Unampigia simu kwa namba ngeni halafu hapokei baadaye anakwambia hapokeagi namba ngeni

Unampigia simu kwa namba ngeni halafu hapokei baadaye anakwambia hapokeagi namba ngeni

huo ujinga nimeukuta kwa watu wengi sana. kuna mmoja ni hakimu mstaafu nilimtafuta mara kadhaa hakutaka kupokea cm akapishana na mchongo wa kama 10million. baada ya wiki namfuata live namuuliza shida nin nilikuwa nakupigia cm cku nzima,
akanambia uwa sipokei namba ngeni, nusu nimkate kibao,

watu wa namna iyo wengi wanakuaga wahalifu
Ukiona simu hazipokelewi tuma sms.
 
Ukimpangia mtu baki jinsi ya kujibu simu yake, aliyoinunua kwa hela zake, anayoilipia kwa pesa zake, katika maisha yake, ambayo yeye anayajua vizuri kuliko wewe, hapo wewe ndiye unajipa umuhimu usiostahili.

Na kuhusu kuwakuta, kila mtu anakutwa tu, ajibu au asijibu namba asizozijua.

Usijipe umuhimu wa kutunga sheria mtu baki apokee simu vipi.
Sahihi kabisa
 
Haijanitokea kwa mtu mmoja au wawili. Ni watu wengi sana. Wengine ni watu wangu wa karibu. Unampigia simu kwa namba ngeni halafu hapokei baadaye anakwambia hapokeagi namba ngeni.

Mwingine labda ni mtu ambae hamjawahi kuwasiliana na ndiyo kwa mara ya kwanza labda umepata namba yake. Nayeye hana namba yako na una shida ungependa kuongea nae. Unapiga simu hapokei. Baadae atakuja kukwambia namba ngeni hapokei.

Nini siri ya kutopokea namba ngeni? Faida zake ni zipi au hata nyinyi mnafanya bila kujua faida na hasara zake?
Kama unawasiliana na mtu kwa mara ya kwanza jaribu kumtumia meseji kujitambulisha, hizi simu zimeshakuwa na usumbufu mwingi kuna vitu vingi watu wanakuwa wanavikwepa ikiwemo mizinga ya ghafla bin vuuuu.....
 
KUNA WENGI NAFASI ZAO ZA KAZI HAZIRUHUSU KUPOKEA POKEA NAMBA NGENI, KAMA NAMBA ZA HUDUMA KWA WATEJA.
PIGA SIMU ISIPOPOKELEWA TUMA MESEJI AU WASAP.HIVYO TU KISHA SUBIRI MUITIKIO/RESPONSE.

MIMI KWANGU HATA KAMA NI RAIS , ANAPIGA KWANGU NA SINA YAKE NAMBA SIPOKEI.

KUTOPOKEA SIMU NGENI NI NJIA NYINGINE YA KUKUFANYA UFOCUS KWENYE KAZI YAKO.
Watu wasiojua umuhimu wa muda na kuondoa distractions hawawezi kukuelewa.

Kuna watu wengine wanapata simu nyingi wakiamua kujibu kila simu itabidi wajipe kazi ya kuwa "Telephone Operator" juu ya kazi zao nyingine.
 
Uoga + Uongo.

Kuna mtu au Hali anaikwepa.
Kuweka cm hewan na kutopokea pindi upigiwapo Ili Hali uko na simu ni nidhamu ya uoga.
 
Kama unawasiliana na mtu kwa mara ya kwanza jaribu kumtumia meseji kujitambulisha, hizi simu zimeshakuwa na usumbufu mwingi kuna vitu vingi watu wanakuwa wanavikwepa ikiwemo mizinga ya ghafla bin vuuuu.....
Mbongo hakawii kutaka kukupiga mzinga wa ghafla bin vuu mtu asiyekujua, halafu, usipopokea simu anakulaumu wewe.

Kama vile wewe ndiye umemsababishia matatizo yake.
 
Madeni ndyo yanafanya watu waogope kupokea namba ngeni. Mfano wewe ni mfanyabiasha sidhani kama unaweza kuacha kupokea namba ngeni, mfano wewe ni boss eneo fulani sidhani kama unaweza usipokee namba ngeni kwasababu unahudumia watu wengi kwahiyo sio kila anaetaka huduma yako ume save namba yake. Mfano kama una familia huwezi kuacha kupokea cm je kama mtoto au mke/mume amepata ajali huko? Watu wanafuata mkumbo tu wa kutokupokea namba ngeni kwasababu alishamsikia mtu fulani hapokeagi namba ngeni. Ukiona mdada anakuambia hapokei namba ngeni achana nae huyo ni mambo mengi (Malaya). Pia mtu ambae hapokei namba ngeni ni mshamba na limbukeni wa maisha. Full stop!
Huo ni ukweli usio na shaka!!!
 
Ni kawaida, hata mimi huwa sipokei namba ngeni, labda iwe ina kodi ya nje ya nchi; unachotakiwa kufanya, tuma sms kwanza, baada ya dakika kadhaa ndio upige. Watu wengi hawapendi kuongezewa 'stress'; kwa sababu wanakuwa walisharizika na hali walizonazo.
 
Uoga + Uongo.

