Tetesi: Usajili wa Mabasi ishirini mapya ya Abood

Tetesi: Usajili wa Mabasi ishirini mapya ya Abood

Humjui abood wewe,utakuwa umezaliwa juzi,kila nusu saa kuna gari inatoka msamvu kuja dar na dar kwenda moro,bado route za mikoa bado yanayokodishwa,reserve na yaliyo service
300 hayafiki mkuu, muda mwingine tusipende kukuza mambo. Hata mm nipo moro hapa na sehemu zake zote garage nk nazifahamu. Utajiri anao ila mabus miatatu uongo kabisa.
 
Asee wakuu kumbe kuna watu wana jax sana hii nchi. Nimeona huko Twitter kuwa huu ni usajili wa mabus 20 mapya ya Abood.

View attachment 1972491
Tutafute hela wakuu.
 
Asee wakuu kumbe kuna watu wana jax sana hii nchi. Nimeona huko Twitter kuwa huu ni usajili wa mabus 20 mapya ya Abood.

View attachment 1972491
Tutafute hela wakuu.
 
Mimi sijui idadi yake lakini sitasahau tukio la almost 20 years ago!!!

Nimefika zangu Ubungo nimekuta basi la kampuni fulani hivi (nimesahau jina lake lakini sio Islam) likiwa na watu zaidi ya robo tatu kama sio zaidi.

Wakati huo huo, basi moja ya Aboud ndo lilikuwa linajitayarisha kupakia abiria, na kwahiyo halikuwa na abiria hata mmoja!!

Sasa kwavile sikuwa na uzoefu na mabasi yaendayo Morogoro, nikapanda lile nililoona limejaa zaidi ya 3/4 huku nikiamini ndo nitawahi kuondoka!!

Kitu ambacho sitasahau, ziliondoka Aboud kama sio 4 basi 5 wakati basi letu lililokuwa limejanza zaidi ya 3/4 kabla yao tukiwa pale pale!!

Na ninachotaka kusema kwamba, labda siku hizi kwavile magari ni mengi lakini kwa wakati, hiyo nusu saa ingekuwa zinaondoka Aboud angalau 3 kwa route moja!!!
Hahahaha Huna makosa yeyote yule common sense ingemwambia apande hilo lenye 3/4
 
Mimi sijui idadi yake lakini sitasahau tukio la almost 20 years ago!!!

Nimefika zangu Ubungo nimekuta basi la kampuni fulani hivi (nimesahau jina lake lakini sio Islam) likiwa na watu zaidi ya robo tatu kama sio zaidi.

Wakati huo huo, basi moja ya Aboud ndo lilikuwa linajitayarisha kupakia abiria, na kwahiyo halikuwa na abiria hata mmoja!!

Sasa kwavile sikuwa na uzoefu na mabasi yaendayo Morogoro, nikapanda lile nililoona limejaa zaidi ya 3/4 huku nikiamini ndo nitawahi kuondoka!!

Kitu ambacho sitasahau, ziliondoka Aboud kama sio 4 basi 5 wakati basi letu lililokuwa limejanza zaidi ya 3/4 kabla yao tukiwa pale pale!!

Na ninachotaka kusema kwamba, labda siku hizi kwavile magari ni mengi lakini kwa wakati, hiyo nusu saa ingekuwa zinaondoka Aboud angalau 3 kwa route moja!!!
Waluguru huwaambii kitu kwa abood
 
[emoji23][emoji23][emoji23] halafu alisikika akimalizia "Bora nife njaa"
😁😁😁 Ogopa sana watu wenye mawazo ya kimaskini! Kila kitu kwao ni uchawi. Ukimiliki hela halafu ukawa na tabia za kutojipenda, au huna hobby ya kupenda kuvaa vizuri, kula vizuri, au una tabia za ubahili! Tayari wanakutangaza ni mchawi! Mara sijui masharti ya mganga nk.

