 
Kuna jamaa na mkewe wana watoto watano lakin jamaa na mkewe wanakula peke yao sebuleni na watoto wanalia jikoni na mfanyakaz na wakimaliza kula ni kulala

Yaan jamaa hakai sebuleni na watoto,afu kuanzia wa miaka 2 na wengine wanalala na beki 3
Hii sio sawa kwa ustawi wa familia. Kila kitu inatakiwa familia ijumuike pamoja isipokuwa muda wa kulala tu watoto walale chumba chao.

Sasa huyo jamaa hata kula tu anawatenga watoto? Ana uhakika gani huko jikoni kama watoto wanakula vizuri wanashiba? Usikute beki tatu ndio anabugia minofu yote watoto wanaambulia mifupa tu.
 
Mama yao anakuwa anapita pita,hata muda wa kulala anaenda kuwaangalia,kuna wakat alikuwa hafatilii wakat wa kulala hasa wanapopata wageni akajikuta watoto wakat mwingine wanalala bila neti ndo akaanza kuwa makin

Wa kwanza na wa pili ni wakubwa wapo darasa la tano beki 3 hawez bugia nyama wakamuacha
 
Wahamishe tu weka ukauzu ukiwahurumia ety wanalia utalala nao hadi wawe wakubwa anza leo wapeleke chumba chao wakilia wambie atakae lala kesho namletea zawadi wakigoma wahadithie au wasomee hadithi watasinzia wenyewe, kama napo bado unawajua wanao tumia mbinu unazozijua lakini hakikisha kufikia jumapili wawe wamehama humo jumapili tunasubiri feedback mama wawili
Mkuu watoto mwanzoni wanaogopa Kula peke yao kwasababu ya vitu vya kutisha wanavyo viona mchana kupitia TV au Wanapocheza.
 
Huwa inatumika nguvu kuwatoa, vilio ni kama kunakuwa na Msiba mpk unajisikia vibaya Mtoto anavyolia mlangoni
Mama ndiyo analea watoto na siyo Baba, ukiona watoto wanamuogopa Mama na kumpenda Baba kaa ukijua malezi ya watoto yamekushinda. Mama haitakiwi mtoto kafanya makosa unamwambia ngoja baba aje.
 
Mimi nilivyokuwa mtoto baada ya kuacha kunyonya tu, nilihamia kwangu. Kila mtoto ahame kwa wakati wake...

Anyway, kama hawataki kuhama, hama wewe.
 
Back
Top Bottom