Urusi vs Wagner: Wagner wasitisha 'Uasi' na safari ya kwenda Moscow yasitishwa, wadai hawataki kumwaga damu ya Warusi

Urusi vs Wagner: Wagner wasitisha 'Uasi' na safari ya kwenda Moscow yasitishwa, wadai hawataki kumwaga damu ya Warusi

Wanajeshi zaidi ya laki 4 wa Urusi wameweka vizuizi 1800 katika barabara inayoelekea mji wa Moscow. Kila kizuizi kimoja kina wanajeshi zaidi ya 300 wa Urusi ili kuwazuia wapiganaji wa Wagner kufika Moscow. View attachment 2667541
Hii ndio sababu Russia haikuwa inapeleka wanajeshi wengi Ukraine. Hatari kubwa iko ndani kuliko nje, ona sasa hao wanajeshi wanatumika kulinda dhidi ya waasi.
 
Kuna watu hawajui PMC hawawezi kusonga mbele maana hawana ndege vita hawana baadhi ya ammunition walizokuwa wanapewa na Jeshi. Hivyo cant fight RF.
Vita vya ndani, ndege na mabomu huwa vina msaada mdogo sana. Ukivitumia sana, utawamaliza wananchi.

Na Serikali ikitumia ndege na mabomu, halafu ikawa inasababisha mauaji ya wananchi, kutatokea uadui mkubwa kati ya Serikali na wananchi.

Ukumbuke waliomwondoa Mrysi Kiev, ni wananchi.
 
Huo muda wa Russia kupigana kumaliza then kuja kuipiga Ukraine wanautoa wapi. Unakumbuka October revolution ya 1917, Russia ilipojitoa WW1 baada ya kupigwa na Bolsheviks walipochukua nchi hawakuendelea na vita tena. Walitumia muda wao kupigana wenyewe kwa wenyewe, kupigana na remnants za serikali iliyopita na kujiimarisha utawala wao.

Muda hauruhusu hao nationalists kupigana na Ukraine. Sababu ikitokea Putin hayupo kutakuwa na pro-Putins, nationalists na Wagners na washirika wao watakaoasi jeshini na usalama. Hapo Ukraine itarudisha maeneo mengi sana, itahitajika nguvu kubwa zaidi kupigana nayo kuliko walivyoanza au wanavyoendelea sasa. Serikali itakayoundwa na kudi lolote kati ya hayo matatu ikitumia nguvu kuingia Ukraine inayaachia makundi mawili mwaya wa kujijenga.

Kawaida ya coups au mutiny hufuatia counter-coups kama msipoelewana. Russia haina watu wenye nguvu na popular, Putin aliwaondoa. So akijitokeza mwenye ushawishi na nguvu akaungwa mkono atakuwa ndio anaanza na moja huo muda wa kuifikiria Ukraine hana.

Russia kuna factions na ubaguzi, mfano huyu Shoigu ndio kabisa hawezi waambia lolote. Mtuva mwenye asili ya Asia kutoka mji wa vichochoroni uko anawaambia Western Russians wa St. Petersburg na Central Russians wa Moscow. Ndio sababu Chechens walianzisha zile vita mbili, ukiwa wa mashambani uko kwenye ngano hakuna anayekuthamini. Shoigu kawekwa pale sababu hawezi ungwa mkono hivyo hawezi fanya mapinduzi.

Waziri Mkuu yule Mishustin kapoa kama uji wa mgonjwa, Kadyrov ni wakuja hawaambii kitu Warusi halisi, Dmitry Medvedev ni pro-Putin ila mnyonge na dhaifu mbele ya vyombo vyote, Dmitry Rogozin ni mwehu fulani anaweza leta chokochoko ila tangu HIMARS zimshambulie kwenye birthday party mwaka jana sijamsikia tena sijui operation aliyofanyiwa ilimuacha hali gani. Hapo juu anabaki mtu mmoja tu, mkuu wa usalama wa taifa ambaye inasemekana ndio alikuwa anaandaliwa kuwa mrithi wa Putin.

