Una maoni gani kwa matokeo haya ya kidato cha pili Shule ya Diplomasia inayopatikana Dar?

Una maoni gani kwa matokeo haya ya kidato cha pili Shule ya Diplomasia inayopatikana Dar?

Tena sio uongo, unakuta boda au bajaj anazurura na mwanafunzi kutwa nzima.

Kuna siku nlikua natoka home naenda sehem, ilikua mchana, sasa niko njian natembea bajaj ikasimama nkapanda,

Nkamkuta mwanafunz wa kike ndan, punde anaanza kulalama "wee fulan unachukua abiria kwan tulikubalianaje?, we c ulisema leo tunashinda wote?" Jamaa akadakia "huyu namjua hana noma ndo maan nimemchukua namdrop had hapo mbelee"

Nilimuangalia yule mwanafunzi kwa jicho bayaa, uvumilivu ulinishinda nlianza kumsema yule mwanafunzi kwa ustaarabu, eti na yeye akajifanya kuanza kupanick n kunichamba, nkasema hunijuii wee nilimchambaa na kumchambua had akabaki anainama chini kwa aibu,

Na hatonisahau, baadae nkamuambia yule jamaa Leo unamchezea akipata mimba unamkana humjui ila unashinda nae kutwa nzima.

Yule jamaa akajibu, "sio mimi yeye ndo anataka, muda wa kuwa shule anataka kuwa na mimi, nifanyeje."
Nilichokaa.
Embu assume ishu kama hii mwalimu anafundisha mke wa mtu!

Aseeee yaani hapo toto hata ulifundishe vipi haliwez khelewa linawaza lirud kutumikia ndoa
 
Unafahamu unachokiongea au wafurahisha genge tu hapa?

Hiyo shule asilimia 98/9 ya wanafunzi wa pale wanaishi nje ya Kurasini. Hawa anzia kwa Aziz Ali ambao bado ni wachache mno wanaoishi hapo, kuendelea mpaka Kisemvule.

Hii shule kimsingi, mazingira ya ile shule ni magumu mno kuanzia kwa walimu wenyewe mpaka wanafunzi. Shule hii unakuta wana mikondo mpaka 7 au 8 na kila darasa unakuta lina wanafunzi 100+ na walimu ni wachache mnooo! Hili la uvutaji bangi kwa wanafunzi na vurugu za hapa na pale ni kiasi kidogo mnoo ila kiuhalisia serikali yatakiwa kujifumua mifumo yake ijidhatiti kwenye elimu.

Kuna mdau kazungumza swala la usafiri, ninamuunga mkono kwa asilimia zote zitakiwazo, wanafunzi wa hii shule na ile ya Uhamiaji majirani zao utawakuta wako mtaani saa 2.30 asubuh au wanakula mihogo kwa wauza mihogo mazingira ya jirani na eneo la shule wakiwa wanategea muda wa break waingie darasani. Mara kadhaa nimekuwa nikizungumza nao hawa watoto kutaka kujua kinachowachelewesha, sababu zao zimekuwa ni moja, TAABU YA USAFIRI UNCLE. Ukiwa unaufahamu mtiti wa usafiri wa Mbagala na viunga vyake kwa asubuhi na jioni utanielewa, na kibaya zaidi wazazi wa wilaya ya Temeke huwa sio rahisi kugombelezea wanafunzi kwa makondakta wafike shule mapema tofauti na wazazi wa huu upande wa Kinondoni na Ilala
Fundisheni vizuri mwalimu acha visingizio
 
hiyo shule ina wanafunzi wa temeke mikoroshini,mtongani,mbagala kusema kweli ni wahuni ukipanda nao kwenye dala dala ni story za kijinga hakuna shule hapo nidhamu ni mbovu na nahisi watakuwa wanahishia beach
 
Shule za daslam za serikali na elimu wapi na wapi?🤣🤣watu wanashinda stend za mabasi kutwa nzima
Walimu nao wako busy na miradi binafsi
 
Ukitaka kuchangamsha shule kama hiyo hakikisha inapata waalimu wa Hesabu na Physics wanaopenda kazi yao (dedicated) na wakutosha; Sio wale wa kuunga unga wanao waambia wanafunzi eti Hesabu/Physics ni ngumu. wakifanya hivyo, miaka mitatu ijayo inageuka na kuwa shule ya mfano
Kumbuka; watoto wakifaulu Hesabu na Physics hufaulu na masomo mengine; waalimu watanielewa
Siku hizi hawapo ,,wengi wanakaa vituoni masaa 4 mengine kwenye mishe mishe ,, serikali inazingua maokoto hivyo wanaingia chimbo kubalance
 
Shule yenyewe ni ya wavaa makobasi! Elimu dunia sio kipaumbele! Mnawalazimisha! Wana wa mnyaaazi mungu!
Wewe ni mpuuzi kuliko upuuzi wenyewe. Dini ya kuletewa imekufanya uwe mjinga square maana umekuwa kipofu.

Hiyo shule ni ya serikali 100% lakini umeingiza udini wa kipumbavu kushambulia pasipo hata kuangalia registration number ya shule kama ni private ama government.
 
sababu kubwa shule za Dar kufanya vibaya mfano zilizopo maeneo ya Temeke, kuna Msimbazi wanavaa blue bahari, kuna chanika na nyingine ipo bunju ni ya kata.

1. Utandawazi; hii ni sababu moja kubwa ya watoto wengi wa dar kufeli. Hili linasababishwa na usimamizi mbovu wa wazazi kwa watoto wao wakiwa busy kukimbizana na maisha, watoto kuingia kwenye starehe za mapema, kuangalia video za ngono.

2. Serikali; maisha ya dar ni magumu, kada hii ya ualimu imesahaulika, miundombinu Mibovu, hakuna Hamasa kwa kwa walimu kufanya kazi kwa asilimia zote wanafanya bora liende.

Nimeona mtaala mpya mambo mengi sana, lakini kama serikali haitajitahidi kuboresha maisha na masilahi ya walimu hatutaona mabadiliko.

Wizara husika waliangalie hili suala kwa kina, usitegemee ukafanya vitu kwa njia ile ile ukategemea matokeo tofauti.
Hakuna shule za mikoani nje ya Dar zinazofanya vibaya zaidi ya Dar?

Kuna shule huko mikoani wanafunzi wawili wana division four halafu 400 wana zero.
 
Back
Top Bottom