Umoja wa Mataifa (UN): Kumbukumbu ya Hayati Dkt. John Magufuli
Salama Wana Mapinduzi wa JF?

Ndugu zangu huko Duniani kwa sasa ni Viongozi wa Dunia wanavyomuenzi Mpendwa Wetu Hayati John Pombe Joseph Magufuli kwa kuelezea Uimara na Misimamo Yake thabiti katika Kuunganisha Taifa Letu na Mapinduzi Makubwa ya kiuchumi.

Link hii hapa chini karibu tufatilie uchambuzi yakinifu unaofanywa kumhusu Mpendwa Wetu JPM.

[emoji116]


Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa maarufu kama Baraza la 75 kukamilisha mkutano wake maalum uliolenga kumkumbuka na kumuenzi Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17 na kuzikwa Machi 26.

Baraza hilo limechukua hatua hiyo kutambua mchango wa Dkt. Magufuli aliyekuwa kiongozi wa nchi mwanachama miongoni mwa nchi 193 wanachama wa Baraza hilo la Umoja wa Mataifa.

Rais wa Baraza, Katibu mkuu na wenyeviti wa makundi matano yanayounda Baraza ambayo ni Afrika, Asia na Pasific, Ulaya Mashariki, Ulaya Mshariki, Amerika ya Kusini na Karibea kushiriki mkutano huo akiwemo mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa (UN) Balozi Prof. Kennedy Gastorn jijini New York, Marekani.

Akihutubia mkutano katika kumuenzi Hayati Magufuli, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Gutteres amesema, katika kumkumbuka kiongozi, UN itaenzi jitihada zake za kusimamia upatikanaji wa huduma za kijamii na mapambano dhidi ya rushwa.

Ameongeza kuwa aliyekuwa rais hayati Magufuli alijijengea umaarufu katika maendeleo ya miundombinu na viwanda ambayo ni dhana muhimu katika kukuza uchumi sambamba na kufanikisha nchi yake kuingia kwenye nchi zenye uchumi wa kati kabla ya kipindi cha makisio cha mwaka 2025.

Aidha akiendelea kutoa sifa za kiongozi huyo aliyedumu kwa miaka mitano na miezi michache madarakani, Guterres amesema, hayati Magufuli aliwezesha kuongeza idadi ya wanafunzi wapya kujiunga na shule za sekondari sambamba na kuboresha uwezo wa upatikanaji wa nishati ya umeme nchi nzima.

"Kwa niaba ya Umoja wa Mataifa, kwa mara nyingine tena ninapenda kutoa pole kwa familia ya Rais, Serikali na Watanzania kwa jumla. Tunatambua historia ya ushirikiano uliotolewa kimataifa na kikanda, na ninachukua nafasi hii kusisitiza na kurudia tena kusema Umoja wa Mataifa tutaendelea kufanya kazi kwa karibu na Rais wa sasa Samia Suluhu Hassan na tunasimama na wananchi wa Tanzania katika kuendeleza na kusaidia mafanikio ya kimaendeleo kwa Watanzania wote.

Ni utaratibu wa kawaida.MATAGA msifurahie
 
Cardinal alisali nae...
Akaanzisha nyimbo... na kuongoza ibada ya kawaida before kufa..

Ndugu wa marehemu said all that.

Sasa hukumu zenu wajukuu wa ibilisi mbaki nazo wenyewe[emoji16][emoji16]
Padre alienda akakuta mzoga tayari, hakumkuta meko.
Meko kaikosa mbingu hivi hivi yani, kafika tu jehanamu wale jamaa waliokuwa wanaungua kwenye tanuru wakaanza kumuita "kiongozi" "kiongozi"
 
Unapingana na mabeberu?
Umoja wa mataifa una watu wenye akili. Ingawa Magufuli aliwaita mabeberu, wao wanaangalia substance kwenye uongozi wake siyo jinsi alivyowaita wao.
 
Padre alienda akakuta mzoga tayari, hakumkuta meko.
Meko kaikosa mbingu hivi hivi yani, kafika tu jehanamu wale jamaa waliokuwa wanaungua kwenye tanuru wakaanza kumuita "kiongozi" "kiongozi"
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 jamani nimeshindw jikaza nimecheka kwa nguvu🤣🤣🤣
 
Hapo Tundu Lissu na genge lake ,Kigogo 2014 na wauwaji wenzake kimewauma.hahahahaaa
 


Alafu kuna wajinga watatu Assad. Lema na Lisu wanatokwa povu kutuaminisha kwamba Magufuli alikuwa zero tu.

Haya sasa hata mabeberu yanayowalea Ulaya yamewakana sasa, yamesema rais Magufuli alikuwa kiongozi mwenye maono na mwenye mapenzi ya kweli na nchi yake.

Ameishakufa hata wakimsifia haisaidii, Wala hana madhara kwa mabeberu hata wakimsifia.
Watu wa ccm chenga sana, wazungu wakiwskosoa mnawaita mabeberu! wakiwasifia mnapiga makofi
 
kama memba wa jumuia hiyo anayo haki ya kukumbukwa,si nchi ilikuwa inilipia ada ya uanachama!

halafu hakuna sehemu hao unaowanaga waliwahi kusema kwamba kabla ya umauti ,un haitamkumbuka.

ameshakufa,ilo ndilo la msingi.
 
Ukitaka kujua watanzania Nani mwerevu na Nani mpumbavu soma hii mada.
 
Kinuju
Una elimu gani ndugu, ulisoma wapi, mitihani ulikuwa unafaulu au unaingia na majibu ndo ufaulu?
Unashangilia Magufuli kuombolezwa na MABEBERU tena ?????
 
Back
Top Bottom