Huyu Prigo siyo mtu wa mchezo. Siyo kichaa, anajua anachokifanya.
Kwanza analijua kikamilifu jeshi la Urusi, anazijua silaha za Urusi, anajua akiba ya silaha za Urusi, anajua msimamo wa wananchi walio wengi. Na kwa vyovyote vile atakuwa ana mawasiliano na baadhi ya makamanda wa jeshi la Urusi na wapiganaji pia.
Putin anaweza kujiona bado ana askari wengi, kumbe siyo askari wake. Ikumbukwe toka mwanzo, askari wa jeshi la Urusi, licha ya kuwa na silaha nyingi, kikubwa walichokuwa wamekikosa ni morali.
Ufahamu kuwa ndani ya hilo jeshi la Urusi, wengi ambao wamekuwa wanapelekwa mstari wa mbele, ni askari wasio na mafunzo ya kutosha. Ni wale walioandikishwa na kulazimishwa kwenda vitani. Na hilo lilifanyika baada ya Urusi kupoteza askari wake wengi elites mjini Kiev, na siku za mwanzo za mapigano kusini mashariki mwa Ukraine, vifo vilivyohusisha makamanda wa ngazi ya juu wa Jeshi la Urusi.
Askari hao wote wanaona kabisa kuwa maisha yao yapo hatarini kwa kuendelea kupigana nchini Ukraine. Kwao ni rahisi zaidi kupigana dhidi ya Serikali yao kuliko kuendelea kupigana Ukraine ambako nchi za Magharibi wameapa kuendelea kuisaidia Ukraine, hata kama vita itachukua zaidi ya miaka 10.