Upinzani bila kubadili siasa mtapata hasara kubwa Kwa Samia..

NAKED truth umeandika
 
Hivi mnatumiaga viungo gani kufikiri hadi kuandika hivi...kama huu ujinga ulioandika una ukweli kwanini mlitumia bunduki ujinga huu ambizianeni huko kwenye korido zenu

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Ukimkosoa Mama kwa hoja hana ujanja wowote , pamoja na yote huyu ni miongoni mwa walioharibu Katiba mpya hadharani na gizani , faili lake lipo , tunamwangalia tu atakachofanya
Halafu mtoa mada ajue tunaonekana kufurahia uwepo wa Mama sio kwa sababu tunampenda au tunamkubali hapana,Bali tunafurahi Chinjachinja muasisi wa Wasiojulikana hayupo madarakani.

Kama vile sio kwamba watu walifurahi kwa sababu kafa,hapana,kwa sababu kila mtu atakufa.
Tulichofurahia Ni Mtu katili yule kuondoka madarakani.
Tungeweza kufurahia kuondoka kwake madarakani hata ingekua kwa
Kupinduliwa,
Kuugua na kushindwa kuendelea na majukumu yake,
Kujiuzulu,
Kushindwa uchaguzi,
Kutoroka nchi,
Ama vinginevyo ilimradi angeondoka kwenye kiti kile mtu dhalimu yule.

Mtoa mada hajui upinzani up tu mioyoni mwa watu,Kuna watu Hatuipendi CCM tu Kama tusivyompenda shetani.
Kama wanaamini mama anapendwa Basi uchaguzi ujao uwe wa haki.Tume huru na Katiba mpya waone mziki wake.

Wamesahau kwama hata wakati Jiwe anaingia madarakani alipewa kila aina ya sifa,lakini Leo kafa kaitwa kila aina ya Jina baya.

Leo namsifu Mama kwa sababu anafuta Mambo ya Jiwe ila siku ya Uchaguzi msimamo wangu Ni Chadema wasimamishe kitu chochote Mimi nitakipigia kura. Ninaposema kitu namaanisha kitu kweli,awe mtu ama gogo ilimradi limesimamishwa na CDM nitalipigia kura.
Kuendelea kuichagua CCM Ni kuendelea kuwachagua akina Lusinde,msukuma,Ndugai na wajinga wengine.Tuanchotaka sisi Ni kubadilisha kabisa Mfumo.
 
Huo ndiyo ukweli husika na Chadema haina chochote cha kubadilisha kama walivyomkabili dikteta ndiyo hivyo hivyo wamkabili Mama kama ATADEMKA atajijua yeye na maccm yake masuala ya kuongoza nchi kwa uwazi, haki na kuheshimu sheria za nchi ikiwemo Katiba, Bunge na mahakama pia kupatikana kwa Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi kabla ya 2025 yote hayo HAYAKWEPEKI.
 
Hivi mnatumiaga viungo gani kufikiri hadi kuandika hivi...kama huu ujinga ulioandika una ukweli kwanini mlitumia bunduki ujinga huu ambizianeni huko kwenye korido zenu

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
Broo umeandika kitu kizito Sana ,CCM huwa kweli wanaondolewa asilimia 95 ya akili wanabakishiwaga asilimia 5 tu kwa ajili ya kupeleka chakula mdomoni badala ya puani,ya kukumbuka kuvaa nguo na kwa ajili ya dharula ndogondogo Kama kuvukia barabara na vitu Kama hivyo.
Uchaguzi mkuu huu uliopita ndio umewavua nguo CCM na dunia nzima ikaona.
Yaani hadi Mimi mfuasi wa Upinzani nikawa naona aibu Mimi.
 
Swadakta
 
Reactions: BAK
Narubongo,

..Upinzani lazima wabadili mwenendo na ajenda zao baada ya kifo cha Magu na ujio wa Mama Samia.

..CCM nao lazima wajipange upya kutokana na mazingira ya kisiasa baada ya kifo cha Mwenyekiti wao.

..Nakubalina na mtoa mada kwamba, Mama Samia, kutokana na haiba na jinsia yake, anaweza kupata huruma na heshima fulani toka kwa wananchi. Na nakubaliana na mtoa mada kwamba wapinzani wanapaswa kulielewa hilo na kutafuta namna bora ya ku-deal na Rais na Mwenyekiti wa CCM wa aina hiyo.

