Unampigia simu kwa namba ngeni halafu hapokei baadaye anakwambia hapokeagi namba ngeni

Unampigia simu kwa namba ngeni halafu hapokei baadaye anakwambia hapokeagi namba ngeni

kwakweli namba mpya sinaga haraka nazo hata ukipiga simu naiona nitaiacha iite then baada ya dakika kadhaa au masaa nakupigia.
Siku hazifanani.Kuna siku hautokuwa na Salio.Sasa sijui utapigaje hiyo simu.

Sema ni vizuri kama anakupiga unasubiri ikate halafu ndo vizuri zaidi kuliko kuiacha una iangalia.
 
Ni vizuri ukiwa na muda upokee simu zote,hata namba ngeni.mambo ni mengi dunia hiii
Kabisaa... Maana Dunia ina mengii mambo.

Hata kama uko bize,Tenga muda wa kumtafuta aliye kupigia muda ule wakati ulikuwa na Shughuli zako, Kumsikiliza anasemaje.

Labda TU uwe tapeli,una madeni,mharifu,mwizi,jambazi, hapo usipo pokea simu ni haki Yako.Maana uko kazini.
 
[emoji119]Ni kwel cjakataa nimekubali ,ni pale mtu anapopiga cmu mara nyingi unakuta Hana option nyingine ya Kutuma sms labda ana dakika tu,sawa bac kutopokea ni woga au ni ukosefu wa akili na kujiona wa maana au kuwa na princeple za kijinga HKBW

Nakazia.

Kutopokea simu Kwa namba ngeni iliyo kupigia ni kujiona wa maana kuwa wewe ndo wewe,Woga, kutojiamini,Kutokuwa na msimamo Kwa kuhisia kuwa utapigwa vizinga sababu nyingine ni utapeli,uharifu na madeni Ukidhani unatafutwa na askari.


WALIO WENGI WASIYO POKEA SIMU,MARA NYINGI NI WALE AMBAO HUWA NDO WAMEANZA KUYAPATA MAISHA KO WAKIONA NAMBA NGENI WANA DHANI WANA OMBWA HELA HII KWA WANAUME NA WANAWAKE

KWA WANAWAKE MARA NYINGI HUWA NI SABABU WAKIDHANI KILA SIMU NI YA KUTONGOZWA HASA WANAO JIONA CAKE KUWA NI WAZURI.
 
Asilimia kubwa hatupokei namba ngeni kwasababu binafsi nimehitimisha ivo
Exactly, pia inaonesha watu wengi ambao hawapokei namba ngeni shauku yao ni kutaka kujua nani aliyepiga pamoja na nia/shida yake, ndyo maana wengi wamesema baada ya dkk au masaa kadhaa wanajaribu Ku-callback , ingawa namba kubwa ya sisi sote imethibitika hukerwa na upigaji wa simu mfululizo mfn missed call zaid ya 5 zinazofuatana.

My take: kila mtu ana Uhuru na mipaka kuhusu simu yake kutokana na mazingira na kazi anayofanya, ukipiga simu Mara mbili hapokei kama ni mtu wa mhimu na hakuna mbadala huna budi kumwachia ujumbe,
Ila kama sio kivile means kuna Alternative potezea usimtumie hata sms atakutafuta yeye
 
Namba 30 Kwa siku.Kwamba namba Yako umeisambaza kwenye mitandaoni??

Huna biznes unasambaza namba kwenye mitandao ya kijamii au kwenye kuta za Nyumba lazima uisome some.Hapo utahisi ni usumbufu Kumbe uliyataka mwenyewe.
Wewe huyajui haya ngoja niscreenshot call log yangu ya leo. Na leo ni PUBLIC HOLIDAY. Na hapa ndio kwanza saa 11 jioni.
Saa 6 hata sijatoka home simu zimeanza. Na ukiona hizo naumber in brackets ujue ni number of times someone has tried to reach me.

Nachoka. Na tunawaambia kila siku, kama sio emergency pls text jitu limekazana kupiga simu multiple times.

Screenshot_20220407-172643~3.png


Screenshot_20220407-172757~3.png


Screenshot_20220407-172931~3.png


Screenshot_20220407-172452~3.png
 
Hivi kama unampigia mtu simu hapokei si unaachana nae. Hawa ndio wale wasumbufu atapiga simu hata mara 20 na ukipokea utaskia nilikua nakusalimia.
Tena nikiona msumbufu wa hivi huwa nakata kabisa ili ajue kuwa namuona,wanakera sana.

Hata kama nina namba yake kuna muda mtu uko busy,umechoka, n.k sasa siyo lazima nipokee simu kama mtu anaona ni muhimu kwanini asiandike msg.
 
Tena nikiona msumbufu wa hivi huwa nakata kabisa ili ajue kuwa namuona,wanakera sana.

Hata kama nina namba yake kuna muda mtu uko busy,umechoka, n.k sasa siyo lazima nipokee simu kama mtu anaona ni muhimu kwanini asiandike msg.
Wanakera sana basi tu.
 
Kwa uzoefu wangu namba mgeni mara nyingi unakuta mtu kakosea namba na wengi wao unakuta ni watumiaji wapya wa simu hasa wa vijijini huko ndanindani.

huyu atabeep weeee ukipokea tu yeye anakata chap ili wewe ndo umpigie hlf kwa saabu bado hajui kutumia cm vzuri unakuta umetumia dakika 5-7 kumwelewesha kuwa ww sio uyo anayemtafuta
 
Wengi hatujui matumiz ya sms,jitambulishe kwanza Kwa sms baada ya kupiga cmu Ili mtu aweze kujua ww n nan,
Unakuta mtu anapiga cmu hachoki tu ,ikikata anapiga Tena ,ikikata anapiga Tena, mwishowe inakuwa usumbufu.
Safi sana.
Hata mimi, inaniwia vugumu sana kupokea namba ngeni. Kwa heshima huwa namtumia ujumbe huu: "Tafadhali, nani mwenzangu? Usipige nitumie ujumbe"
Kwa mshangao, mara: prii prii, priprii,...
Inakera!
 
Vipi hawa ambao ukiwapigia wao hawapokei, bila wao wakiwa na shida wanakupigia.


Pia wapo ambao hata ukijitambulisha wa SMS hawajibu labda uwafuate manually.


Dunia inamambo mengi sana.
 
Nimepitia kwa uchache comments sijaona yenye kutoa mawazo ya ki_IT, mfano kama mnaogopa kisa unknown caller kuna app nyingi sana za kum_identify anayekupigia na nyingi ya hizo app hazina ukubwa hata wa 20mb's.

Download unayoipenda kuna za bure na kulipia so chagua alafu fanya settings aya weka simu mezani subiri wapige.
 
Back
Top Bottom