Uliwahi kuzingua kwenye mapishi, iwe ni mara ya kwanza unapika ama ukiwa mzoefu tayari?

Haha,
Maskiini, ukamsingizia malaika wa watu jamani.!
 
Siku moja niko home maza akanipa kazi nipike ubwabwa. Ilibidi nimuite mdogo wangu wa kike ana 9yrs akawa ananielekeza jinsi ya kufanya. Siku hiyo nilikoma maana kalikua kananielekeza kananisema na kunicheka
Haha..!
9 years ndiyo akaendesha mtambo.! Hapo ukute ulikuwa unamuoneaga lazima ujute.!!
 
Hahahahahaaaa..
Nimecheeeeka, eti nikahisi kuna sinema nachezewa na wazee wa kazii.!!
 
Haha..
Muujiza ungekufuata huko uliko.!!
 
Ya mbele ya watu mbona kawaida saana[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Nishawahi kimbia nikawaachia ugali sijui mchele jikoni maana ulikuwa unatawanyika tu[emoji2297]
Hahahaa...
Ukaja kujiteteaje sasa..???
 
Una bahati sana, shukuru mno mzee wako walaqhi'...!!
 
Eti katika kumbukumbu zangu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hakuna kitu kilinisumbua kupika kama egg chop sijui, daah!! Zilikuwa nikiziweka kwenye mafuta zinatawanyika zinakuwa kama chura.
 
Una bahati sana, shukuru mno mzee wako walaqhi'...!!
Mkuu umenikumbusha mbali Sana enzi izo 2010 naenda kureport advanve kusini uko nikafikia kwa bro wangu mwanajeshi nitumie angalau week mbili tatu kabla sijaingia shule, sasa siku nimefika nikakuta kapika fresh Sasa kesho yake akanielekeza mazaga ya kupika yalipo nirekebishe ugali(yeye alikua stand bay) kwenye Sasa sita wakaja wanajeshi kibao pamoja na bro waje wale then waendelee na Mambo yao uko, nikawa nmepika mboga fresh tuu baada ya kuwaona nikawa naweka maji nisonge ugali nikapata kama panic flan, maji hayakuchemka vzuri pia sikuacha uji uchemke, bhana bhna ugali ukatoka mbichi aufai wazee uko wanapiga kelele dogo tunachelewa leta ugali huo. Ili kuuwa so nikafunikua ugali kwenye sinia moja na mboga nikawatengea nikawa pembeni nasikiliza. Daah kama mnavyojua wanajeshi walivyo baada ya kuanza kula tuu kuona ugali mbichi walianza kushusha matusi pale bro akawa anacheka tuu npo apo nataka hadi kulia, waliula wote Ila kwa matusi, bro badae akanambia dogo usipanic ndo kawaida yetu Ila ujifunze kupika. Toka ile siku nilijifunza kupika ugali ulionyooka wakawa kila siku wananisifia balaa hadi Sasa wengine ni washkaji zangu Sana.
 
[emoji38][emoji38][emoji1] Kwamba wajeda walikua wanatukana mmae huyu dogo msnge tu hajui kupika anatupikia ugali mbichi sie wacha tule na hii njaa hakuna namna, ila dogo uache ufaler siku ingine usitulishe ugali mbichi.

Nmecheka sana hii
 
Huu uzi umekuja muda muafaka, iko hivi kuna mboga ile wanaita brocol nadhani basi kiukweli sikuwahi kuiona udogoni mwangu na mkoa niliopo haipo ama sikuwahi kuiona na itoshe kusema niliionea ukubwani kabisa tena youtube kipindi cha mapishi basi siku moja hamaaadii mtaani nikaziona zinauzwa nikanunua na kwenda kuzipika kwa muongozo wa youtube acha niishie hapa mana nachoka kabisaaa kiufupi haikulika nilikua kama nakula mironge yani
 
Naendelea kufatilia najua tu kuna mwanaume wa daslam hachelewi kuja kutoa ushuhuda jins alivyo fundi wa kupika wali nazi
 
Mi nilikua nakamwanamke kangu kupika 0 ila masifa Sasa .Siku moja kalinipikia kisamvu Cha chukuchuku ugali na maziwa mgando.Mchanganuo ulikua hivi ; Kisamvu kilikua Kama upalato wa mtoto .Maziwa Kama maji ya kwenye beseni walioshea watu wenye mikono michafu na yananuka hata ukoroge vipi yanajitenga.Nilivyo mnafiki nikakaambia leo umeniweza mapishi Kama ya mama yangu.Nikaenda kutapikia mbele huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…