..Mama Samia naye anapaswa kuelewa kwamba wananchi wana mategemeo fulani naye. Hii HESHIMA ambayo wanampa asiitumie vibaya. Kwa mfano, nini kitatoke ikiwa Mama Samia ataanza kutawala kwa mkono wa chuma kama Magufuli? Siamini kama wananchi wanategemea uhuni-uhuni, ukatili, na ubaguzi, na mambo mengine ya hovyo aliyokuwa nayo Magufuli ktk utawala wa Mama Samia.

..Je, ktk utawala wa Mama Samia ikitokea mpinzani mwingine akaumizwa kama alivyoumizwa Tundu Lissu wananchi watamchukuliaje Mama Samia na utawala wake? Je, ikitokea wapinzani wakaanza kufanyiwa vurugu, na dhuluma, na vyombo vya dola na mahakama, wananchi wataendelea kumheshimu Mama Samia? Je, kundi la WASIOJULIKANA likiendelea kutamba wananchi watatulizwa na kauli ya upole za Mama Samia?

..Kwa mtizamo wangu fursa na agenda za kisiasa zipo kwa kila upande. Kinachotakiwa ni kila upande kujipanga kuzitumia fursa hizo. Vilevile ni vizuri mazingira ya kisiasa yakawa ya HAKI SAWA kwa kila mwenye nia ya kufanya siasa hapa Tanzania.
 
Jiwe alichokwa na watu wenye akili timamu na wanaojielewa.
 
You guys have you ever had an engagement on policy issues with politicians of Tanzania? .

I am a very close friends to many in opposition ? I also have many politicians pro government, for smooth operation of my businesses, I seldom engage both on political issues and governance .

This engagement has led me to believe that, there is a thin line separates both.

Together tuimarishe serikali yetu, nafikiri sio kweli kabisa tutakuwa salama opposition wakitawala.
Tulichagua opposition Hai, uongozi wote kwa miaka 20, Kwa tulioyapitia leo wakazi wanaoishi Hai wanamwita Sábaya kijana wao.

Watanzania echos zimebadilika sana.
 
Naamini kama ungekuwa na close personal engagement na pande zote mbili na ukawa mkweli naamini usingeandika uliyo andika. Kuna taabu kubwa. Njia aliyoitumia Mwendazake sikuipenda, lakini nia na ujasiri wake kutaka kupunguza matatizo ya integrity namuunga mkono.

Wengine hatuzungumzi kwa kufikiri au kushawishiwa, tuna mabinti na vijana wa kuwazaa katika highest echelon in government leadership.

We have to revisit our ethos.
 
Acha uwongo, wakupe Lori la pesa bado huipendi, kwa hiyo wewe siasa ni ushabiki na sio maisha? Hufai kuchangia hapa unatupotezea muda na kujaza kurasa tuu.
 

Kwa maelezo haya najiuliza kama “upinzani” una muhimu kwenye siasa za Tanzania. Je, wananchi/Watanzania tunahitaji kuwa na wanasiasa wa upande wa upinzani? Je, tunahusika, tunaelewa na tuna interest na masuala wanayoyapambania?

Au ni vikundi vya wanasiasa wenye maslahi yao binafsi wanayoyatafuta serikalini na inabidi watumie mbinu na mikakati maalum kutushawishi Wananchi tuwaunge mkono ilhali sisi tunaelekea kuwa “more sympathetic” na Rais na serikali yake?

Kama ni hivyo, hatuna haja na upinzani. They might as well close shop and look for other vocations.

LAKINI kama upinzani ni muhimu na unahitajika isipokuwa vyama vya upinzani vilivyopo sio makini, basi tuhamasishane kuanzisha upinzani makini badala ya kuhangaika kutoa ushauri kwa failures (if that’s the concern). Hakuna mwenye monopoly na upinzani.

Huwa sioni sawa kuona wengi wakichukulia “upinzani” kama brand na shughuli ya kina Mbowe, Lissu, Zitto, Lema, n.k. pekee.

Inatolewa kauli kama “wasipobadili namna wanavyofanya siasa kuna hatari watatoweka au watakuwa irrelevant kwenye siasa za Tanzania”! Au, even worse: “...upinzani utakuwa irrelevant Tanzania”! So what? Je, hao wakipotea ndio mwisho wa upinzani Tanzania? Kama itakuwa hivyo (upinzani ukiwa irrelevant) tatizo liko wapi?
 
