UPDATE: Padri afikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kulawiti watoto 10 Moshi

UPDATE: Padri afikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kulawiti watoto 10 Moshi

Ki ukweli ni jambo la kusikitisha sana hasa kwa familia ambazo watoto wao wamekutwa na madhila hayo, inaumiza kama mzazi ni maumivu yasiyoelezeka. Huyo padri afungwe miaka yake anayostahili. Ameiaibisha jamii ameliaibisha kanisa.

Binafsi naona hata wakiruhusiwa kuoa bado kama mtu ni fuska ataendelea tu. Wanaume wangapi wana wake zao bado wanachepuka? Bado wanatamani wake za watu na pia kubaka. Tuzidi kumuomba Mungu kila mmoja aishi maagano aliyoapa kwa Mungu. Kama ni mwanandoa kua mwaminifu na kama ni mapadri wawe pia waaminifu kwani waliapa kumtumikia Mungu wakiwa hivo. Pole kwa familia zote zilizokumbwa na madhila hayo.
 
Roman katoriki nao wamepitwa na wakati.
Mwanamme rijali kumlazimisha asioe ni jambo lilipitwa na wakati.
 
UPDATES:

Sostenes Bahati Soka, Padri wa Kanisa Katoliki, Parokia Teule ya Mtakatifu Deonis Aropagita, Jimbo la Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro amesomewa mashtaka matatu katika Mahakama mbili tofauti. Padri huyo mwenye miaka 41, amesomeshwa mashataka hayo leo Jumatatu, Septemba 26, 2022 kwa nyakati tofauti akianza na Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kisha Mahakama ya Wilaya ya Moshi.

Kesi ya kwanza ilisomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Salome Mshasha ambapo Padri huyo anakabiliwa na shtaka moja la kumbaka mtoto wa miaka 12. Wakili wa Serikali, Kasimu Nasiri amesema upelelezi wa kesi hiyo umekamilika

Mshtakiwa huyo amekana shtaka hilo huku Wakili wa Serikali, Kasimu Nasiri akisema upelelezi umekamilika na Hakimu Salome ameiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 10, 2022 ambapo atafikishwa kusomewa maelezo ya awali. Mshtakiwa huyo alitakiwa kuwa na wadhamini wawili wakazi wa Kilimanjaro ambao wawe na uwezo wakuweka bondi ya Sh10 milioni, kika mmoja.

Padri Soka amekosa dhamana kutokana na wadhamini kutokidhi vigezo. Katika kesi nyingine, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya, Erasto Phily mshtakiwa huyo amesomewa shtaka moja la ubakaji wa mtoto. Kesi hiyo namba 349 ya mwaka 2022, mwendesha mastaka wa Serikali, Verediana Mlenza na Nitike Immanuel wamesema upelelezi umekamilika. Hata hivyo, mshtakiwa huyo amepata dhamana na kesi hiyo itakuja tena Oktoba 12, 2022 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.

Aidha, katika kesi ya tatu, padri huyo ameshtakiwa kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 12, eneo la kanisa alilokuwa anahudumu. Kesi hiyo ya Jinai namba 44 ya 2022, imetajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Jenipha Edward ambapo padri huyo nadaiwa kutenda kosa hilo Agosti 2022. Waendesha mashtaka wa Serikali, Kambarage Samson na Veridiana Mlenza wameieleza Mahakama hiyo upelelezi umekamilika.

Mshtakiwa ameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili wa kuweka bondi ya Sh2 milioni. Kesi hiyo imehairishwa hadi Oktoba 18, 2022 ambapo kesi itakuja kwaajili ya kusomewa maelezo ya awali
==============================

Vitendo vya udhalilishaji wa kingono kwa watoto vinazidi kuitikisa nchi na sasa padri mmoja wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuwabaka na kuwalawiti watoto zaidi ya 10.

Watoto hao ni wanafunzi wa kuanzia darasa la sita hadi kidato cha kwanza waliokuwa wakihudhuria mafundisho ya komunio ya kwanza na kipaimara.

Inadaiwa kila alipomaliza haja zake, padri huyo humpa kila mmoja kati ya Sh3, 000 na Sh5,000.

Wakati Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, akikataa kuthibitisha au kukanusha kukamatwa kwa padri huyo, Mkuu wa Mkoa huo, Nurdin Babu amethibitisha uwepo wa tukio hilo alilosema “ni baya linalofedhehesha”.

