Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
- Thread starter
- #81
Uelewa wa watu wengi humu jf au Tanzania una walakini.Yaa i watu wanatetea uvunjwaji wa sheria kisa tu yanayowakuta ni watoto wa maskini! Hivi tukisema mtu akifanya kosa auawe bila kufuata sheria wangapi watauawa. Mfano hao watoto wa ushuani wakichukua gari za baba zao na kwenda nazo kwenye sherehe za birthday za ulevi kisha kutokana na kuendesha gari wakiwa wamelewa wakisababisha ajali nao wauawe papo hapo au wazazi wao watakuwa wa kwanza kutaka sheria ifuatwe? Au watoto wao humo ndani wakibaka housegirl mbona wanajitahidi kuyamaliza kimya kimya? Je nao wauawe bila kuhukumiwa mahakamani?
Ni vyema tutatue matatizo ya jinai mbalimbali kwa kufuata sheria.
Sasa sheria zilitungwa ili zifanye kazi gani kama kuwa tu mtuhumiwa unauliwa?
Hawa wanaotafuna mabilioni ambayo yangejenga health center na kununua dawa si wauaji?