Uliwahi kuwaza kuua mtu? Hii ndiyo mara yangu ya kwanza kupata wazo la kuua mtu

Ni mtihani sana mkuu.
 
"Ndo siku ya kwanza kulia machozi huku nacheka.Nimemwekea nadhiri moyoni"...[emoji848]
 
Nilipanga kumgonga na gari mtesi wangu, yaani nilikua namvizia njia ya mtaa kabisaa huku nimekunja ndita, ila Mungu si athumani kila nilivyokua nafanya hivyo kile kiumbe kilikua hakikatishi njia ile.
 
Una anger issues, tafuta mtaalamu wa afya. Yasije yakatokea kama ya yule dada wa Kenya, binti wa miaka 24 ambaye ameona kumuua mtoto wake ndilo lilikuwa suluhisho na akaishia kutafuna hadi utumbo wa mtoto.
 
Ukipata nafasi ya kulipa kisasi chako wewe lipa tu kwa kweli hata kama ni Mimi nimekufanyia ubaya. Kisasi kinatesa sana nafsi.
 
Nilitamani kuuwa mtu siku ambayo mama angu anafukuzwa kwenye nyumba aliyojenga na mume wake, Hali hiyo ilitokea baada ya Baba kufa.

Kama sikuuwa kipindi naamini sitakuja kuuwa tena aisee
 
Moja ya vitu naogopa na sipendi mtu anizoee ni cheti Cha form four yaani cheti Cha form four nakihusudu Sana Bora mtu achane Cha ubatizo naweza msamehe lakini sio form four maana nimesoma shule za gharama Sana Hadi form four.
Kila cheti kinapatikana upya, mi huwa sijihangaishi na kitu ambacho naweza kipata tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…