As usual, you have never disappointed Ndugu The Boss
 
What is "closed personal engagement"?

Nipinge nilichoandika hapo kwa hoja, kuwa na mabinti serikalini kwangu sio hoja, ni kujimwambafai.
 
Hivi mnatumiaga viungo gani kufikiri hadi kuandika hivi...kama huu ujinga ulioandika una ukweli kwanini mlitumia bunduki ujinga huu ambizianeni huko kwenye korido zenu

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
Kila unavyo chambua kwa kudhania kudhania huwezi kujua hali halisi.
Furahisha jukwaa, lakini sisi hutukuwataka wabunge tulio letewa. Sijui sehemu nyingine lakini mkoani kwetu hata uchaguzi ufanyike leo kama wagombea wa upinzani ni wale wale matokeo bado yatabaki hivi hivi.
 
Pole sana.
 
What is "closed personal engagement"?

Nipinge nilichoandika hapo kwa hoja, kuwa na mabinti serikalini kwangu sio hoja, ni kujimwambafai.
Kutoheshimu utawala bora upo katika public institutions ( the very meaning ya public institution, iwe CCM, CHADEMA, CUF na vyama vingine ) zote, tumekosa ubunifu wa kutatua matatizo ya kijamii bila kuumizana kimwili, kiihisia na kiuweredi. ( kwenye chama hata kama um elimika vipi, hutakiwi na mwenyekiti wewe ni mjinga tuu. Na kilaza kapendwa na mwenyekiti ili amlalie basi yeye ana maarifa na akili nyingi)

Uchu wa madaraka na pesa upo wa hali ya juu mno kiasi wahitaji hawataki kufuata njia za kiustaarabu kufikia wanacho kitaka.

Watu wanajali matokea bila kujali process. Suala na kupata matokeo tuu kitakiwacho, Matumizi ya elimu na ujuzi imekuwa sio kitu muhimu kama unapata matokeo.

Viongozi wote wamekuwa miungu watu katika hizo taasisi za umma.
Uhusiano mzuri hautegemei uwezo wako wa akili bali hali ya kipesa na instruments zinazo kulinda na Ushabiki.

Kuna ubinyaji wa demokrasia katika vyama vyote na ni kundi dogo walilokubaliana ndilo linalo tawala chama na sio uongozi uliochaguliwa.

Matumizi ya pesa yamekuwa yapo kufuata kiongozi atakavyo na sio kufuatana na mahitaji halisi ya chama.

Na mengine mengi tuu.
 
Mimi naona tuna upinzani imara sana, maana hawajabadilika no matter what. Wanaonekana wanahoja nzuri na ni wazalendo. Kwa sababu kama ingekuwa upinzani wanaangalia tumbo tu, hivi sasa hawana ubunge wala uwaziri vivuli,tusingewaona wakiwa na mission yoyote kisiasa wangesambaa.
Kuhusu kukosoa sidhani kama kunastaha kwenye kukosoa,kukosoa ni kukosoa tu. Hakuna lugha nzuri katika kukosoa jambo la msingi wasikilizwe penye tija parekebishwe.
Mfano mmoja ni Nape amekosoa maamuzi ya spika kuwabakisha wabunge bila kujali kwamba walifukuzwa na vyama vyao, ccm wamekuwa mbogo. Point ni Haijalishi umekosoaje,inategemea na utashi wa aliyekosolewa.
 
Naona unataka kuingilia maamuzi ya wengi kwa kuleta mashinikizo yako. Huyo mwenyekiti anapigiwa kura na wajumbe anashinda, sasa hapo huelewi kitu gani? tatizo mnataka mnaemkubali nyie ndio awe halafu yule anayekubalika na wengi asiwe, hiyo sio demokrasia.

Unaposema kuna kundi dogo linalotawala chama na sio uongozi uliochaguliwa wakati tunaona kura zinapigwa na mshindi anatangazwa na washindani wake, unataka kulazimisha rushwa ndio inatumika, nikikuuliza ushahidi wa hilo unao sijui kama utanipa jibu sahihi, kwangu kiongozi anaetumia rushwa ni yule asiekubalika, wengine record zao zinawabeba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…