Hypersonic
JF-Expert Member
- Apr 14, 2012
- 996
- 1,913
Mimi sijazaliwa hospitali nakukulia kwenye mitaa yenye vibao vyenye majina, nimezalia nyumbani kijijini, nimetumia maisha mengi toka nkiwa mtoto mdogo mpaka kijana nimetumia maporini nikichunga mifugo, hakuna nyoka ambaye sikuwahi kudeal naye kwa mazingira ya huko kwetu, ukiona comment yangu inejikita kwenye comment ya black mamba na Cobra. Kifupi nyoka, wanyama kama chui,simba, nyati na tembo tumedeal nao mno. Na wajua vizuri sana kwa elimu yetu ya asiliWengi mnachanganya mafaili hapa. Mmeishi mkiua cobra (ambaye hata bibi kizee mmoja akitia bidii kidogo tu anamuua)huku mkiamini mliwaua black mamba. Koboko havimbi taya na hauawi kirahisi namna hiyo.
NB: Usiwachukulie poa wanyama jamii ya paka kwenye mishe zao ukasema tu "...aaah kaweza paka nishindwe miee?". Wewe hapo ukijifungia ndani upambane na paka mwenye afya yake ya mwili na akili hutoamini balaa lake pamoja na fimbo yakoπ. Njia salama kumuua mnyama wa jamii hiyo ni kumnyemelea akiwa hana habari.
Hahahaah kwahyo amekuwa mbwa tena mkuu.Yule mbwa hafai kbs staki hata kumwona
Huwa unaona umakini wanaotumia wakipata case ya koboko?.Hawana lolote kuna wale wa south mtu na mkewe wanawakamata kama panya tu wanawaweka kwenye mfuko, haya mambo ya koboko yamekuzwa sana japo ni nyoka mkali sana.
Yeah koboka ni nyoka anajiepusha na binadamu kuliko kawaida ,ndio maana akibananishwa ana react aggressive mno kujihami.Huwa unaona umakini wanaotumia wakipata case ya koboko?.
Mkuu pamoja na huo uhatari unaongelea hebu elezea madhari mabaya ambyo yamewahi kutokea kwenye jamii. Kila jamii inajua sana kudeal na hao vimbe achaneni na stori za kizungu hakuna nyoka hatari kwa jamii za kiafrika. Mtoto anazaliwa mpaka anazeeka anapishana nao itakuwaje asijue namna ya kupambana nao. Hizo ni stori tu. Niliamia Kibaha huko nikakuta kuna stori za nyoka anaitwa sijui Msanga, siku nimepambana naye niliona ni wa kawaida sana. Hivi vitisho wanapokea wale walizaliwa na kukulia magetini. siyo sisi wachunga ngo'ombeWale koboko wa Nat Geo watakuwa wanaugua mshipa wa ngiri, si kwa udhaifu ule.
Koboko tulionao huku si mafala, hata wanakijiji wanaochunga mifugo na kufanya shughuli zao maporini tu wanawaheshimu, na ikitokea wanamuwinda basi kuna process za kijadi wanazifanya kwanza na wanakuwa serious nazo kweli. Leo hii watu wapo huko Mbezi na Manzese darajani anasema ni wepesi kisa kaona Nat Geo. Nakataa kabisa kuwa koboko ni nyoka mpole.
Nyoka ninayefahamu ana sumu hatari lakini ana uboya mwingi ni cobra. Hao nimewaua wengi na wakubwa kirahisi tu nikiwa dogo. Wao silaha yao kuu ni kurusha mate. Ukiwa makini tu kwenye kukwepa mate yake unammaliza kirahisi maana ana ubonge fulani hivyo ni mzito. Lakini black mamba kinachomfanya kuwa hatari zaidi ni mwili wake wa mazoezi na speed yake kali sana (ndiye nyoka mwenye speed zaidi kwa mujibu wa tafiti). Kwahiyo wapuuzeni tu hao wanaosema ni rahisi kumuua maana uwezo wa kukwepa na kushambulia kwa haraka anao wa kutosha. Huyo hutoki tu mtu mmoja na kushika fimbo kindezi eti unaenda kumuua akiwa mkubwa kama unavyomuua cobra, lazima mjadili na majirani kadhaa kama si ubalozi mzima, mikakati ipangwe na tahadhari zichukuliwe, la sivyo maturubai yanaweza kutundikwa kama utani tu.
Umemjibu vyema .Mimi nilikutana naye kwenye kitabu cha kiada nadhani upatu shujaa Alisha Fanya mamboNakutana nae kwenye maandishi kama hivi
Eti unaweza kuishi nae ndani, amekuwa diwani wa chaumma huyo? kwanza unakutana na kichwa sura ya jeneza kuta za mdomo nyeusi tii kama amekula mkaa, mnakutana kwenye mandoo ya maji usiku, em niambie utaanzaje kujieleza yaani utamfafanuliaje kuwa hapo ni kwako mpaka akuelewe.Nmesoma quora ulipoona pia nmesoma uko uko quora kwa watu wanaishi na black mamba zimbabwe mwamba kwa macho yake kaona mtu anakimbizwa na black mamba na anachezea kichapo au uliza wasukuma wa tabora wakuhadithie koboko alievurugwa akiingia kwa kundi la ng'ombe hutenda nini ?
