Unampigia simu kwa namba ngeni halafu hapokei baadaye anakwambia hapokeagi namba ngeni

Wengine hatupokei sababu ya madeni. So unakuwa unahisi anayekudai kaamua kubadilisha namba. Au unakuta unamkwepa mtu kwa sababu flani flani so unahisi kabadilisha namba. Eg mchepuko uliyemwacha bila yeye kujua
 
Mimi sio kwamba sipokei namba ngeni, napokea sana tu. Ila sipendi ile mtu kapiga sijapokea yeye anaendelea kupiga na kupiga mara kumi. Ukipiga once or twice na mtu hapokei kitu muhimu ni kutuma ujumbe mfupi, kama alikuwa mbali na simu lazima atakutafuta.
 
ukinipigia sipokei acha sms. mwingine anapiga kama mara 8 mfululizo. tambua hata kama mimi ndo mwenye shida sitapokea simu yako jumla. unanitia hofu na kunirusha roho
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Nimecheka sana hapo mwisho, kuwa anakurusha roho. Watu wengine ni wajinga sana, et anapiga simu mara 18.
 
Wengi hatujui matumiz ya sms,jitambulishe kwanza Kwa sms baada ya kupiga cmu Ili mtu aweze kujua ww n nan,
Unakuta mtu anapiga cmu hachoki tu ,ikikata anapiga Tena ,ikikata anapiga Tena, mwishowe inakuwa usumbufu.
Sasa si unapokea ndio anajitambulisha hapo hapo, unaogopa nini?
 
Binafsi namba ngeni napokea,hata nikikuta m/call Ninakuwa na shahuku ya kujua ni nani??

Lakini kama namtafuta mtu kwa mara ya kwanza,naanza mtumia sms kuwa mie mawardat,,,,,,,,,,,,,,,,
 
Ni kujipa umuhimu usiostahili ila siku yatawakuta tu
Ukimpangia mtu baki jinsi ya kujibu simu yake, aliyoinunua kwa hela zake, anayoilipia kwa pesa zake, katika maisha yake, ambayo yeye anayajua vizuri kuliko wewe, hapo wewe ndiye unajipa umuhimu usiostahili.

Na kuhusu kuwakuta, kila mtu anakutwa tu, ajibu au asijibu namba asizozijua.

Usijipe umuhimu wa kutunga sheria mtu baki apokee simu vipi.
 
Nakuelewa what you mean na upo sawa kabisa
 
huo ujinga nimeukuta kwa watu wengi sana. kuna mmoja ni hakimu mstaafu nilimtafuta mara kadhaa hakutaka kupokea cm akapishana na mchongo wa kama 10million. baada ya wiki namfuata live namuuliza shida nin nilikuwa nakupigia cm cku nzima,
akanambia uwa sipokei namba ngeni, nusu nimkate kibao,

watu wa namna iyo wengi wanakuaga wahalifu
 
Sms zina umuhimu wake, huwa najiunga kifurushi cha mwezi kabisa, 1500 napata 9000sms.
Za kazi gani sasa, piga simu, vifurushi vya dakika bei chee siku hizi
Ku chat ni whatsapp
 
Wengi hatujui matumiz ya sms,jitambulishe kwanza Kwa sms baada ya kupiga cmu Ili mtu aweze kujua ww n nan,
Unakuta mtu anapiga cmu hachoki tu ,ikikata anapiga Tena ,ikikata anapiga Tena, mwishowe inakuwa usumbufu.
mim bhana sina kabisa utamaduni wa kufungua inbox, inaweza ikapita ata siku 3 adi nne ndio naingia inbox, sms nyingi za mtandao kama vodacom ukijiunga kifurushi wanakuletea sms adi sita. mfurulizo wa sms niheri nipige cm sio kuchart
 
Hata mimi Kaka nipo hivyo.
Mwingine anakupigia anaanza kushangaa shangaa anachoongea ukielewi ,ukikata anapiga tena inakera
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…