MONA WA KYEN
JF-Expert Member
- Dec 23, 2016
- 340
- 271
hiyo ni kweli hakuna ubishi naona unanirudisha shule hapanakubali kuwa gas ndio inafanyiwa processing na oil huwa refined BUT still CH4 inaweza kuwekwa kwenye cylinders.... ule mradi unaosua sua kusini wa LNG unadhani ni kwa ajili ya nini???? sawa CH4 ni dry gas but you can liquify it na ukaiweka kwenye mitungi
mkuu nilikuwa na pambana na hali yangu. mimi nipo tu naendelea kazi hizi za ujasilimali wa uchimbaji madini.Sasa nimekuelewa mkuu,, ila ulipotea sana.
sawa mkuu wenye kusikia wameelewahiyo ni kweli hakuna ubishi naona unanirudisha shule hapa
bentonite nitapata wapi mkuunina degree ya Bsc in geology from UDSM. toka nihitimu nafanya uchimbaji mdogomdogo wa madini. na pia huwa natoa ushauri kwa wachimbaji wadogowadogo wa madini.
Una chimba Madini gani na sehemu gani?nina degree ya Bsc in geology from UDSM. toka nihitimu nafanya uchimbaji mdogomdogo wa madini. na pia huwa natoa ushauri kwa wachimbaji wadogowadogo wa madini.
yaaa. zipo. but kitaalamu tuseme hizi zinaitwa njia za kijeolojia na kikemia( uzoefu wa miamba ya madini na utaalamu wa kuangalia sample bila kwenda mabara). yaani. unaenda site ambapo unaona panaudongo ambao unafanana na sehemu zinapopatikana dhahabu. kisha unauchota na kwenda kupiga bangala, chabo au kwa kimobo panning . kama kunazahabu utaziona. ukiziona kwenye udongo huo au mchanga unaweza anza kutafuta sehemu zilikotokea. kama unauzoefu na knowledge ya miamba utafanikiwa kugundua sehemu mwamba zilipo. hii njia nisiseme ya asili bali ni local methodi. na machimbo mengi madogomdogo ya gundulika kwa njia hii. lakini tofauti kubwa wachimbaji wadogo wadogo huwa hawana mission ya kuwa na mikakati ya kutafuta miamba. mala nyingi huwatokea tu na ndiyo maana inabaki kuwa madini ni bahati nasibu.kuna njia yoyote ya asili ya utafiti wa madini kama dhahabu n.k,?
nachimba madini ya dhahaku mkoani lindi. pia niaviwanja vywa jipsum. si hayo tu pia ninaviwanja vya dhahabu geita ambavyo sijaanza kuvifanyia kazi ambako ni nyumbani twetu. pia nilikuwa na chimba gemstoni aina ya malaya garnet huku lindi. na nilikuwa naendesha mladi wangu wa uzalishaji kokoto huku huku lindi. kwa bahati nzuri au mbaya nimeuuza.
Hongera mkuu! Mm nimemaliza mining hapa udsm. Mpango wangu ni kuanzisha crusher na ball mill nyarugusu geita. Unanishauri vipi katika hilo maana una uzoefu wa kutoshanachimba madini ya dhahaku mkoani lindi. pia niaviwanja vywa jipsum. si hayo tu pia ninaviwanja vya dhahabu geita ambavyo sijaanza kuvifanyia kazi ambako ni nyumbani twetu. pia nilikuwa na chimba gemstoni aina ya malaya garnet huku lindi. na nilikuwa naendesha mladi wangu wa uzalishaji kokoto huku huku lindi. kwa bahati nzuri au mbaya nimeuuza.
nafikri nimekujibu. NB sijawahi kuajiliwa toka nihitimu wala sijawahi kupanga kuomba kazi za kuajili. hivyo sina profile ya kwenye migodi mikubwa.
mkuu French.
kwani hii ni tofauti na bentonite clay? alafu kama kuna mtu anauza au ana mgodi aniambie, maana kuna sehem nimepata order. kama yupo ani PM nimpe specification ili tufanye biasharamkuu French.
View attachment 582689 View attachment 582692 View attachment 582693 View attachment 582694
picha za miamba mbali mbali za bentonita
Bentonite naomba nikukumbushe kuwa ni madini yatokanayo na mabadiliko ya mavumbi au macjivu ya volcano endapo italipuka na kutua kwenye maji na hasa maji ya chumvi( sea water). kutokana na halii inaamanisha mara nyingi bentonite inapatikana maeneo ambapo volkano imetokea na ikatua kwenye maji ya chumvi.
kwa tanznia yetu maeno haya ni ya ukanda wa bonde la ufa. hasa la upande wa mashariki. yaani ARUSHA-MOSHI-MANYARA-SINGINDA-KIDOGO NA DODOMA. ukiangalia ukanda huu maji yake ni ya chumvi sana hata maziwa yake kama manyara na natroni.
French
Bentonite inakazi nyingi sana kama kama kufyoza uchafu au langi fulani kutoka sehemu flani, inatumika kwenye petroleum refining as catalysis , kutengeneza plastic na paper etc zipo nyingi sana. but swali lako halijalenga huku.
