Upangaji wa Makao Makuu Dodoma. Nani aliamuru Ikulu izungukwe na Makazi ya Watu?

Upangaji wa Makao Makuu Dodoma. Nani aliamuru Ikulu izungukwe na Makazi ya Watu?

Kuwa Rais sio kuvuka hadhi ya ubinadamu.

Yule ni mtu kama wewe tu.

Hivyo kukaa na watu kama yeye sio makosa.

Acha kutukuza watu.

Mpe utukufu Mungu tu.
Siku hizi una akili sana wewe 😁😁😁
Ila enzi za mzilankende anazunguka na wanajeshi na silaha zabkivita ardhini na angani ulikuwa ume mute tu
 
Sisi Waafrika vitu kama ikulu huwa tunamsikiliza sana mganga (sio daktari) wa taifa aseme ijengwe wapi...
 
Naona utakuwa umepita barabarani ukiingia Dodoma au ukitoka Dodoma ukielekea Morogoro na wala hujaingia Ikulu wewe. Ikulu ya Dodoma ni eneo kubwa sana upande mmoja imepakana na Kambi ya Jeshi pia imepakana na wananchi. Kwa taarifa yako ni salama zaidi kupakana na wananchi kuliko unavyofikiria wewe!!
Ili likitokea la lutokea unatoroka kujichanganya na wananchii🤣🤣
 
Mfn Nchi gani?

Hapo ni swala muda, kwanza kbs majengo na baadhi ya shughuli hazitafanyika maeneo hayo ikumbukwe kuwa IKULU yenyewe haijakamilika 100% ktk swala la ujenzi
Hiyo Ikulu ni kwamba haikamiliki au haikamilishwi? Inajengwa kwa muda gani?!
 
Huyu mleta Uzi haijui vizuri Ikulu ya Chamwino, yeye kaona ukuta ulizonguka Ikulu upo karibu na Makazi ya Watu ndiyo anasema Ikulu.
Hiyo siyo hoja yangu. Hata ikulu ya DRC ipo hivyo ila haijazungukwa na makazi ya wananchi. Likitokea siku utakuja kuelewa hoja yangu
 
Usanifu nao ni hoja, si sawa kujenga ofisi kuu ya Serikali katika karne hii kwa sanifu ya Seraseni ya mwaka 1922. Tunashauriwa kutunza majengo ya zamani, lakini katika ujenzi mpya ni vema kuangalia wakati wa Sasa na ujao
Zamani mtu alikuwa akivaa suruali iliyochanika aliitwa Masikini...leo hii suruali zilizochanwa chanwa ndiyo fashion halisi.
Kujengwa fashion ya zamani siyo hoja, hoja ni kuwa inakidhi mahitaji ya sasa?
 
Safari ya kuifikisha nchi hii kwenye maisha bora ni ndefu sana,why mkuu uhangaike na ikulu kuzungukwa na makazi ya watu?,tatizo lipo wapi?au ndio wale wale wanaowaona ma no 1 wetu kama miungu wadogo?,President wa Botswana alikua anatumia pikipiki kusafiri na ana ride mwenyewe, state house pale GABS imezungukwa na makazi, Union Building pale Arcadia ya SA imezungukwa na watu na ruhusa ipo kuingia mle,state house pale Newlands Capetown ukuta wake ni public parking!!,loo middle class wangu ni shida,hangaika kutafuta fedha
Bora mkuu kwa kumjibu, maana amefoka sana, alafu uyu mtoa mada yawezekana alikua nje miaka mingi, maana ni juzi ametembelea Dodoma mpaka anazungumzia ukumbi wa bunge na mazingira yake ambayo yapo vile na ukumbi haujajengwa leo wala sikuwahi sikia wabunge lalamika wanakosa parking
 
Akili yako ya kindezi huwezi elewa.
Kakwambia ukweli.Watu wakiamua kumfanyia umafia rais wa nchi yoyote watamfanyia tu haijalishi ikulu itakua imejengwa wapi.Na mara nyingi matatizo ya ikulu yanaanza na waliopo ndani ya ikulu.Wa nje wanakuja kwa maelekezo ya wa ndani.Kwahiyo eneo ilipo ikulu wala haina maana.
 
Klemrin tu ambako pana ulinzi putin kakoswa koswa. Pata picha ikulu ya Urusi ingekuwa karibu na makazi ya wananchi leo hii ingekuwaje?
Kakoswa koswa na wahuni tu ambao hawakujipanga sawasawa.binadamu akijipanga vizuri kukuangamiza labda ukaishi kwenye jua,ila kwenye hii dunia huna ambako hawawezi kukufikia.
 
Watanzania kama sio kukosa exposure basi ujinga unatutesa sana na kuna siku utakuja kutugharimu sana

Wiki iliyopita nilikuwa Dodoma nimeangalia namna ya Jiji la Dodoma lilivyopangwa na kusema kweli nimesikitika sana.

Hii nchi kuna siku yatatukuta ya Haiti wahuni wanaingia kwenye makazi ya Rais kufanya umafia na kutokomea bila hata kukamatwa alafu ndo tunakuja kuunda tume kujua tatizo kumbe hatushughulishi akili zetu kwa wakati sahihi.

Nani aliyesema Chamwino kwenye Ikulu pazungukwe na Makazi ya watu binafsi? Waliopendekeza hili hawakuona hatari yake?

Nani alipendekeza Mji wa Serikali ujengwe Mtumba na sio Chamwino?

Kwa sehemu nyingi duniani makazi ya Rais yanazungukwa na Ofisi Kuu za Serikali na hata makazi ya viongozi wa Kiserikali na sio watu binafsi. Kujenga mji wa Serikali sehemu tofauti alafu kuweka ikulu kwenye makazi ya watu hawakuona hili linaweza kuleta matatizo siku moja?

Kiuhalisia Mji wa Serikali na Makazi ya Viongozi wa Serikali vyote vilitakiwa kuwepo Chamwino na kuzungukwe na kambi za Jeshi ila kwa Dodoma haya hayajafanyika

La kunichekesha zaidi ni Jengo la Bunge. Hili Jengo lipo sehemu ya ajabu kabisa. Nje kuna vibanda vya chips na makazi holela. Inafika hadi wabunge wanakosa sehemu za kupaki magari na mwishowe kusababisha msongamano mkubwa sana kipindi cha Bunge.

Kusema kweli kwa watu wasio na akili wataifurahia Dodoma ila kwa wenye akili na wanaoona mbali Dodoma itakuja kuligharimu sana Taifa siku za mbeleni mbeleni!

Kwani si wanapakigi kwenye temesa yao ile pale upande wa pili wanapojazia mafuta mule hao wanaopaki wabunge wanaopaki njee wahuni tu kuvizia vitoto vya CBE hapo
 
ikulu ya USA white house kwanzia saa 2 asubuhi hadi saa 6 na nusu mchana unaruhusiwa kwenda kutalii muda mrefu raia wamejaa ikulu kama kukaa mbali na watu ndo ulinzi wangeanza jamaa wa Washington kuzuia raia wasisogee
 
Back
Top Bottom