Upinzani bila kubadili siasa mtapata hasara kubwa Kwa Samia..


Wasioitaka CCM ni wananchi

Kwa tulipofika huhitaji fedha wala chochote kumshawishi mwananchi kuipigia kura chama pinzani,sababu tayari asilimia kubwa ya watanzania wameshakinaiwa na CCM


Tume ya uchaguzi,dola na mengine ndio yanayoendelea kuiweka CCM madarakani & nothing rather than that ushahidi tosha ni chaguzi kuu 2020
 
You are right about 2020, lakini je kutoitaka tu CCM inatosha? Ok assume tume iwe fair, kuna mbadala wa ccm kwa sasa?
 
Yaani kifo cha JPM kimezika kabisa upinzani

Kisiasa walitakiwa wanyakue agenda zake na kumlazimisha mama aendelee nazo....walikurupuka vibaya

wangekosoa uhuru wao tu wa siasa na wananchi angehamia upande wa upinzani....na kuiacha CCM inajizoa zoa
Kofia naiinua, sikudhani kama unao muono wa ndani kama huu, nilifikiri ni sisi wa chache sana wenye kutafakari na kuona. Asante.
 
The reverse is true, uwerevu wa wananchi ndio faida yako.

Swali pana hapa ni huo uwerevu uwe kwenye nini? Hakuna siku binadamu akawa mwereu kwa kila jambo.
 
Andiko lako liko vizuri sana lakini kuna mahali umeteleza mkuu
 
Umeongea ukweli..japo sina wasiwasi. Upinzani upo na watu smart sana kama Mbowe
Siku Mbowe akiwa smart, nitarudi upinzani kabla jua halija chomoza.

Wewe mwana siasa uliye pevuka lazima ufahamu kuwa Mwendazake alikuwa na constituency yake, na kwa hiyo kisiasa lazima uirithi.
Chadema ina mpango gani kisiasa kufaidika na kifo cha Mwendazake?

Mwendazake, aliichukua Constituency ya Chadema, watu wa chini wote kimaisha na kibiaashara lakini hakuwapa manufaa ya kuridhisha, hapo ndio chama kinazoa wanachama na wafuasi.
 
Mkaruka unakosea kutumia wishful thinking kwa jambo ambalo imekuwa ajenda yao toka vyama vya siasa vianzishwe.

Kwa katiba ya sasa vyama vya upinzani havitaweza kutawala kwa amani bila kufanya system overhaul na system overhaul itawezekana tu kwa kufanya mabadiliko makubwa ya kikatiba.

Vyama vya upinzani vikiingia madarakani ni lazima vitafanya hayo mabadiliko ili viweze kutekeleza sera zake.
 
Ipo tofauti, lakini ni kidogo sana. Wenye kutoa maoni kwenye mitandao na uongozi wa vyama vya upinzani. A symbiotic relationship.
 
Mkuu huku mwisho umemalizia vizuri na kwa uhalisia.

Sisi wakazi wa Wilaya ya Hai, vijana wengi ni wapenzi wa Chadema lakini ni ukweli usio na kigugumizi chochote ya kuwa wazazi wetu wengi wanaipenda CCM.
Na tunaishi na wazazi wetu na tunafurahia maisha.
 
Usiwasemee wananchi unaweza ukawa sio sahihi.
 
Kwa sasa hatuna Wapinzani kabisa na naona watatoka ndani ya CCM km ilivyokuwa G55
kweli Mpinzani unadai Hotuba ya mama Samia ilikuwa dk 1 tu kuzungumzia upinzani?
unadai ulipwe mafao na gari yako iliyopigwa risasi na kuzuiliwa, ufutiwe kesi km huna umuhimu baki Ubelgiji
Mpinzani unadai Magufuli kachukiwa kwa kifo cha Ben Saanane wakati walioumizwa ni wengi, tuna ndugu zetu walifukuzwa kazi kwa uonevu, Vyeti fake, umri bado, ukabila nk
Wapinzani watatoka ndani ya CCM km kina Nape, Gambo nk
Katiba mpya na Tume bado muda upo kwa sasa Wapinzani wa kweli waanze na makosa ya mwendazake lkn kwa CHADEMA bado nasema hakuna
Gambo hana nguvu km Lema kwa wananchi, lkn kwa sasa ndiye atakuwa mpinzani anayeleta mabadiliko kwa Wananchi wa Arusha, sio maandamano
cc

BAK

 
wapinzani waliingiza emotion issue ya JPM, na wakasahau siasa ni wakati JPM kaondoka nao😂
Kweli kabisa na sasa hivi wataongozwa na Jemedari Shibuda sio kila mmoja aende akanywe chai au kuelza matakwa yake binafsi, nirudishiwe shamba langu au mafao yangu. Agenda zote zipitie kwa John Shibuda au Francis Mutungi
 
You are right about 2020, lakini je kutoitaka tu CCM inatosha? Ok assume tume iwe fair, kuna mbadala wa ccm kwa sasa?