Tukio hilo ambalo ni la kwanza kusikika likifanywa na kiongozi wa dini mkoani Kilimanjaro, huku likihusisha idadi kubwa ya wanafunzi, limeibua taharuki kwa wazazi na walikuwa wamejipanga kuandamana kwenda kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Wananchi hao walikuwa wamepanga kuandamana kwenda kwa Waziri Mkuu aliyekuwa mgeni rasmi katika Siku ya Amani Duniani ambayo kitaifa ilifanyika mjini Moshi, ili kupaza sauti zao kutokana na kigugumizi cha kukamatwa kwa padri huyo.

Baada ya polisi kupata fununu za wazazi kujipanga kuandamana na mabango kwenda kwa Waziri Mkuu, ndipo jioni ya Septemba 20, siku moja kabla ya kiongozi huyo kuwasili mkoani Kilimanjaro, walikwenda kumkamata.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa alipotafutwa juzi ofisini kwake kuzungumzia uwepo wa tukio hilo, alikataa kuthibitisha au kukanusha kukamatwa kwa padri huyo zaidi ya kusema wanaendelea kuchunguza tukio hilo.

“Siwezi kusema kama tumemkamata au hatujamkamata, ila suala hili tunaendelea kulichunguza ili kujua ukweli wake, kwa sababu tuhuma hizi zinaelekezwa kwa kiongozi wa dini, hatuwezi kukurupuka kutoa taarifa,” alisema Maigwa.

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali, zinadai kuwa baada ya wazazi, kubaini watoto wao kufanyiwa vitendo hivyo, walitoa taarifa hizo kwenye vyombo husika ikiwemo uongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi na Polisi.

Jina la padri huyo na kituo chake cha kazi tunavihifadhi kwa sasa kwa sababu za kimaadili, hasa kwa kuwa hatujapata upande wake wala vyombo vinavyomshikilia.

Jana, gazeti hili lilimtafuta kwa simu Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi, Ludovick Minde na baada ya kuulizwa taarifa za padri huyo, alisema wapo katika kipindi cha sala, hivyo asingeweza kuzungumza chochote kwa wakati huo (ilikuwa saa 7:12 mchana).

Ilipofika saa 10 jioni Mwananchi, lilimpigia tena simu Askofu Minde ambapo ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

Hata hivyo, akizungumza na Mwananchi kuhusu tukio hilo, Mkuu wa mkoa Babu alisema tukio hilo lipo na kwamba ameviagiza vyombo vya usalama kwamba mtu yeyote atakayekamatwa kwa matukio hayo na ushahidi upo, hakuna kurudi nyuma wanapaswa kuchukuliwa hatua kali.

“Katika tabia mbaya zisizo za watu waliostaarabika ni hizo, inaonekana mkoa wetu umezidi kuwa na matukio kama haya. Naviagiza vyombo vya usalama kwamba mtu yeyote atakayekamatwa na ushahidi upo hakuna kurudi nyuma,” alisema RC Babu.

“Kwa sababu haiwezekani kiongozi wa dini kama huyo afanye mambo kama hayo yanayofedhehesha hata waumini wake. Mambo kama haya kwa nchi yetu ni ya kuchafua taswira ya mkoa na nchi na nitaomba mahakama impe adhabu kali,” alisema.

Hali ilivyo kanisani

Mwananchi lilifika katika kanisa analohudumu padri huyo na kukuta ofisi zimefungwa, lakini wahudumu waliokuwepo walidai padri huyo aliongoza ibada Jumapili Septemba 18 na baada ya hapo alienda kwenye mafungo.

“Baada ya misa ya Jumapili aliondoka kwenda mafungo na bado hajarudi, lakini Jumapili ijayo (leo) anaweza kuwepo, kama mnamuhitaji mnaweza kuja kumuona,” alisema mmoja wa wahudumu kanisani hapo ambaye hata hivyo hakutaka kutaja jina lake.

Vilevile, Mwananchi lilizungumza na wananchi wa kada mbalimbali wakiwamo madereva bodaboda wa eneo hilo, ambapo walionyesha kulifahamu suala hilo na kueleza kusikitishwa na kitendo kinachodaiwa kufanywa na kiongozi huyo.

Kauli ya wazazi "Tukio limetuumiza"

Mmoja wa wazazi wa watoto wanaodaiwa kufanyiwa kitendo hicho, alisema kitendo hicho kimemuumiza na kimemfanya apoteze imani kwa kuwa kiongozi wao huyo walimuamini na watoto walimchukulia kama baba yao.

