Urusi vs Wagner: Wagner wasitisha 'Uasi' na safari ya kwenda Moscow yasitishwa, wadai hawataki kumwaga damu ya Warusi

Nasikilizia kwa kusoma vyombo mbalimbali vya habari bila kukosa kusoma kupitia JF.

Mambo ni 🔥 kiukweli, kama sikosei niliona kupitia CNBC ndege ya Putin inapiga jaramba, japo msemaji wake ikulu anasema Putin bado yupo ikulu.

Pamoja na ndege za jeshi la Urusi kuwapiga kisawasawa Wagner, jamaa wana roho ngumu wanasonga mbele huku wakipewa moyo na wananchi wanaowashangilia, daaa aiseee!.
Nikupongeze sana kwa hilo la kusikiliza na kusoma vyombo mbalimbali vya habari inasaidia sana kuwa na uelewa mkubwa na kuwa na takwimu sahihi za uhakika kuhusu jambo husika likiwemo hili la Wagner kutaka kupindua serikali ya Urusi
 
Sisi waislamu tunawaona mayahudi ni wabaya kuliko wakristo.La kushangaza wakristo wengi wanawaona ni ndugu zao kuliko waislamu.

Kumchuki mtu kwa mlengo wa dini sababu tu dini yako imekwambia mchukie ni ujinga. Matter of fact you should qn your religion kama inasambaza chuki.
 
Huu ujasiri wa Prigo si bure, huenda ameona wazi kuwa Putin hachomoi na pia huenda anaungwa mkono na makamanda wa serikali au hata amepokea dau nono toka Nato
Huyu Prigo siyo mtu wa mchezo. Siyo kichaa, anajua anachokifanya.

Kwanza analijua kikamilifu jeshi la Urusi, anazijua silaha za Urusi, anajua akiba ya silaha za Urusi, anajua msimamo wa wananchi walio wengi. Na kwa vyovyote vile atakuwa ana mawasiliano na baadhi ya makamanda wa jeshi la Urusi na wapiganaji pia.

Putin anaweza kujiona bado ana askari wengi, kumbe siyo askari wake. Ikumbukwe toka mwanzo, askari wa jeshi la Urusi, licha ya kuwa na silaha nyingi, kikubwa walichokuwa wamekikosa ni morali.

Ufahamu kuwa ndani ya hilo jeshi la Urusi, wengi ambao wamekuwa wanapelekwa mstari wa mbele, ni askari wasio na mafunzo ya kutosha. Ni wale walioandikishwa na kulazimishwa kwenda vitani. Na hilo lilifanyika baada ya Urusi kupoteza askari wake wengi elites mjini Kiev, na siku za mwanzo za mapigano kusini mashariki mwa Ukraine, vifo vilivyohusisha makamanda wa ngazi ya juu wa Jeshi la Urusi.

Askari hao wote wanaona kabisa kuwa maisha yao yapo hatarini kwa kuendelea kupigana nchini Ukraine. Kwao ni rahisi zaidi kupigana dhidi ya Serikali yao kuliko kuendelea kupigana Ukraine ambako nchi za Magharibi wameapa kuendelea kuisaidia Ukraine, hata kama vita itachukua zaidi ya miaka 10.
 
Hapo ulipomalizia sasa "kweli counter offensive imekuwa ya AKILI zaidi badala ya nguvu". Mkuu hiyo ndiyo tofauti kati ya kupigana na mzungu na mwarabu.
Ha ha ha waarabu weusi wakikusikia watakuporomoshea matusi.
 
Sisi waislamu tunawaona mayahudi ni wabaya kuliko wakristo.La kushangaza wakristo wengi wanawaona ni ndugu zao kuliko waislamu.
Kwa sababu ya kupigana vita na Pakistan ndio mnawaona wabaya?
 
Pia huo ndio utakuwa mwisho wa Wegnar ambapo itamlazimu Urusi kuwatoa wanajeshi wake kwenda kupigana Ukrain kitu ambacho Putin alikuwa hataki.

Yani hii hali ya leo imekaa vibaya sana kwa Putin.

Toka mwanzo nilikuwa nasema hii vita ni faida tupu kwa USA na washikrika wake
Tuliwahi kusema humu, ni ngumu kujua CIA wanawaza nini juu yako.
 
Huyu Prigo siyo mtu wa mchezo. Siyo kichaa, anajua anachokifanya.

Kwanza analijua kikamilifu jeshi la Urusi, anazijua silaha za Urusi, anajua akiba ya silaha za Urusi, anajua msimamo wa wananchi walio wengi. Na kwa vyovyote vile atakuwa ana mawasiliano na baadhi ya makamanda wa jeshi la Urusi na wapiganaji pia.

Putin anaweza kujiona bado ana askari wengi, kumbe siyo askari wake. Ikumbukwe toka mwanzo, askari wa jeshi la Urusi, licha ya kuwa na silaha nyingi, kikubwa walichokuwa wamekikosa ni morali.

Ufahamu kuwa ndani ya hilo jeshi la Urusi, wengi ambao wamekuwa wanapelekwa mstari wa mbele, ni askari wasio na mafunzo ya kutosha. Ni wale walioandikishwa na kulazimishwa kwenda vitani. Na hilo lilifanyika baada ya Urusi kupoteza askari wake wengi elites mjini Kiev, na siku za mwanzo za mapigano kusini mashariki mwa Ukraine, vifo vilivyohusisha makamanda wa ngazi ya juu wa Jeshi la Urusi.

Askari hao wote wanaona kabisa kuwa maisha yao yapo hatarini kwa kuendelea kupigana nchini Ukraine. Kwao ni rahisi zaidi kupigana dhidi ya Serikali yao kuliko kuendelea kupigana Ukraine ambako nchi za Magharibi wameapa kuendelea kuisaidia Ukraine, hata kama vita itachukua zaidi ya miaka 10.
Kimeumana
 
Back
Top Bottom