Unajua Mungu aliumbwa na nani?

Vipi kuhusu watu wanaozaliwa vipofu macho yao hayawezi kutazama na kutofautisha rangi ?

Je hao wana kosa gani? Ama kwa sababu gani wameumbwa hawajakamilika kama wenzao
Zipo sababu zaidi ya moja mtu kuzaliwa kipofu
 
Wewe unayesema ni Mungu kaweka, unatakiwa uthibitishe. na ukithibitisha beyond doubt, Mimi nitaamini na kumuabudu.

Lakini kama ukishindwa kuthibitisha, Tusiseme ni Mungu bali tuseme ni hizo mechanisms.
Mkuu usiniwekee maneno ambayo sjayaandika, hakuna mahala nmesema Mungu ndo kaweka hizo mechansms, ila nimekuuliza ''nani ameziweka hizo mechanisms''?
 
Kwanini kuhoji dhana yenye utata kuhusu mungu iwe ujinga,?

Ujinga ni nini?
Hoja ya kawaida kutoka kwa wakanamungu na wenye wasiwasi ni kwamba ikiwa vitu vyote vinahitaji sababu, basi Mungu lazima pia ahitaji sababu. Hitimisho ni kwamba ikiwa Mungu alihitaji sababu, basi Mungu si Mungu (na kama Mungu si Mungu, basi bila shaka hakuna Mungu).

Hii ni aina ya kisasa zaidi ya swali la msingi "Ni nani aliyemfanya Mungu?" Kila mtu anajua kwamba kuna kitu hakitokani na kitu chochote. Kwa hivyo, ikiwa Mungu ni "kitu," basi lazima awe na sababu, sivyo?

Swali ni gumu kwa sababu linaingia katika dhana ya uwongo kwamba Mungu alitoka mahali fulani na kisha anauliza hiyo inaweza kuwa wapi. Jibu ni kwamba swali halina maana hata kidogo. Ni kama kuuliza, "Bluu inanuka nini?" Bluu haipo katika kundi la vitu ambavyo vina harufu, hivyo swali lenyewe lina kasoro. Kwa njia hiyo hiyo, Mungu hayuko katika kundi la vitu ambavyo vimeumbwa au kusababishwa. Mungu hatumiki na hajaumbwa—Yeye yupo tu.

Tunalijuaje hili? Tunajua kwamba kutokana na chochote, hakuna kinachokuja. Kwa hivyo, ikiwa kungekuwa na wakati ambapo hakukuwa na chochote kabisa, basi hakuna kitu ambacho kingewahi kutokea. Lakini mambo yapo. Kwa hiyo, kwa kuwa hakungekuwa na kitu kabisa, kitu kilipaswa kuwepo kila wakati. Kitu hicho kilichopo daima ndicho tunachokiita Mungu. Mungu ndiye Kiumbe asiyetumiwa ambaye alisababisha kila kitu kingine kuja kuwepo. Mungu ndiye Muumba asiyeumbwa ambaye aliumba ulimwengu na kila kitu ndani yake.
 
Kuna hizi bangi matoleo mapya ni mtihani sana, ile ya zamani ukivuta mapushabu nayo mtihani sasa kuna hizi za sasa wanaita bongo_shit, na matoleo yake ndio yanayofanya hivi watu
 
Mkuu usiniwekee maneno ambayo sjayaandika, hakuna mahala nmesema Mungu ndo kaweka hizo mechansms, ila nimekuuliza ''nani ameziweka hizo mechanisms''?
Sasa kumbe tunabishana nini sasa?? Maana mimi sijamleta Mungu na wewe hujamleta..
Au hapa ulimaanisha nini??
5. Fikiria unakula ugali mwili unatenganisha kinachohitajika na kisicho hitajika kinatolewa kama kinyesi halafu unasema hakuna mungu.
Tafakari kijana
 

MUNGU amekuwepo duniani hata kabla ya ujio wa dini.
Waafrika walimuabudu Mungu hata kabla ya ujio wa hizi dini.Do and don't do yaani sheria za asili mfano usiue,usiibe,usiseme uongo ndio hizo hizo zilizopo kwe amri kumi za Mungu.Mwafrika ashiki dini wala kuongozwa na dini thus ana matatizo kibao.

