Umeshawahi kukata tamaa ya maisha? Ipi ilikuwa sababu

Mimi nilikuwa na ups and downs nyingi sana lakini sijawahi kushika panga au kisu kukata tamaa. Kitu nilichobarikiwa ni kwamba niligundua mapema sana tangu niko O'level kuwa mimi ndio boss wa maisha yangu. Ngumu sana kuzaliwa na kukua kwenye judgemental societies kama ya Dar es salaam lakini mwisho wa siku I won 🏆
 
ndio kitu napitia bado siamini lakini kwa comment yako nimepata nguvu
 
Since 17 life ilikuwa mbaya sana #nilipotez parents backtoback nikakosa ada.
# At the same time Nikagombana na ndg .
#Nilikonda sanaa hadi wakasema ni positive.
sikuwahi fikili mwili wangu utarudi tena.
# from 17 to 25 ni financially broke.
#niliyekuwa nampenda akazingua.

26, mungu ni mwema nimejiari now mambo yako good i feeel kufufuka mwili umerudi now nguo zote zinanibana . this yr is myn.
 
Wakuu mnawezaje kukata tamaa? Mimi huwa naona kila jambo linatokea/linakuja katika maisha ya mwanadamu kwa kusudi maalumu. Na kanuni ya maisha ni kwamba baada ya Kiza ni Nuru,baada ya Nuru basi Kiza hufuata.
Ni kawaida tu ya maisha,ni kama majira ya mwaka au siku,so tunapokutana na mitihani mikubwa katika maisha yetu basi neema/baraka kubwa zinafuata.

Pia kuna jambo ambalo wengi hatulizingatii,hapa nazungumzia kujinenea/kujitamkia mema. Wakuu hata iweje usijitamkie mabaya,jinenee yaliyo mema.

Mimi maisha yangu yanashangaza sana na yanatisha kwa mtu ambae atakua hajazoea changangamoto. Nina mitihani ya kimaisha mpaka kuna jamaa huwa ananiuliza nawezaje kuwa ni mwenye furaha muda wote licha ya mitihani ninayopitia.
Sijawahi kukata tamaa,simtupii lawama mtu yeyote kwa yanayotokea katika maisha yangu,huwa naacha nature ifanye kazi yake,na majibu ya matendo yao huwa wanayapata.
Wala huwa sitafuti sababu ya kujilaumu kwa jambo lolote lile,hata nikipoteza nachukua walau funzo tu katika kile nilichopoteza.

HAKUNA KUKATA TAMAA!! SIMAMA IMARA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…