Uongo mgumu kuutetea, Tundu Lissu, CHADEMA na CCM wanahaha!

Lisu na Lema wamejivisha ukimbizi wanajiita wakimbizi wa kisiasi

Usifurahie janga la mwenzako kisa tu mpinzani. Leo Kuna watu wanalia Makmba kamsema vibaya mwendazake Magufuli lakini ni hao walimdhihaki Lissu alipolimwa risasi dodoma.
 
Angekuwa amekufa, sasa Yuko hai, aende akatoe taarifa ya tukio,

Sasa yy anakimbia kimbia Tu na kutengeneza madrama kibao

Punguza dharau wewe ni mwadamu acha kukufuru. Watu wanahama mtaa kisa katishiwa kisu na kibaka usiku , sembuse kumiminiwa risasi na watu wasiofahamika na hawajakamatwa.

Endelea kuiabud CCM na kuacha utu kisa chama. Unaona sifa kumlamu mhanga wa shambulio lakini polisi walioshindwa hata kutoa ulinzi walipopewa taarifa unaona sahihi?. Sawa ipo siku kila kiti kitakuwa wazi.
 
Lema awe mkimbizi wa kisiasa kweli ?

Unaniuliza?. Alipokaa rumande miezi sita ulikuwepo?. Kama sio mahakama kuu kuingilia Kati asingetolewa rumande. Kemea maovu usiyachekee siku yakifika mlangoni mwako hatakuwepo wa kukusaidia.
 

Unajuaje kama hakupewa ulinzi?

Unajuaje kama police walishughulikia tatizo lake?

Mnaaminishwa madudu Tu ndio shida yenu chadema

Wakati mambo yako wazi na fact zipo za kutosha

Sasa just because umesema kuna gari inakufata so unataka upewe escort?

Kama jeshi litatoa escort Kwa kila mtu ambae anahisi anafatiliwa then itakuwaje?

Acha utumwa wa fikra wakup

Akili za kuambiwa changanya na zako

Me nakwambia kama serikali inataka kukuua watakufata hata nyumbani kwako na wakuue
 

Kumbe tatizo lako ni CHADEMA?. Endelea na CCM yako ya Makamba. Unajadili vitu kwa kuangalia CHADEMA au uhalisia, Yani leo Kinana ashambuliwe kwa risasi watasema wanamsubiri aamke kwenye comma ya miezi sita?.

Endelea na UCCM wako na kushangilia mabaya ya wengine kisa CHADEMA, siku yakikufika mabaya hakuna ambaye atakuchukulia serious. Juzi hapa CCM walimcheka Lissu alipolimwa risasi lakini Leo wanalia Makamba kamsema vibaya Marehemu. Aombe radhi.

Najua Lissu alipona kwa makusudi na ipo siku kila kitu kitakaa wazi. Maana angekufa ingenyamazishwa kimya kimya. Akina sirro bado wapo watasema tu ukweli siku moja, hii dunia inazunguka .
 
Wewe endelea kuwa BWABWA wala usijifiche kwa ccm
 


Huna hoja
Unakimbia kimbia Tu,

Ww unamuongelea lisu kama chadema na sio kama binadamu wa kawaida tu

Sasa unasema kitu bila details

Sakata la lisu lilifanywa na nyie wenyewe chadema
 
Kudo!

Mimi huwa najiuliza sana,hivi enzi zile kina Nyerere wakitafuta UHURU wa nchi hii.

Na kama wangekuwepo watu wanasiasa kariba ya Tundu Lissu!

Ingewezekana UHURU kupatikana kweli?

..mkoloni angekuwa katili kama Magufuli, na utawala wake, Tanu wangeendeleza harakati za uhuru?

..Tanu hawakuwahi kupigwa mabomu na Muingereza, hawakuswekwa mahabusu, hawakufunguliwa makesi mabaya, hawakudhalilishwa, kama ilivyotokea kwa wapinzani wakati wa Magufuli.

Cc Kalamu, Mag3
 
Sasa kama wamepuuuzia, Kwa Nini mhanga asilalamike kwenye vyombo vya Dola ili shambulio lake lifanyiwe uchunguziii??

..wenye wajibu wa kufanya uchunguzi ni vyombo vya dola.

..waliopuuza kufanya uchunguzi ni vyombo vya dola.

..Lissu amelalamika mara nyingi tu kwamba vyombo vya dola havishughulikii tukio lake.
 
Hiyo CCtv ilikua ya nani?
Na mlienda kutoa maelezo mkaonba hiyo CCtv iletwe?

Kwa Nini huyo tundu asiende kuiomba hiyo CCTV baada ya kutoa maelezo?

..Cctv ni kidhibiti toka ktk tukio la jinai.

..Kidhibiti huwa ni mali ya Polisi na hakitolewi mahali popote isipokuwa mahakamani.

..Lissu haruhusiwi na sheria kupewa Cctv zilizokuwa eneo aliposhambuliwa.
 
..wenye wajibu wa kufanya uchunguzi ni vyombo vya dola.

..waliopuuza kufanya uchunguzi ni vyombo vya dola.

..Lissu amelalamika mara nyingi tu kwamba vyombo vya dola havishughulikii tukio lake.

Lisu anataka vyombo vya Dola vifanye anavyotaka yy while kila kitu kina utaratibu wake
 
Walking miracle ni uzembe wa kufikiri .
Hata shetani anakushangaa.
 
Lisu anataka vyombo vya Dola vifanye anavyotaka yy while kila kitu kina utaratibu wake

..Ni miaka mitano tangu ashambuliwe.

..huwezi kumlaumu Lissu kwa kulalamika kuwa Polisi wamelegalega, au hawana nia, kufanya uchunguzi.

..Jaribu kuwa ktk nafasi ya Lissu. Je, ungeridhika na mwenendo wa Polisi?

..Tutangulize ubinadamu ktk suala hili.
 
Tangu lini Chadema wana-command vyombo vyote vya ulinzi na usalama? TISS, Jeshi, Polisi, Magereza, Uhamiaji wote wanawajibika kwa Chadema?

Uongo kweli ni dhambi.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…