.Sasa hasa hasa wapi utaipata BENTONITE KATIKA UKANDA HUU?.
French
1. minjingu karibu na ziwa manyara
2.Gelai karibu na ziwa Ntroni
3.Arusha karibu na lake Amboseli
4.Iramba siginda ndani ya bonde lawembere-manonga
mkuu French usitoke mbio kwenda kuanza kuchimba ukapata hasara ukanilaumu bureeeeeeeeee et nimekudanganya. mambo ya madini hatakama ukiambia kuwa ndani ya uwanja wa mpira ule kunamadini. usibebe vifaa ukaanza kuchimba.
unahitaji detail nyingi sana ili kujilizisha mahali exactly yalipo na kina pamoja na kujua ubora wake. kwa kifupi maeneo niliyokutajia huwezi kukosa bentonite.
asante kwa swali kama sijakujibu vizuri unaweza kuniuliza kwa upya tena mkuuu.
Hongera mkuu! Mm nimemaliza mining hapa udsm. Mpango wangu ni kuanzisha crusher na ball mill nyarugusu geita. Unanishauri vipi katika hilo maana una uzoefu wa kutosha
Sent using Jamii Forums mobile app
kwani hii ni tofauti na bentonite clay? alafu kama kuna mtu anauza au ana mgodi aniambie, maana kuna sehem nimepata order. kama yupo ani PM nimpe specification ili tufanye biashara
Sent using Jamii Forums mobile app
Bado nasubili swali jingine. Karibu sanaUmejibu vyema sana nitaendelea kutuma maswali kama nitakuwa na la kuuliza...... Asante sana
Wana JR uliza swali lako lolote kuhusu madini, mafuta na gas, kuanzia njisi yanavyojitengeneza ardhini, kufanyiwa utafiti, kuchibwa hadi kuuzwa nawe utajibiwa na mtaalamu wako hapo.
Mkuu Mimi swali langu ni hivi kwa mtu ambaye hajui kabisa kuhusu madini je inachukua muda gani kujifunza hayo mambo ya madini na kuanza kufanya hizo kazi?na je anatakiwa awe na mtaji kiasi gani ili aingie porini na kufanya hizo projects Kama unazozifanya wewe(uchimbaji mdogo)?Uliza ujibiwe
Mkuu asante sana kwa swali lako.Mkuu Mimi swali langu ni hivi kwa mtu ambaye hajui kabisa kuhusu madini je inachukua muda gani kujifunza hayo mambo ya madini na kuanza kufanya hizo kazi?na je anatakiwa awe na mtaji kiasi gani ili aingie porini na kufanya hizo projects Kama unazozifanya wewe(uchimbaji mdogo)?
Mkuu asante kwa swali lako ila maomba unifafanulie swali lako vizuri.Nipe formation ya dhahabu inakuwaje had I kujitengeneza ardhini, na kwanini dhahabu ya njombe inatofautiana process take ya upatikanaji na ya mbeya,kahama etc.
Mkuu nashukuru sana na nakupongeza kwa kujibu maswali kwa uweledi wa hali juu.Mkuu asante sana kwa swali lako.
Kwanza kujihusisha na project za madini siyo lazima uyafahamu kwa kitaalamu. Kwa maana hii unatakiwa kujua soko na aina ya madini yanayohitajika. Kwa maana hii unahitaji kuwa na mzoefu au mtaalamu atakayekuongoza katika biashara hii. Wapo wataalamu wa uzoefu na wa kusomea kisha wakapata na uzoefu katika madini hayo. Mkuu wataalamu wakusomea wako katika ngazi za cheti (miezi 3-mwaka1), diploma (miaka 2-3)na degree (miaka 4) na vyuo vipo hapa tanzania na nje ya hapa. Elimu ya madini imegawanyika katika vitengo vitatu
1. Utafiti (exploration)
2. Uchimbaji (mining)
3. Uchenjuaji (processing)
Napenda kukujuza kuna aina za madini zaidi ya 2000, ambayo yamegawanyika katika makundi mbalimbali (hili ni somo kubwa sana) lakini unaweza chimba aina moja ya madini na ukatajirika.
Pili swala la mtaji
Biashara ya madini ni biashara yenye highest risk sana, ndiyo maana unasikia alienda hana mtaji na karudi na mamilioni na wengine wanaenda na mtaji wanarudi mikono mitupu, hii inatehemea mtaalamu wako au uzoefu wako katika namna ya kuwekeza. Hivyo kama wewe ni mgeni kabisa unahitaji kukaa na mzoefu kisha umwambie unakiasi gani na yeye akueleze kulingana na mtaji wako utawekeza katika namna ngani, ukiona mtaalamu wako amekueleza vizuri then unaamua. Kama wewe ni mgeni ukiingia kichwakichwa utapoteza pesa zako bure.
Madini ni yetu tuyachine yatunufaishe,
Kama unashauku ya kujua zaidi karibu uulize tena mkuu.