Ila kwa kua umeamua kuwasikiliza Nat Geo endelea tu maana hao hao experts wako walikua wanasema boomslang hana sumu, na baadae wakaja kugundua otherwise ila wanaoishi na hayo majoka hawaaminiki sababu hawana phd
Wale mwisho wao ni kugongwa na nyoka. Unachokifanya na kukizoea ndio kitakuua mcheki hamisi dereva wa pikipiki za mashindano pale MorogoroHawana lolote kuna wale wa south mtu na mkewe wanawakamata kama panya tu wanawaweka kwenye mfuko, haya mambo ya koboko yamekuzwa sana japo ni nyoka mkali sana.
Koboko akiwa mdogo anakuwa na rangi ya kama ya brownish gray. Kadiri anavyoongezeka umri rangi inakolea na kuelekea kama kwenye weusi, japo sio mweusi kabisa! So, ni kweli, koboko aliyekomaa anaonekama kama mweusi.Hakuna black mamba mweusi kwa taarifa yako
Hata wewe muongo.muongo..koboko kwanza hatemi sumu..pia havimbishi kichwa..yule uliyemsema mwanzo ni spitting cobra(swila)..na hao Nat geo wild kama ndio walikufunza hivyo kadai ada yako au kawashitakiNimechanganya kuhusu kuruga rusha sumu tu.....
Wakuu dunia ya leo tumekwisha toka kwenye myth za kudanganyana toka utotoni kwamba Koboko anafukuza watu sijui anau ng'ombe zizi zima just for no reason au amekasirika
Google it
Ask Ai
Kaulize Quora
Nenda Youtube
Achana na habari za "nasikiaga" au kuna jamaa aliniambiaga
Hakuna nyoka dunia anakazi ya kufukuzana na binadamu labda wale wanaoweza kutufanya chakula...... The rest wata kukwepa na ukimbananisha sana atakushambulia
Kuna video niliona koboko aliingia ndani akakaa chini ya fridge wakaitwa jamaa wa maliasili akaweka rifle usawa wa pale maana yule koboko alikuwa mkubwa amejaa kule chini, akachanwa chanwa katikati na ile risasi uti wa mgongo ukavunjika, sasa speed aliyotoka nayo huko chini kwanza kulikuwa na taulo akaliteremshia bite za kutosha kisha akageuka kwa kasi ya ajabu kulia na kushoto mwa fridge kutafuta muhusika ni nani?.Hayo ya Nat Geo Wild nashauri uyaache huko, lile onyo la WWE hapa linafit vizuri kabisa "don't try this at home, at school or anywhere". Usije kujaribu kumkamata nawe umweke kwenye mfuko na utarajie kumwacchia akimbilie porini, atakushangaza.
Achana na hao black mamba wa huko kwenye TV wanakuwa kama pets, hawa wa huku Kagera, Tabora, Kigoma nk kwanza wanatumia bangi kama chakula chao cha mara kwa mara.
Ninafahamu matukio kibao yaliyofanywa na koboko. Jambo ninalofikiri hao nyoka kadri wanavyokua wanaingiwa na kichaa, maana matukio yote ninayoyafahamu ni koboko wakubwa (wazee).
Huyo alikua ni moja ya vikatuni kwenye gazeti la saniNini maana ya Kaboka machozi?
Niliwahi kulisikia neno hili miaka ya nyuma
Huwa sometimes anakosea anajiparaza mwenyewe kwa meno yake baada ya muda anakufa.Ndio nyoka kidume pekee niliyemuona akiwinda panya kwa kufukuzia na akamshika
Suzy na Simon, wanazunguka mabara yote, majiji mbalimbali kuwinda na kukamata nyoka hatari ktk makazi ya watu, na kuwatibu kama wameumia, kuwauuguza na wakipona wanawarudisha porini πKuna yule jamaa na mke wake kule south Africa wale watu ni binadamu kweli? wale wana matatoo mwili mzima na mabangili banging, mke sijui ana nywele za orange, wanawashika koboko kama nyoka wa bandia aisee.
Hahahah hawa hawa mkuu, hivi hawa jamaa wako normal kabisa?.Suzy na Simon, wanazunguka mabara yote, majiji mbalimbali kuwinda na kukamata nyoka hatari ktk makazi ya watu, na kuwatibu kama wameumia, kuwauuguza na wakipona wanawarudisha porini π View attachment 3445298
Wewe unataka tufanyeje boss wewe kama weweWewe nahisi unazungumzia Tom and Jerry, eti unajihami kwa kufanyaje?.
Wako normal, ni professional snake handlers, na ni kazi inayowapatia kipato kikubwa, waanahusishwa kwa uhifadhi na tafiti za taasisi za kutengeneza madawa/snake antidotes (snake antivenom), pia wanapata oder ya ku-supply sumu za nyoka za spishi mbalimbali kwa taasisi za kimataifa zinazotengeneza antidotes na chanjoπHahahah hawa hawa mkuu, hivi hawa jamaa wako normal kabisa?.