Uliwahi kuzingua kwenye mapishi, iwe ni mara ya kwanza unapika ama ukiwa mzoefu tayari?

[emoji38][emoji38][emoji1] Kwamba wajeda walikua wanatukana mmae huyu dogo msnge tu hajui kupika anatupikia ugali mbichi sie wacha tule na hii njaa hakuna namna, ila dogo uache ufaler siku ingine usitulishe ugali mbichi.

Nmecheka sana hii
🤣🤣🤣🤣Kama vile ulikuwepo mkuu
 
Nlilud kazin saa4 usiku,nmechokaaa toop!!!
Nakaingia kuoga,nkakaanga chips
Nkagongea mayai
Sasa ile nigeuze upande wa pili sahani ikateleza
Yakalia pwalaaaaatu chini ,mayai yanalendemka tu
Nkasema pumbav!!! Nkazima jiko nkajitupia kitandan
 
Ndugu, mimi nilizungua mara yangu ya kwanza kupika, na ikawa ndio kama ile ya yesu na wafuasi wake maana siku hiyo nilipozingua nilipika ugali usioiva na mimi pia mdogo wangu tukaula hadi mwisho... baada ya hapo, nikaenda kuchunga ng'ombe, huku nyuma mdogo wangu akakwea mti wa ma maembe, akaanguka, ubongo ukamwagika na kufa pale pale... Siku hiyo siwezi isahau, ilikuwa 24.10.1987. Ugali ule ulikuwa lunch yangu ya mwisho na mdogo wangu- R.i.P
 
Msinikumbushe maana naweza lia.
Kulikuwa na 40 ya marehemu somewhere Ilala. Mie nikajifanya kushika jungu la pilau la mchele wa kilo 15....acha tu, uchawi upo jamani.
Kila nikigeuza pilau, ni kama nimeloweka mchele yaani full bichi, pilau limepiga msamba kila kiungo kipo upande wake.
Kuondoa lawama,nikategua jifya moja...jungu chini, pilau likamwagika hapo ndo ikawa pona pona yangu. Maana nikaaga na kuaga.

Sahv, hata unipe majungu ya kilo 100 napika.
Uchawi kwenye mashughuli upo jamani.
 
Kuna jamaa aliitwaga Dotto wa kanda ya ziwa alisomaga Ulayasi secondary alikuwa anapika msosi mbichi kila siku akawa ana harisha mwaka mzima siku 365 na robo.
 
Hahaha..
Kama nakuona ulivyojikunyata maskiini wakati wazee wa kazi wanakusimanga.! Pole sana ndiyo kukua!;
 
Hahahahaha..!
Eti mironge cheese sana wewe.!
 
Naendelea kufatilia najua tu kuna mwanaume wa daslam hachelewi kuja kutoa ushuhuda jins alivyo fundi wa kupika wali nazi
Haha..!
Siku hizi mpaka wa mikoani tunashindana jikoni..!
 
Hahahahhahahaaa...
We phaller, ni nini lakini..???!
 
Reactions: EEX
Kuna jamaa aliitwaga Dotto wa kanda ya ziwa alisomaga Ulayasi secondary alikuwa anapika msosi mbichi kila siku akawa ana harisha mwaka mzima siku 365 na robo.
Hahaa...
Niacheni hebu bhaana..
 
Good Lord,
Pole sana mkuu jamani..!!
 
Mwezi uliopita tu hapo nilifanya kituko kwenye kupika wali na rost maini. Wali ulitoka bokoboko flani kabisa ila una ladha nzuri tu (mchele wa Kilosa tena)vitunguu vilisaidia flani kuongeza harufu kwenye hii nilijitetea sababu ya kupikia kwenye jiko la gesi. Kwenye maini sasa nyanya kadhaa na tomato paste niliweka yote wakati yale maini yalikuwa nusu mwenyewe najua leo naua kwa diko adimu doh! hiyo mboga kilichotokea balaa tupu. Lengo ilikuwa kumsaidia wife kupika lakini tamati ilikuwa vyote kumwagwa kisha akapika ugali dagaa tukala. Mpaka leo mzuka wa kukaa kitchen bado haupo hata chai sitaki kuchemsha
 
Sikuwahi kupata shida kubwa kwa. Mapishi maana nilikuwa nacheki kwa mama kupita kawaida licha ya kuwa ni mtoto wa kiume nikicheki kitu anapika nikija pika napita mulemule

Siku moja tu nilipika wali kama kilo 5 hivi haukuiva vzr, alipokuja kutest unakaubichi ka mbali akaongeza maji ukaiva sie tushakula hivyo hivyo na kusepa mishe

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…