Akisimulia namna alivyofahamu tukio hilo, alidai alipigiwa simu na mtu mmoja akimtaka amchunguze mwanaye kwa kuwa wapo watoto wanaodaiwa kubakwa na padri huyo na mwanaye ni miongoni mwa waliotajwa na wenzake.

“Mwanangu anasoma mafundisho kanisani hapo, nilipopata taarifa hizo, nilimbana akanieleza kuwa amekuwa akiingiliwa na padri huyo tangu Januari mwaka huu,” alisema mzazi huyo ambaye aliomba jina lihifadhiwe.

“Aliniambia wanapokwenda mafundisho, huambiwa waingie ofisini kuungama ambapo huingia mmoja mmoja na ndipo huwafanyia ukatili huo na kuwaambia kuwa wasiwe na shida na wamchukulie kama baba yao,” alieleza mama huyo.

“Taarifa hiyo iliniumiza sana, na ndipo nilipoenda kutoa taarifa kanisani na baadaye polisi, ambapo watoto ikiwemo wa kwangu walipelekwa hospitali ya Mawenzi na kubainika ameingiliwa, jambo ambalo mpaka sasa linaniumiza.”

“Kibaya zaidi baada ya kumbana na kunieleza ukweli, aliniambia baada ya kufanyiwa ukatili huo, hupewa Sh3,000 hadi Sh5,000 ambazo huenda nazo shule na sikuwahi kujua haya, mpaka nilipombana baada ya kuambiwa nimchunguze”.

Mzazi mwingine alisema hawezi kuzungumza kwa undani kuhusiana na tukio hilo kwa kuwa limemuumiza moyoni na limemuathiri mwanaye, kutokana na jamii inayomzunguka kufahamu unyama huo.

“Tukio hili limeniumiza sana, maana mwanangu bado ni mdogo amefanyiwa unyama na ukatili huo na aliyefanya ni kiongozi wa dini tuliyemuamini na hata watoto walipokwenda kanisani hatukupata shaka.”

Baadhi ya wananchi katika eneo hilo, walieleza tukio hilo limeibua taharuki kubwa na kuchafua hali ya hewa, kutokana na kudaiwa kufanywa na kiongozi wa kiroho ambaye wanasema ukimtazama ni mtu mnyenyekevu na asiyedhaniwa kufanya unyama huo.

“Watoto waliofanyiwa ukatili huu wameathirika sana, kwani wapo wanaosoma shule za hapa jirani na wanafahamika na baada ya tukio hili hawawezi kwenda shule kwa sababu ya kunyooshewa vidole na wenzao,” alisema.

Mkazi mwingine wa eneo lilipo kanisa hilo, alisema, “jambo hili limetushtua sana wananchi na baadhi ya wazazi tunaambiwa tayari wamewasitisha watoto wao kwenda mafundisho. Tunaiomba Serikali ilifanyie uchunguzi wa kina suala hilo ili kubaini ukweli wake,” alisema.

Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti mmoja wa kitongoji jirani na wananchi hao, alikiri kupata taarifa za watoto hao kufanyiwa ukatili huo na kwamba vyombo vya dola likiamo Jeshi la Polisi vinaendelea kulichunguza, hivyo viachwe vifanye kazi.

“Nikiwa mtaani hapa, nilipata taarifa za watoto 10 kufanyiwa ukatili na kiongozi huyo wa dini, naambiwa wazazi tayari walitoa taarifa kwa uongozi wa kanisa na polisi na tayari vyombo husika vimeanza kulichunguza,” alisema.

Matukio ya udhalilishaji wa kingono kwa watoto yanazidi kushika kasi na uchunguzi unaonyesha ndugu, walimu na viongozi wa dini hushiriki.

MWANANCHI
NAANDIKA KWA HERUFI KUBWA.HAFAI KUWA PADRE HUYO NA HERI AJIHUDURU AKADAKE NANGA HUKO MTAANI KAMA AMESHINDWA KUISHI USEJA.
 
Huyu Padri ilitakiwa asifikishwe mahakamani kwanza bali wazazi wa watoto waliofanyiwa unyama watafute mabandidu wa kitaa kimya kimya wamle kiboga huyu padri

Dawa ya mshenzi ni kumfanyia ushenzi tu,, bladfaken
 
Hao watoto waliofanyiwa hivyo ninwa kiume au wa kike? Inasikitisha sana, Mungu atusaidie.
 
