Unadhani kwanini vijana wanapenda sana kuajiriwa serikalini kuliko kampuni binafsi?

Unadhani kwanini vijana wanapenda sana kuajiriwa serikalini kuliko kampuni binafsi?

lazima ukae

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2013
Posts
791
Reaction score
414
Je, nini mtazamo wako juu ya wahitimu wengi wa vyuo kupenda kuajiriwa serikalini ilhali kampuni binafsi ndio zinazoongoza kwa kulipa mishahara minono?

Mtu yuko radhi kuacha kazi kwenye kampuni binafsi yenye mshahara wa 1.5M na kwenda kupoke basic salary ya 900k serikalini

Je ni job security au fursa za mikopo ukiwa unafanya kazi serikalini?

Au kuna sababu nyingine ya msingi inayopelekea vijana kupenda kuajiriwa serikalini?

Embu
 
Kampuni nyingi za watu binafsi ubabaishaji mwingi, mishahara ni mikubwa kwenye makaratas ila kiuhalisia hadi upate mshahara hesabu trh za 40 hadi 50. Pia serikalini unafanya bila pressure kubwa na unalipwa vitu vingi kama Likizo na usafir, bima za afya kwako na familia yako za uhakika, semina nyingi na unaweza kwenda kujiendeleza kielimu kwa kusomeshwa na serikali.
 
Serikali hamna kubanwa banwa pressure ya kazi sio kubwa na hamna kazi kiviile tofauti na watu wa private wanafanya kazi Sana pia serikali Kuna uwezekano wa kupata vihela vya hapa na pale
 
Wakati mwengine sekta binafsi mvutano mwingi, malipo ubabaishaji, mikopo hakuna. Na kingine sekta binafsi upige Kazi Kweli na siyo bla bla kama serikalini, sekta binafsi ukizembea tu ni rahisi kukubalasa, akaletwa mwengine. Lkn serikalini presha hakuna.
 
Comfortability. Tunapenda comfort zone kinoma.

Mtu yuko radhi akalipwe take home ya laki nane serikalini anaacha milioni nne kule Roche au GSK kisa security.

Ukifanya kazi private “za maana” ni opportunity ya kulevel up na kupata madili ya maana huko mbeleni.
 
Back
Top Bottom