Hello Wafugaji wenzangu 👋🏽,
Nimeona kuna watu wengi wanaanzisha ufugaji wa kuku, hasa kwa lengo la kupata mayai ya kutosha kwa matumizi au biashara, lakini ndani ya miezi michache wanakata tamaa. Nimeona hii mara kwa mara, na mara nyingi chanzo kikubwa ni
kununua kuku bila utafiti sahihi.
Unapopanga kununua kuku waliokwisha lelewa (hasa wale waliozidi umri wa mwezi 1+), ni muhimu sana kujua
aina ya kuku unayonunua na uwezo wake wa kutaga. Kwa bahati nzuri, kuna breeds za
Sasso ambazo zimeonesha matokeo bora katika utagaji na hizi hapa ndizo tano za juu kabisa kulingana na
Sasso Poultry Resources:
1. Ciara🐔
- Rangi: Nyeusi na vidoti vya dhahabu shingoni
- Mayai: 302 kwa wiki 75 (siku 525)
- Umri wa kuanza kutaga: Wiki 20
- Uzito wa kuanza kutaga: 2.205kg
View attachment 3325159
2. Scarlet🐔
- Rangi: Kahawia, hufanana na kuku wa layer (ISA brown)
- Mayai: 318 kwa wiki 75
View attachment 3325161
- Umri wa kuanza kutaga: Wiki 20
- Uzito: 2.050kg
3. Ivory🐔
- Rangi: Manyoya meupe
- Mayai: 318 kwa wiki 75
- Umri wa kuanza kutaga: Wiki 20
- Uzito: 2.050kg
View attachment 3325166
4. Irona🐔
- Rangi: Mchanganyiko wa kijivu na meusi
- Mayai: 318 kwa wiki 75
- Umri wa kuanza kutaga: Wiki 20
- Uzito: 2.050kg
View attachment 3325169
🐔 5. Silver
- Rangi: Kahawia na meusi (kichwani zaidi)
- Mayai: 298 kwa wiki 75
- Umri wa kuanza kutaga: Wiki 20
- Uzito: 2.140kg
View attachment 3325170
💡 Kabla hujafanya uamuzi, tumia FUGA CALCULATOR yetu ya bure 🧮👇
➡️ Nenda
www.primaxtz.com
➡️ Bonyeza
"Fanya Makadirio Hapa"
➡️ Weka aina ya kuku na idadi utajua
gharama halisi, feed ya kila siku, na mapato ya uwezekano!
🎁 Kama unapata thamani kutoka kwa hii calculator unaweza kutuunga mkono kwa kubonyeza kitufe cha
"Support Us" kilichopo pale pale kwenye ukurasa. Inatusaidia kuendeleza zana hii kwa wafugaji wengi zaidi! 🙏🏾❤️
View attachment 3325175
🎯 Angalizo Muhimu:
Tafadhali
usinunue kuku kutoka sehemu ambayo hujaridhika na hali ya usalama wa kiafya (biosecurity). Wengi wamepata hasara kubwa kutokana na kuleta kuku wagonjwa au waliobeba magonjwa nyumbani.
Najua kuna wafugaji wengi humu mna uzoefu -mnaweza ku-share breeds nyingine pia zilizowalipa vizuri? Na kwa wale wanaoanza,
tafadhali jisomeeni haya kabla hujatoa hela yako. Hii ni biashara kama nyingine, na maamuzi madogo ya mwanzo yanaweza kukuokoa au kukuangusha kabisa.
Stay smart. Fuga kwa maarifa 💡
#PoultryFarming #Mayai #KukuWaMayai #UfugajiBora #FugaSmart #KilimoBiashara