Wtf is happening here?
Huyu mshenzi amelawiti na kuharibu maisha ya watoto 10! WATOTO 10??.. cha kushangaza kuna mbuzi zinacomment simple tu. Eti "Aisee hawa watu waruhusiwe kuoa tu" are you fucking joking?...WTF?.... unamaanisha unajaribu kujustify ufala na ushenzi sababu hajaoa?
Kwa hiyo wote ambao hawajaoa waanze kulawiti watoto? fuk this bitchiness.

Mtu yoyote anayeharibu watoto haijalishi ni nani au ana cheo gani anatakiwa achukuliwe ni "mshenzi" kama washenzi wengine. It seems like mapenzi ya dini yamewazidi waafrica mpaka inapelekea wachukulie vitendo vya kikatili na vichafu simplesimple.
Mnatakiwa muwe na hasira na maswala machafu kama haya ili kuhakikisha hayatokei tena na viongozi kuona wananchi wanachukizwa na huu uchafu ili kuchukua hatua kali! instead watu mnaandika na kuchukulia simple kama mmeona post ya celebrity. this shit is highly serious. where's your self respect? where's your fucking rage? fucking simpletons.

Mindsets kama hizo ndio zinapelekea kulea na kukuza watoto kipumbavu matokeo yake wanashindwa kujitetea na kuwa waoga na submissive. Mzazi unatakiwa kuwa mgumu, mkali na katili non-agreeable non-submissive kwenye maswala ya kipumbavu ili ukuze mtoto atakayekuwa kama wewe na atakayeweza kujitetea. hakuna father figures matokeo ndio haya.

Huyo mbwa akamatwe na anyongwe mpaka kifo ili iwe fundisho kwa mbwa wengine kama yeye haijalishi hata kama ana undugu na malaika.
Fuk everybody anayechukulia hili swala zito kirahisi. society is full cretins and maniac Aholes and sychopath just like in here! so fuk them all.
Mkuu em tafuta glass ya maji kwanza!
 
Manawalewa hao mashetani
Check majibu ya RPC na askofu
Kwani ni huyo tu? Makasisi na mapadri wa Kanisa katoliki wanayafanya hayo dunia nzima, tena hawakuanza leo wala jana, ni uozo wa miaka na miaka, Mpaka Umoja wa Mataifa umepiga kelele.
 
Kwani ni huyo tu? Makasisi na mapqdri wa Kanisa katoliki wanayafanya hayo dunia nzima, tena hawakuanza leo wala jana, ni uozo wa miaka na miaka, Mpaka Umoja wa Mataifa umepiga kelele.
Haya mambo yasipochukuliwa hatua kali yatakuja kuwa very dangerous maana nahisi shetani yupo kazini sasa
 
Dunia ya sasa sijui huko madrasa na makanisani hakuna usalama kwa watoto....
Mzazi unamuacha mtoto huko masaaa kadhaaa,mzazi ukiamini
Mtoto yuko sehemu salama
Kumbe mtoto huko wakati wowote
Anaweza zibuliwa mtaro

Ova
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Askofu akapokea simu halafu anakwepa kujibu swali eti wanafanya sala. Sasa alipokeaje simu kama wanafanya sala? Uongo mtupu.
Hili ni kosa la jinai. Liko nje ya nguvu za Askofu. Siku hizi padri au Askofu aakifanya kosa kama hili, hata kama yuko Vatican kwenye immunity, ruksa kukamatwa.
Ni moja ya dhambi inayokwaza vijana wengi kuwa waumini wazuri kanisani. Kanisa lazima libadilike. Mapadri wake wengi ni wahalibifu mno. Na wanalindana. Wale wanaosema ukweli wanatengwa na kunyanyaswa.
Ila kama waswahili wasemavyo, mficha maradhi, kifo kitamuumbua. Mapadre na Maaskofu, mbadilike. Rudini kwenye mstari. Tumechoka kugombania mademu bar. Na hili la watoto wadogo ni laana kabisa
 
Kwani ni huyo tu? Makasisi na mapqdri wa Kanisa katoliki wanayafanya hayo dunia nzima, tena hawakuanza leo wala jana, ni uozo wa miaka na miaka, Mpaka Umoja wa Mataifa umepiga kelele.
Ningeshangaa usiwepo kwenye huu uzi.
 
Back
Top Bottom