Urusi vs Wagner: Wagner wasitisha 'Uasi' na safari ya kwenda Moscow yasitishwa, wadai hawataki kumwaga damu ya Warusi

Urusi vs Wagner: Wagner wasitisha 'Uasi' na safari ya kwenda Moscow yasitishwa, wadai hawataki kumwaga damu ya Warusi

Mapigano ya kwanza yameripotiwa kati ya wapiganaji wa Wagner na jeshi la Urusi katika mji wa Rostov. Wanajeshi wa Urusi walikuwa wameweka vizuizi vya barabarani lakini Wagner wamesambaratisha vizuizi hivyo. Wanajeshi 38 wa Urusi wamejisalimisha kwa wapiganaji hao. View attachment 2667271
Wagner ni battle hardened na ndo waliwasumbua sana Ukraine na Ukraine ilikiri hilo
 
Huu mpango umesukwa na West na kwa hakika Kuiangusha Russia ni pigo kwa Dunia nzima tutaambiwa tuwr mashoga woote ....naamini West watatumia vizuri ssna huu mtego kuishambulia Urusi vikali sana na hivyo hata jaribio la kumuua Putin litafanywa na ikiwezekana watamuua hapa hapa katika huu mzozo..Sioni kama Putin atanusurika na hili. MASHETANI yanatuumiza kwa kuisambaratisha Urusi..dah hii ni jambo baya sana...

Jana niliangalia wale maseneta 2 Graham na mwenzake wakiongea kwa codes nikajua kuna jambo haliko sawa sawa
 
Mkuu wa kundi la mamluki la Wagner nchini Urusi ameapa "kufanya kila awezalo" kupindua uongozi wa kijeshi wa Urusi, saa chache baada ya Kremlin kumshutumu kwa "uasi wa kutumia silaha".

Yevgeny Prigozhin alisema wapiganaji wake wa Wagner wamevuka mpaka kutoka Ukraine na kuingia katika mji wa Rostov-on-Don nchini Urusi.

Bw Prigozhin alisema wapiganaji wake watamuangamiza yeyote atakayejaribu kuwafungia njia.

Mkuu wa mkoa huo aliwataka wananchi kuwa watulivu na kusalia majumbani.

Bw Prigozhin alidai kuwa vikosi vyake viliidungua helikopta ya kijeshi ya Urusi ambayo "ilifyatulia risasi msafara wa raia". Hakutaja eneo na madai hayo hayajathibitishwa.

Kundi la Wagner ni jeshi la kibinafsi la mamluki ambalo limekuwa likipigana pamoja na jeshi la Urusi nchini Ukraine.

Mvutano umekuwa ukiongezeka kati yao kuhusu jinsi vita hivyo vinavyoendeshwa, huku Bw Prigozhin akikosoa uongozi wa kijeshi wa Urusi katika miezi ya hivi karibuniIjumaa usiku katika maeneo muhimu mjini Moscow, yakiwemo majengo ya serikali na vyombo vya usafiri, shirika la habari linalomilikiwa na serikali ya Urusi TASS lilisema.
Gavana wa eneo la Lipetsk nchini Urusi pia anawaomba wakaazi wasisafiri kuelekea kusini.
Lipetsk iko karibu kilomita 280 (maili 175) kaskazini-mashariki mwa mpaka wa Ukraine, na zaidi ya kilomita 500 kaskazini mwa Rostov.
Katika chapisho kwenye mtandao wa Telegram, Igor Artamonov alisema hatua za usalama katika eneo hilo zinaimarishwa, kwa kuzingatia hasa kulinda vifaa muhimu vya miundombinu.
Katika ujumbe wa Twitter mwishoni mwa Ijumaa, Wizara ya Ulinzi ya Ukraine ilisema kwa urahisi: "Tunayaangalia."
Ikulu ya White House ilisema inafuatilia hali hiyo na itashauriana na washirika wa Marekani.
Jenerali Sergei Surovikin, naibu mkuu wa vikosi vya Urusi nchini Ukraine, ambaye uongozi wake Bw Prigozhin ameusifu siku za nyuma, alimtaka "kusitisha msafara wa wapiganaji wake na kuwarejesha kwenye vituo vyao".
"Sisi ni damu moja, sisi ni wapiganaji," alisema kwenye video. "Haupaswi kufanya masihara na adui wakati ambao ni mgumu kwa nchi yetu."
Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu
 
Back
Top Bottom