Commonwealth imetoa maelekezo yanayohitaji utekelezaji sio majadiliano wala maridhiano kama ya Chadema, ni amri.
Anatakiwa achague moja,
1. kumwachia Lissu au
2. kuendelea kumshikilia.
Samia akiamua kumwachia ataonekana dhaifu, muoga kitu ambacho wapambe na chawa wake hata yeye hataki ionekane hivyo.
Akiamua kuendelea kumshikilia, Tanzania itakuwa kwenye hatari ya kuvuliwa uanachama, kufutwa kwa misaada yote iliyokuwa inatolewa na jumuiya ya commonwealth.
Chaguo ni moja, kuonekana dhaifu au kufutiwa misaada.
COUNTDOWN, leo zimebaki siku 28 za maamuzi.
Ndani ya CCM na vyombo vya ulinzi na usalama kumejaa manguchiro, ndezi, na kenge-mijusi. Yaani pamoja na yote haya ambayo taifa linayapitia hivi sasa, lakini bado wao wanaona wamejaa upofu akilini mwao, na kuhisi ni vyema kabisa kushikamana na kumuunga mkono kiongozi wao kilaza, dhaifu, na dhalimu.
Pamoja na kuifikisha nchi hapa ilipofikia hivi sasa kisiasa, kiuchumi, na kijamaa, lakini wao wanaona bora tu liende huku kikundi kidogo ndani ya chama kikifaidika na mema yote ya nchi pamoja na ndugu, marafiki, na jamaa zao wa karibu.
Maalaiki ya vijana wa CCM, UVCCM, Green Guards, na machawa, pamoja na kuishi katika lindi kubwa la ufukara na kutopea katika umaskini wa kutupwa, lakini wao bado wamejitoa ufahamu na wamegeuka kuwa ni mazuzu ambao wamekosa hoja na kuamua kusheherekea udhalimu na ufedhuli unaofanywa na watawala wachache kupitia matumizi mabaya ya madaraka waliyoyatwaa kwa njia haramu.
CCM imechoka, imedhoofu mno, na imekosa uhalali wa kuliongoza Taifa letu. Kitu pekee inachokitegemea hivi sasa ni kupitia mbeleko ya vyombo vya dola, hasa kwa kuungwa mkono na viongozi wasiojitambua wa Jeshi la Polisi na TISS. Muda unakuja hata navyo vitaigeuka na kuamua kukaa upande wa wananchi wengi wanaojielewa.