Atakayepita hapa itabidi aue vigogo kadhaa (hii itafanyika 100%, that's how Russia exist). Au yeye mwenyewe anaweza uwawa, mfano Prigozhin sio presidential material hata kidogo. Then uhamisho, kustaafisha watumishi muhimu, exiles, asylums, kuvunjika kwa baadhi ya organs za jeshi, polisi na usalama na mengine yatafanyika.
Ikiwa Putin atabaki tutarajie mabadiliko machache ila mauaji mengi na nadhani hatotaka kuendelea muda mrefu atawaachia msala usalama kama ambavyo Godfather wake alivyomuachia.
1. Mpaka hiyo coup itokee na ifanikiwe....
2. Na tofauti zao zote wanachofanana ni kitu kimoja, they all hate the West.
3. Unclear mpaka sasa nini kinaendelea, sababu hakujawahi na Coup ya hivi duniani ( nilizofanikiwa kuzisoma).
 
Nasikilizia kwa kusoma vyombo mbalimbali vya habari bila kukosa kusoma kupitia JF.

Mambo ni 🔥 kiukweli, kama sikosei niliona kupitia CNBC ndege ya Putin inapiga jaramba, japo msemaji wake ikulu anasema Putin bado yupo ikulu.

Pamoja na ndege za jeshi la Urusi kuwapiga kisawasawa Wagner, jamaa wana roho ngumu wanasonga mbele huku wakipewa moyo na wananchi wanaowashangilia, daaa aiseee!.
 
Mkuu dini za wakrsto zimetokana na dini za wayahudi......Utasemaje uyahudi umefanana na uislamu wakati uislamu umekopi kwa wayahudi na wakrsto....Ila waislamu hasa wenye chuki dhidi ya wayahudi waga wanajitahidi kusema wayahudi hawawapendi wakrsto wakati ukrsto umetokana na uyahudi
Hilo ni swali unapaswa kuwauliza wayahudi sio mimi.
 

Anaehitaji kujua mambo yanayoendelea link hii hapa ya telegram wanajiita intelslava ndio wako Frontline vitani.
Shukrani

Sent from my TECNO PR651H using JamiiForums mobile app
 
PUTIN HATISHIWI NYAU ILA ANATISHIWA NA WAGNER 🤣🤣🤣😊
Kabisa anasema NATO na US hawamtishi ona sasa anatishika na Wagner
Wanajeshi wa Urusi walikuwa wanqgoma kwenda kupigana huko Ukrain
Ndio sababu ya Putin kutumia mamluki
Alipoona haungwi mkono na jeshi la serikali kama commander in Chief alitakiwa ajiuzulu haraka hata kusingizia sababu za kiafya

Kuwatumia Wagner ilikuwa dharau.kwa jeshi ni sawa na kuwatukana kuwa to hell with you hata kama hamtaki nina jeshi langu la Wagner mbwa nyie
Kwani nyie Jeshi la serikali ni nani nyoko nyie mimi nina Jeshi langu la Wagner.

Eeh sasa.anavuna alichopanda baada ya Wagner kuona Putin hana support ya jeshi la wapiganaji wa serikali yuko tu na support ya maofisa tu wa wizara wala Chips, kuku makao makuu ya Jeshi na wizara ya Ulinzi wameamua Wagner kuchukua nchi sababu wanajua Putin hana Support kubwa ya wapiganaji washika silaha frontline sio desk officers wa makao makuu ya jeshi na wizara ya Ulinzi

Wapiganaji ndio mpango mzima.Wakiweka silaha chini Putin anaondoka
 
Kuhusu leo....?
Ni kwamba Prizoghin andai anataka Justice dhidi ya Ministry of Defence under shoigu and Gerasiminov ( wateule wa Putin).
Has nothing to do with holding cities or Political position ( mpaka sasa anadai hivyo).
Uja specify anataka haki ua nn?
 
