Ulivyokuwa mdogo ulikuwa na ndoto ya kuja kufanya kazi gani?

Ulivyokuwa mdogo ulikuwa na ndoto ya kuja kufanya kazi gani?

Ndoto zangu ziliyeyushwa nikiwa Std 2 baada ya kumuambia mama nataka baadae kuwa hivi, alichonijibu "hivi wee uko timamu au umerogwa ndo akili zako zimeishia hapo? Sasa km ndoto zako za baadae ndo hizo futa haraka kichwani.kwako"

Toka palee nikaanza kupita ktk ndoto wanazotaka wao hadi hapa nilipo. But 1 day ntaishi ktk ndoto zangu.
 
Leo nimekumbuka kipindi nipo mdogo nilikua na ndoto ya kuja kua Miss Tanzania.

Akili yangu yote ilikua inajua Miss Tanzania ni kazi kama daktari, mwanasheria, mwalimu au kazi zingine.

Nilivyofika form 1 ndo nikajua kumbe sio kama nilivyodhani, hapo nikapata mawazo ya kua mwanauchumi mpaka sasa napambania ndoto yangu.

Mliotimiza ndoto zenu nyoosheni mikono juu tuwapigie makofi!😹

"Tangu mdogo nilikuwa na ndoto niishi kitajiri kama John kaboko ,hata mbuyu ulianza kama mchicha polepole namimi yatakwisha" - Q chief - Imma Dreamer.

Nilivokua mtoto primary hivi nilikua natamani kuwa "mwalimu" hii ni baada ya kula fimbo nyingi shule nikawa naona walimu wanafaidi kuchapa so nilikua napenda ualimu kipengele cha fimbo,

Nikawa napenda kazi ya kuuza duka ile exchange ya vitu afu unapewa hela nzuri sana😀😀

Baada ya kujitambua sasa nikawa napenda kuwa Banker, namshukuru Mungu ndiyo nilichosomea ila kazi sasa ndiyo nimeswitch kidogoo,ila fresh tu😧
 
Nilikua natamani kuendesha ile mitambo ya barabarani zile chuma za ujenzi za kushindilia , kijiko nyingine za kusawazisha ! Au kuendesha malori ! Sikuwahi kubahatika leo nafanya vitu vingine kabisa yani 😂
 
Nilivokua mtoto primary hivi nilikua natamani kuwa "mwalimu" hii ni baada ya kula fimbo nyingi shule nikawa naona walimu wanafaidi kuchapa so nilikua napenda ualimu kipengele cha fimbo,

Nikawa napenda kazi ya kuuza duka ile exchange ya vitu afu unapewa hela nzuri sana😀😀

Baada ya kujitambua sasa nikawa napenda kuwa Banker, namshukuru Mungu ndiyo nilichosomea ila kazi sasa ndiyo nimeswitch kidogoo,ila fresh tu😧
Mungu akupe kazi yako!
 
Back
Top Bottom