[emoji16][emoji16][emoji16] Ogopa sana watu wenye mawazo ya kimaskini! Kila kitu kwao ni uchawi. Ukimiliki hela halafu ukawa na tabia za kutojipenda, au huna hobby ya kupenda kuvaa vizuri, kula vizuri, au una tabia za ubahili! Tayari wanakutangaza ni mchawi! Mara sijui masharti ya mganga nk.
Kumbe utajiri kwa sehemu kubwa uko benki, usimamizi mzuri wa biashara, nidhamu na matumizi mazuri ya fedha, umakini, nk. Bahati mbaya hawa matajiri huwa hawapendi kujianika kwa kila mtu. Ila kiukweli wengi wana mikopo mikubwa benki kwa kutumia dhamana za vitu visivyo hamishika kama nyumba, mashamba makubwa yenye hati, nk! na mikopo hiyo kwa kiasi kikubwa, ndiyo iliyo wafikisha hapo walipo.