Kuna mtu au Hali anaikwepa.
Kuweka cm hewan na kutopokea pindi upigiwapo Ili Hali uko na simu ni nidhamu ya uoga.

Hapana.

Kupokea kila simu unayopigiwa ndiyo nidhamu ya uoga.

Unakosa uhuru wa kusema sitaki usumbufu.

Unaogopa kulaumiwa hupokei simu.

Unaogopa matukio.

Unaogopa kutokujua anayekutafuta anakutafutia nini.

Unajiwekea nidhamu kupokea kila simu, kwa uoga.
 
mim bhana sina kabisa utamaduni wa kufungua inbox, inaweza ikapita ata siku 3 adi nne ndio naingia inbox, sms nyingi za mtandao kama vodacom ukijiunga kifurushi wanakuletea sms adi sita. mfurulizo wa sms niheri nipige cm sio kuchart
Hapa Sasa wabongo tunafeli sana,wazungu sio wajinga kuleta hiz smart phone,unakuta mtu kanunua smart hataki Tena kutumia sms 😂 anadai et nichek wasup😂 ,duh ,wenzetu Bado wanatumia zile smu za public za mtaani ,lakin cc wabongo tumezitoa eti zimepitwa na wakat😂,shida watuwengi Wana jiona ni WA maana sana kuliko ndio maana tunapitwa na michingo mingi,
 
Hapana.

Kupokea kila simu unayopigiwa ndiyo nidhamu ya uoga.

Unakosa uhuru wa kusema sitaki usumbufu.

Unaogopa kulaumiwa hupokei simu.

Unaogopa matukio.

Unaogopa kutokujua anayekutafuta anakutafutia nini.

Unajiwekea nidhamu kupokea kila simu, kwa uoga.
Moja kati ya matumizi ya sm ni kupiga na kupigiwa.
Usipopokea simu inamaanisha unakwepa kupata taarifa ya anayekupigia.
Na kwanini namba mpya tu? Huo ni uoga mkuu unaowasukuma wengi kutopokea namba ambayo hajasave.
 
Moja kati ya matumizi ya sm ni kupiga na kupigiwa.
Usipopokea simu inamaanisha unakwepa kupata taarifa ya anayekupigia.
Na kwanini namba mpya tu? Huo ni uoga mkuu unaowasukuma wengi kutopokea namba ambayo hajasave.
Hapana.

Kupokea kila simu ndiyo woga.

Unaogopa lawama kwamba hupokei simu.

Unaogopa kukosa kujua anayekupigia simu anataka kukuambia nini.

Mimi nisiyepokea namba nisiyoijua ndiye siogopi.

Siogopi lawama kwamba sipokei kila simu.

Siogopi kukosa kujua anayenipigia anataka nini.

Nishajiwekea kanuni sitaki usumbufu wa simu za kutoka namba nisizozijua na naifuata kanuni yangu kwa uhuru wangu bila woga.

Simu yangu, kanuni zangu, sina woga.
 
Mimi namba ngeni sipokei hata iweje, ila baada ya muda naipigia.
 
Mimi namba ngeni nilikuwa sipokeagi kabisa, Yani mpaka utume msg kuwa Mimi ni Fulani ndipo nitakupigia au lah upige mara nyingi ndiyo nitajua uyu Kweli ana shida nitakusikiliza, hii tabia ilishasemwa Nyumbani mpaka basi. Na Sina madeni, sina mchepuko, sio tapeli Ila tu sipokeagi.

Ila kuanzia mwaka Jana, last born alivyoenda bweni, mimi napokea namba ngeni zote, Yani ata ukibip tu Mimi nishapiga fasta, silembi. Ngoja amalize shule nirudie utaratibu. Namba ngeni muda mwengine zinaboa[emoji849]
 
Hapana.

Kupokea kila simu ndiyo woga.

Unaogopa lawama kwamba hupokei simu.

Unaogopa kukosa kujua anayekupigia simu anataka kukuambia nini.

Mimi nisiyepokea namba nisiyoijua ndiye siogopi.

Siogopi lawama kwamba sipokei kila simu.

Siogopi kukosa kujua anayenipigia anataka nini.

Nishajiwekea kanuni sitaki usumbufu wa simu za kutoka namba nisizozijua na naifuata kanuni yangu kwa uhuru wangu bila woga.

Simu yangu, kanuni zangu, sina woga.
Okay sawa kama ni kanuni Yako hivyo kutopokea uko sahihi pia.

Lakini Mimi iwe namba ya kuzimu iwe ya wapi napokea bila kujali ni taarifa Gani napewa, coz siogopi kuface challenge yeyote. Ikiwa Niko bize siitaji usumbufu na fly✈️.
 
Wengi hatujui matumiz ya sms,jitambulishe kwanza Kwa sms baada ya kupiga cmu Ili mtu aweze kujua ww n nan,
Unakuta mtu anapiga cmu hachoki tu ,ikikata anapiga Tena ,ikikata anapiga Tena, mwishowe inakuwa usumbufu.
Sasa kama namba yako nilipewa na mtu kitambo tu, leo nimekutana na mishe inayohusiana na wewe, naanzaje kukutumia sms ukizingatia hatujuani!?
 
Back
Top Bottom