Kumbe utajiri kwa sehemu kubwa uko benki, usimamizi mzuri wa biashara, nidhamu na matumizi mazuri ya fedha, umakini, nk. Bahati mbaya hawa matajiri huwa hawapendi kujianika kwa kila mtu. Ila kiukweli wengi wana mikopo mikubwa benki kwa kutumia dhamana za vitu visivyo hamishika kama nyumba, mashamba makubwa yenye hati, nk! na mikopo hiyo kwa kiasi kikubwa, ndiyo iliyo wafikisha hapo walipo.
 
Mimi ninadhani hicho ni kiwango cha kawaida tu kwa kampuni kama Abood. Hata alipoingiza hizi zilizopo sasa ni hivyohivyo tu. Ninakumbuka ilikuwa sherehe pale Msamvu, misele ya kufa mtu roundabout wakipokewa na bodaboda.

Ninafikiri kwetu wateja, muhimu sasa ni kuletewa basi zilizo comfortable na rafiki kimatumizi. Yutong tunazoletewa ni za kikuda sana. Pot za kuchajia zinadumu miezi,hazifiki mwaka. AC halikadhalika—ikishabuma mtakoma humo kwenye basi. Siti pia ni ndogoo,ukiwa mrefu ama kibonge imekula kwako.

Ninajua haya ndo huchangia kushusha bei ya basi huko sokoni uchina. Lakini,kwakuwa kampuni ina uwezo, ingia dau kubwa, lete chache za ukweli wenye uwezo wapande kwa bei elekezi. Wateja wapo. Tunaona BM ana zile zenye daraja la kwanza na la pili. Kila siku daraja la kwanza zinajaa fasta.

Halafu Abood kama mnanisoma acheni ubahili. Katikati ya Dar na Moro jengeni kahoteli uchwara ka kupata bites na kujisaidia. Mnahama vihoteli, mnapeleka abiria vihoteli vinanuka choo utasema vyoo vya stend. Bites za kiwango cha chiiini.

Safari ni starehe jmkuujkhk
Mkuu,ni kama umeniona Yaani hivi vibasi vya yutong vinazi gua Sana,mm kimo changu ni mrefu wa kiasi cha haja,huwa nalazimika kukata tiketi ya mbele ili nisiumie magoti.nateseka Sana,ni vizuri wakaanza kuleta Scania ama kampuni zingine.
 
[emoji16][emoji16][emoji16] Ogopa sana watu wenye mawazo ya kimaskini! Kila kitu kwao ni uchawi. Ukimiliki hela halafu ukawa na tabia za kutojipenda, au huna hobby ya kupenda kuvaa vizuri, kula vizuri, au una tabia za ubahili! Tayari wanakutangaza ni mchawi! Mara sijui masharti ya mganga nk.

Kumbe utajiri kwa sehemu kubwa uko benki, usimamizi mzuri wa biashara, nidhamu na matumizi mazuri ya fedha, umakini, nk. Bahati mbaya hawa matajiri huwa hawapendi kujianika kwa kila mtu. Ila kiukweli wengi wana mikopo mikubwa benki kwa kutumia dhamana za vitu visivyo hamishika kama nyumba, mashamba makubwa yenye hati, nk! na mikopo hiyo kwa kiasi kikubwa, ndiyo iliyo wafikisha hapo walipo.
Definitely
 
Mkuu,ni kama umeniona Yaani hivi vibasi vya yutong vinazi gua Sana,mm kimo changu ni mrefu wa kiasi cha haja,huwa nalazimika kukata tiketi ya mbele ili nisiumie magoti.nateseka Sana,ni vizuri wakaanza kuleta Scania ama kampuni zingine.
Kabisa. Hapo brand si hoja sana lakini mkuu. Hizohizo Yutong, mchina hashindwi kuweka ama kufanya haya tunayodai. Hili si eneo gumu katika utengenezaji magari. Ingekuwa tunadai engine,hapo ndipo tungeanza kufikiria brand.

Ni kwamba mabasi haya yanatengenezwa kichumi. Ndo maana utaona basi kali,linavutia lakini bei ni ya chini ukilinganisha na mengine sokoni. Ni makusudi tu kwa sababu za kibiashara.

Hata hivyo, hatusemi tuingilie mikakati yao,wajasiriamali na wazalishaji magari, wao wajaribu kukidhi haja za wateja wa makundi tofauti.
 
Back
Top Bottom