Binafsi naona awamu iliyopita haikufanikiwa kuua upinzani hata kama juhudi zote zilizofanywa kuanzia 2015 mpaka 2020 na ndio maana ndio maana kulihitajika msaada mkubwa wa tume na dola ili kupata kiti

Upinzani unatokana na madhaifu yanayotokana na mtawala ambapo kwa hapa kwetu bado mtawala ana madhaifu mengi sana ambayo hata hafahamu anaanzia wapi kuyarekebisha

Kwahiyo penye chaguzi huru na haki bado mtawala anaachia nchi kwa upinzani huu huu ambao mnadhani kua ume expire
 
Kabisa.

Na huwezi kusema eti kwa kua wewe humpendi ama sio shabiki wa ccm basi watanzania wote sio mashabiki wa ccm wakati unajua kabisa kuna wengine tena ndugu zako wanaipenda ccm.
 
Unaogopa sana demokrasia wewe.
 
Nimeipenda hii!.
P
 
Kama sera zipi hizo zinazohitaji system overhaul ??
 
Uko sawa kuhusu mapungufu ya watawala sana tuu, lakini kwa mimi ambaye nilishiriki uchaguzi na kuufuatilia ki utafiti na kwa vigezo, naona bado sana kwa upinzani kipigiwa kura za ushindi.

Nilitumia muda wa kutosha kupita kanda ya Magharibi na kuungana na watafiti wengine Kaskazini ambako ni nyumbani.

Matokeo:
Mwendazake katika utawala wake aliweza kuaminiwa na kuwaunganisha vizuri kanda ya Magharibi, Mara, Mwanza, Simiyu,Shinyanga, Geita, Kagera, kigoma, Tabora, Rukwa, Katavi na Songwe, Ruvuma, Mtwara, Iringa, Morogoro. Na alifanikiwa kuwaunganisha watanzania wanaoishi sehemu mbali mbali nchini mwetu lakini wana asili ya Mikoa hiyo. Kama ilivyo kawaida ya kisiasa upinzani kwa hizo jamii bado upo.

Maeneo yaliyokuwa na upinzani kabla:

Tunadanganyana sana humu kwenye mitandao, lakini wapiga kura waliokuwa wanaishi mkoa wa Kilimanjaro walikuwa na mawazo tofauti na sisi tunaishi nje ya Mkoa wa Kilimanjaro lakini tuna asili ya huko.

Wao walihamishia kura zao CCM, sisi tukiwa bado upinzani na tulio wataka wawe wabunge, huko majimboni, wao walikuwa hawawataki na hii ilikuwa wazi kwenye majimbo mengi tu.

Na hata maelezo ya wizi wa kura wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro ambao wanaishi Kilimanjaro hawaelewi hilo. Na hili ni kuanzia Same mpaka Siha.

Upinzani lazima upiganie kura za Mwendazake uzirithi ili kuchukua nchi. Tutabeza, tutadhihaki lakini ukweli unabaki kuwa kuna kura za kupoteza kama hatuto tupia jicho na kuzipata kura za Mwendazake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama sera zipi hizo zinazohitaji system overhaul ??
Unaposema unahitaji kuleta utawala bora lazima uanze na katiba.

Unaposema uboreshe mifumo ya haki za binadamu lazima uanze na katiba.

Katiba inasema nchi ni ya ujamaa na kujitegemea unatekeleza vipi sera za kibepari bila kuondoa kwanza hiyo blah blah ?

Ndiyo maana ccm wanaendesha nchi kwa mihemko na matamanio binafsi ya rais kwa sababu sera zao zote hazina msingi wa kikatiba.

Unaposema utaleta taasisi imara utaunda vipi taasisi imara bila kuwa na katiba inayoweka misingi ya taasisi imara ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…