Unatafuta msaidizi wa nyumbani? Kwa Million 100 jipatie Optimus Robot kutoka kwa Elon Musk

Unatafuta msaidizi wa nyumbani? Kwa Million 100 jipatie Optimus Robot kutoka kwa Elon Musk

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Tajiri mwenye ahadi nyingi Elon Musk wakati wa uzinduzi wa Tesla Robotaxi alionyesha pia humanoids robots zake zinazoitwa Optimus.

IMG_0454.jpeg

Kutoka na presentation yake aliahidi kwamba Optimus inaweza kufanya chochote unachotaka. Akazidisha akasema “Optimus ni biggest product ever katika human kind” na inaweza ikawa mwalimu, akawa mlezi wa wanao, akakutengenezea bustani, ukamtuma dukani, mkacheza nae music, akawa anafanya kazi bar kama muhudumu nk.

IMG_0453.jpeg


Na ata baada ya event yake ya We Robot wakati wa after party, Optimus walisave drinks kwa waudhuriaji.
IMG_0455.jpeg

Kuhusu bei itauzwa $30,000 tu!

Sijui tumejiandaaje kuanza kucompete ajira na aga maroboti.
 
wakiambiwa kua watu walianza kwenda mbele yamuda tokea enzi za mababu zetu wanaona kama nindoto au mambo yakufikirika tuu.
Sasa musk anakuja taratibu badae watu watamuelewa na wataelewa kua Akili yabinadamu nizaidi yawakati wenyewe.
Tutaanza kugombana na aya maroboti maana itafika kipindi yataanza kua na conscious.
 
Hivi ninyi mnadhani wenye dunia yao watakubali kila kitu. Wenye dunia yao mtaji wao wa kwanza ni watu.

Nimesema watu, sijakosea. Narudia tena. Mtaji wao namba moja ni watu.

Uwepo wa watu ndio uwepo wa PHARMACEUTICAL industries, hapa nazungumzia dawa za binadamu, wanyama na dawa za kilimo (mimea). Watu wasipokuwepo hizo industries zitakufa, watakubali?

Sekta ya kilimo wasipokuwepo watu itakufa, watakubali? Tunalima ili tule, dunia ikijaa miroboti atakula nani?

Wenye dunia yao lazima watalinda ajira zenu, ili mle mshibe, mzaliane, wauze magari, ndege, meli, wauze dawa, nguo, viatu, music, electronics.

Kupunguza ajira ni kuitia dunia umasikini ambayo itapelekea kupungua vizazi, idadi ya watu as a result and hence kuuwa industries kubwa kubwa.

That can't happen.

Kuna baadhu ya ajira zitapotea na kupungua ila sio kuzifuta zote duniani.

Signing out .
 
Duh! Hapa nimetoka kutizama movie inaitwa subservience ya 2024 ikizungumzia hizo AI robots.

Robot lina hadi adult mode, jamaa alipoweka adult mode, robot likaanza kurembua jamaa akagegeda robot halafu mkewe si akajua😂

Robot linafanya kazi zote nyumbani.

Na haya maendeleo ya AI, kila siku watakuwa wana update hizo robots, pia zitatokea kampuni shindani ikiwamo za China, hapo ndipo binadamu wataanza kuandamana kupinga uwepo wa robots...
Watu watapoteza ajira, migodini, kampuni za ujenzi,viwandani, hospital hata surgery yatafanya. Robot halichoki halafu lina nguvu kuliko mtu na akili za AI.
 
Mimi naona kama hii mada ni ngumu sana inatakiwa ijadiliwe na wataalam wa hayo mambo;

wahandisi na wanauchumi
Kwa US na EU kuwa na mfanya kazi wa ndani ni expensive na sheria kibao.

Watayanunua sana tu yalee watoto, kupika na kusafisha nyumba.
Kazi za nguvu na akili kidogo kama viwandani, mashambani, driving n.k hizo robots zitachukua nafasi, cause hata sasa mmeona nchi kama UK, Canada n.k wanavyohitaji skilled labor na wakaanzisha policy yao ya skilled immigrants..

Hapa wazungu hawana shida, kazi ipo kwa wahamiaji. Wazungu wanapiga kwenye mshono, baada ya muda utasikia hawahitaji tena skilled immigrants hata wakihitaji ni kwa uchache.
 
Back
Top Bottom