Wapiganaji wa Wagner waelekea Moscow kuuondoa utawala wa kijeshi unaoongozwa na SERGEI SHOIGRU. Kiongozi wa Wagner anadai kwamba majeshi ya urusi yamekuwa yakishambulia kambi zao nchini UKRAINE.

Huu Uzi nitatoa update ya kila kinachoendelea.

=====
Update: Maafisa wa Ukraine wasema watatumia 'mapinduzi ya kijeshi' nchini Urusi kurejesha eneo lililochukuliwa

Katika tishio moja kwa moja kwa mamlaka ya Putin, Yevgeny Prigozhin, kiongozi wa Wagner, aliishutumu jeshi la Moscow kwa kupiga bomu askari wake na kudhibiti jiji muhimu la Urusi mapema asubuhi.

Kiongozi huyo mwenye msimamo mkali wa jeshi binafsi maarufu zaidi ulimwenguni aliahidi kwenda kwenye mji mkuu kwa kulipiza kisasi.

Katika hotuba isiyokuwa ya kawaida, Bwana Putin alilitaja tukio hilo kuwa "uhaini" na akasema wale wanaounga mkono vitisho na njia za kigaidi watapata adhabu isiyoweza kuepukika.

Rais wa Ukraine, Zelensky, alivunja ukimya na kusema kuwa hii ni mfano mwingine wa "udhaifu kamili wa Urusi".

=====

Mamlaka katika eneo la Lipetsk nchini Urusi waagiza watu kubaki nyumbani

Mamlaka katika eneo la Lipetsk nchini Urusi walitoa wito kwa watu kubaki ndani ya nyumba zao kwa sababu za usalama.

Walitoa onyo hilo kutokana na ripoti kuwa wapiganaji wa Wagner walikuwa wakitumia eneo hilo wakati wa safari yao kuelekea Moscow.

=====

Wagner wateka makao makuu ya jeshi la Urusi ukanda wa Kusini
Gavana wa Voronezh, nchini Urusi alisema Jumamosi kuwa huduma za dharura zilikuwa zikijaribu kuzima tanki la mafuta linalowaka katika kituo cha mafuta.

Zaidi ya askari zimamoto 100 na vifaa 30 vya kuzimia moto walikuwa wakifanyia kazi katika eneo hilo, alisema Gavana Alexander Gusev kupitia Telegram.

Awali Jumamosi, chanzo cha usalama nchini Urusi kiliiambia Reuters kuwa wapiganaji wa Wagner walidhibiti vituo vya kijeshi katika jiji la Voronezh, umbali wa kilomita 500 (maili 310) kusini mwa Moscow. Reuters hawakuweza kuthibitisha madai hayo.
=====

NDEGE YA RAIS YADAIWA KUONDOKA MOSCOW, WAGNER WAKIDAIWA KUKARIBIA MJI

Inadaiwa Wapiganaji wa Wagner wameendelea na mapambano na sasa wamefika katika Mkoa wa #Lipetsk, takriban Kilometa 450 kutoka Moscow

Aidha, inaelezwa kuwa Ndege za Kivita za Urusi zimeshambulia misafara ya Wapiganaji wa #Wagner na tayari Wanajeshi wameshajipanga katika nafasi za kuulinda Mji Mkuu, Moscow

Kiongozi wa Wagner, Yevgeny #Prigozhin amedai kuwa Wapiganaji wake wamepokelewa kama 'Wakombozi' na kuwa waliweza kuchukua Makao Makuu ya Kijeshi huko #Rostov bila mapigano

Katika hatua nyingine, imeelezwa kuwa Ndege ya Rais imeonekana kuondoka #Moscow, hata hivyo Ikulu imedai kuwa Rais #Putin bado yupo katika Mji Mkuu huo
Putin ameiangamiza Russia, hii Vita ya Ukraine imegeuka anguko lake.
 
Umeota hivyo? Kila mmoja akileta anachoota hapa JF, si itakuwa vurugu?

Hapa tunajadili hoja au habari. Mleta mada ameleta habari, wewe u aleta ndoto zako. Lipe heshima jukwaa.
Asipokuelewa mchape kibao
 
Back
Top Bottom