Dini ndio asili chanzo cha maendeleo na ustaarabu kwa nchi za Ulaya na uarabuni. Mwafrika angeshika dini hata 40% angekuwa na maendeleo makubwa sana SAwa na zilipoanzia dini.
Inatakiwa kwanza uelewe tabia za muafrika ni zipi, tabia za muafrika si tabia za kidini yaani uvivu, ubinafsi, uroho, roho mbaya, starehe, utengano, ulafi hizi ni kinyume na mafundisho ya dini.

Mababu au watu waliokufa kabla ya ujio wa dini hata SAsa hawa wanahukumiwa kwa sheria za asili yaani do and don't do yaani miiko na makatazo kwa mujibu wa sheria kanuni mila na taratibu zilizowekwa na Jamii usika.

Sala na maombi hazijasaidia kumaliza matatizo kwa sababu mwafrika ajashika dini kikamilifu. Dini ni muongozo wa maisha yote ya kiroho na kimwili, yaani huwezi fanikiwa maisha ya kimwili pasipo kwanza kutengeneza maisha YAKO ya kiroho.
 
Ngojea nikupe mfano mdogo ndugu katika ushirikina inawezekana kuna visa vya ushirikina vinahadithiwa ila havina uthibitisho lakini kuna visa unaona kabisa live Kama mbeya kuna nyumba ilikuwa inaangukiwa na kinyesi hakijulikani kinapotokea au babati watu wanapigwa na mawe hayajulikani yanapotoka na mpaka mwandishi wa habari kapigwa sasa huu ni mfano wa nguvu za giza zitokanazo na shetani sasa kama tunaweza kuona hizo amini kuna nguvu za nuru zinazohubiri mambo mema na kukataza maovu yote.

Huyo ndio Mungu ndiye anayeongoza maisha yako ndiye anayekufahamu kabla hujazaliwa ndie anayejua utapita wapi na utaishia wapi usikufuru ndugu yangu Mungu yupo wengine tumemshuhudia katika maisha yetu ingawa hatujamuona uso kwa uso stay blessed.
 
Unajua mleta mada kuna moja kati ya haya linakusumbua ama yote
1. Unadhani una akili sana
2. Una mapepo.
Hakuna nje ya hayo mawili.
 
Kwanini kuhoji dhana yenye utata kuhusu mungu iwe ujinga,?

Ujinga ni nini?
Ikiwa Mungu yupo ni moja ya maswali ya msingi na muhimu ambayo mtu yeyote anaweza kuzingatia. Maoni juu ya Mungu yanazidi, lakini kujibu swali je, Mungu yupo? inadai zaidi ya sekunde chache za umakini na inahusisha mawazo na ushahidi mbalimbali. Hatimaye, kile tunachokiona katika uzoefu wa binadamu, sayansi, mantiki, na historia husababisha jibu la ujasiri: ndiyo, Mungu yupo.

Mara nyingi, swali hili linaulizwa kama "Je, unaweza kuthibitisha Mungu yupo?" Tatizo ni kwamba, wakati ukweli wenyewe ni kamili, kuna karibu matukio sifuri ya uthibitisho kamili nje ya mantiki safi na hisabati. Kwa sababu hiyo, vyumba vya mahakama havihitaji uthibitisho kamili ili kufikia uamuzi; badala yake, wanatafuta kuondoa "shaka ya busara" na kufikiria kile "kinachowezekana zaidi."

