Upangaji wa Makao Makuu Dodoma. Nani aliamuru Ikulu izungukwe na Makazi ya Watu?

Ni vile watu hawaelewi utendaj kazi wa Intelijensia.

Hao unaosema ni Wananchi wamezunguka IKULU una uhakika ni Wananchi/Raia wa kawaida?.

Humo kuna Nyoka kama wote.

Mbili huwezi rundika Viongoz ktk sehem moja ni risk kama itafanyika shambulio la Anga.

Tatu huna uhakika kama RAIS anakaa IKULU.. sio kila muda anakuwepo pale.

Nne Chamwino imewekwa strategically kwa kuzingatia Environmental factors.

Tano RAIS mwenyewe hapapendi Dodoma, hivyo hakaagi sana huko.

Sita, Wazo lako la kuwa DODOMA ni mji wa kisenge senge nimekubaliana na ww, ule mji ni wakipumbavu lingebaki Bunge tu kule. Tunadhalilisha Taifa.
 
Makazi yenyewe ya raia waliozunguka ikulu hayajaplaniwa vizuri yani yamejengwa hovyo wasije wasumbua baadae kuanza kuwatoa.
 
Kuhusu wananchi wa kawaida kuzunguka maeneo yale hilo nina uhakika nalo maana nilikuwa maeneo yale . Hata Halmashauri ya Jiji wamepima viwanja na wanaviuza kwa watu mbalimbali maeneo yale.

Mbili ni safe zaidi kwa Ofisi Kuu ya nchi kuzingukwa na Ofisi za Serikali na Makazi rasmi ya viongozi na watumishi wa serikali kuliko kuwa otherwise.

Nchi nyingi duniani nilipofika iko hivyo. Ikulu ipo karibu na Bunge, Wizara na Makazi ya wafanyakazi wa Serikali na viongozi
 
Kwa mawazo yako kitendo cha Ikulu kuwa karibu na Makazi ya Watu ndiyo inakuwa rahisi kuingilika? Hivi ulishajaribu kwenda hapo Ikulu?

Taratibu za kuingia pale ni ngumu mno sasa sijui wewe hofu yako ni ipi? Au Rais hatakiwi kuonekana na Wananchi wa kawaida? Kama suala ni usalama wa Rais akiwa Ikulu bado upo kwani ulinzi wake ni mkubwa mno..
 
D
Dar tu naskia Manji alijenga jengo karibu na ikulu naskia Serikali walichukua floo zote za juu.

Kwa Dar ikulu yetu imezungukwa na Ofisi za Serikali na nyumba ambazo zinasemwa ni za watumishi wa Serikali/ za serikali.

How comes Dodoma inapangwa tofauti?
 
Mkuu Yoda heshima kwako bora ibaki hapo hapo gharama za hama hama ni kubwa sana mkuu
Sasa hivi ni kama serikali iko Dodoma na Dar es Salaam na hali inaweza kudumu hata miaka 30 ijayo au ikawa ya kudumu milele. Kwenye maisha ni vyema pia kujiepusha na kitu kinaitwa "sunk cost fallacy".

Sunk cost fallacy ni ile hali ya kuogopa kuachana na mpango, uamuzi au biashara fulani hata kama kufanya hivyo ndio uamuzi wa busara zaidi hali ilipofika kwa sababu tu umewekeza sana katika huo mpango/uamuzi/biashara.Badala yake unabaki tu ukifariji kisaikolojia kuendelea labda ipo siku faida au tija itapatikana huku ukizidi kupoteza, kuumia au kupata hasara.
 
Mfn Nchi gani?

Hapo ni swala muda, kwanza kbs majengo na baadhi ya shughuli hazitafanyika maeneo hayo ikumbukwe kuwa IKULU yenyewe haijakamilika 100% ktk swala la ujenzi
 
Kupanga ni kuchagua, sidhani kama hilo suala lipo kikanuni au kisheria kwamba Ikulu lazima zifanane!

Kama suala ni usalama wa Rals hata Ikulu izungukwe na Makazi ya Watu hakuna athari yoyote na kama kuna njama dhidi yake hata azungukwe na Kambi za Jeshi au Ofisi za Serikali bado haitasaidia.

Wewe mwenyewe kuna sehemu kwenye maandishi yako umekiri kuwa Rais wa Urusi alikoswakoswa licha ya Ikulu yake kuwa mazingira ambayo wewe unaamini ni salama.
 
Mfn Nchi gani?

Hapo ni swala muda, kwanza kbs majengo na baadhi ya shughuli hazitafanyika maeneo hayo ikumbukwe kuwa IKULU yenyewe haijakamilika 100% ktk swala la ujenzi
Marekani, Urusi, China, India Nigeria, Rwanda na Afrika Kusini
 
Architecture inaweza ikawa sio hoja sana. Ila kupima viwanja na kuwauzia watu maeneo karibu na ikulu kabisa itakuja kutufanya tuwe tunawaza vizuri siku si nyingi sana
Usanifu nao ni hoja, si sawa kujenga ofisi kuu ya Serikali katika karne hii kwa sanifu ya Seraseni ya mwaka 1922. Tunashauriwa kutunza majengo ya zamani, lakini katika ujenzi mpya ni vema kuangalia wakati wa Sasa na ujao
 
Fire Fire Fire my comrade,all I hear is facts. Let's keep spitting facts later generations gonna understand.
 
Usalama kwa kiongozi mkuu unapaswa kuwa sawa mahali popote pale
Hata pale Chamwino usalama upo licha kuwa na Makazi ya Watu, alafu lazima utambue kuwa kile unachokiona karibu na Makazi ya Watu ni ukuta ambao ni zaidi ya kilometa 20.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…