Kudai "uthibitisho" wa Mungu ambao hakuna mtu anayeweza kukataa ni jambo lisilo na maana. Hakuna ushahidi wala watu wanaofanya kazi kwa njia hiyo katika ulimwengu halisi. Ukweli wa "Kukutana" na "kuzikubali" ni tofauti sana. Hoja nzuri zitabaki bila kushawishika kwa wale walioamua kutoamini. Kwa mwenye shaka, sio "uthibitisho," hata kama ingeweza kumshawishi karibu mtu mwingine yeyote. Dhamira ya mtu ina ushawishi mkubwa kuliko ushahidi wowote uliokutana.

Hiyo inamaanisha kiasi fulani cha "imani" ni muhimu—na sio tu kuhusu kuwepo kwa Mungu. Maarifa kamili ni zaidi ya uwezo wetu. Upendeleo na chuki ni maoni yetu. Daima kutakuwa na pengo kati ya kile tunachoweza "kujua" na kile "tunachoamini." Hii inatumika sawa kwa wasiwasi na waumini. Hatuwezi kujua kila maelezo yanayohusika kila tunapokaa kwenye kiti, kula chakula, au kupanda ngazi. Vitendo kama hivyo vyote vinaonyesha kipimo cha imani. Tunachukua hatua, licha ya kile ambacho hatujui, kwa sababu ya kile tunachojua. Hicho ndicho kiini cha imani, ikiwa ni pamoja na imani katika uwepo wa Mungu. Tunaamini kile kinachojulikana, kinatuongoza kwa vitendo, licha ya uelewa mdogo.
 
SAS izo mechanism kwann unazo wew na sio jiwe [emoji41]
Na kwanini Jiwe ni gumu wakati mimi sio???
Kwenye huu ulimwengu kuna gradient, Vitu sio homogenous, Vitu vinatofautiana.

Labda swali ni kwanini kuna gradients?
Mimi Sijui, Wewe unajua?
 
Kwanza umejuaje ni nani?? Kwanini hujauliza ni Nini??
Inamaana umeshaassume ni fulani sio?

Haya mimi sijui ni nani, wewe unajua??
Na kama unajua, unaweza ukathibitisha?
Huwa nacheka sana hoja za Wakana Mungu, kitu ambacho wakana Mungu hamkijui ni kuwa hamjijui kama hamjui yaani nyinyi ni Wapumbavu, huku mkijiona mnajua.

Umeuliza swali rahisi sana kwanini ni "Nani ?" na si "Nini ?" hili hata wenzako waliuliza sisi tukawajibu hivi nini hakina uwezo wa kusanifu wala Hakika ila nani ana uwezo wa kisanifu na anajua, ana Elimu, ana hekima na ni mkamilifu. Yaani kwa ufupi "Nani" ni dhamiri inayo kwe chenye akili, maarifa na kujua, ila nini ni dhamiri ya swali kwa kisichokuwa na akili, kisichojua, kisichokuwa na malengo.

Mimi najua na ninaweza kithibitisha kwa kutumia akili, mazingira na ufunuo.
 
Nani alilwambia Mwanadamu anaumba ? Unajua maana ya kuumba ?
 
Don't talk out loud,you lower the IQ of the whole street. [emoji2960]
 
Huo ni uamuzi wake yeye Mwenyewe[Muumba] na yeye tu ndo anajua kwanini unaumba hivo.
Hivi wewe unajua siku yako ya kufa? Unajua kifo chako kitakuaje?
Hicho kifo nani au nini kilikiweka?
Wewe umejuaje kwamba ni uamuzi wake? Una mawasiliano nae?
 
Kwanini unafikiri ni lazima viwe vimepangwa na "nani"?
Nani Ina maarifa, Ina sanifu, Ina jua, Ina malengo.

Vipi kuhusu "Nini ?" Ina nini ? Unaweza kunipa mfano wa nini ? Na ukamiambia kwanini isiwe "Nani ?"
 
Kwa hiyo majibu yakipatikana kuhusu maswali hayo basi hakutakua na haja ya kuwa na mungu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…