Tetesi: Usajili wa Mabasi ishirini mapya ya Abood

Tetesi: Usajili wa Mabasi ishirini mapya ya Abood

Hizo
Screenshot_20211013-212431.jpg
 
I
Islam hajawah kuwa mpinzani wa kweli wa abood....yan abood usimlinganishe kabisa na islam...wakat islam angalau ana basi kidogo za kueleweka, abood ndio alikuw na zile andare zikiwa mpya kabisa...na wakati huo abood alikuw anachuana sana na Hood wakati bado hajafa....islam alikuw pembeni kabisa huko....Hood akafa,Islam sijui akapotelea wapi, BM ndio akaibuka baadae ukaanza mchuano wa Abood na BM...labda kama umezaliwa juzi mkuu
Hivi mzee hood amefariki au nimeelewa vibaya?
 
Leo mji was Morogoro umemeremeta, Mabasi 20 yameingia kwa wakati mmoja, Samia kafungua uchumi, matajiri hawaogopi tena kufungua fursa kwa vijana kuajiriwa, hii ni baada ya Aboud Bus kushindwa kuingiza basi mpya tangu Magufuli awe Rais, kipindi cha Magufuli kampuni nyingi za mabasi zilifilisika.

Hongera Samia kwa kuanza kutujaza utajiri, wale wengine walitaka tuwe masikini na wanyonge
Abood ameingiza mabasi mara 2 ktk utawala wa magu kila awamu kamwaga basi 12 jumla 24 hiyo ni rekodi ambayo nimeiona kwa macho yangu sio kusimuliwa so muda mwingine usipende kumzunguko anko magu mabaya tuu ongea na mema aliyofanya
 
Mimi ninadhani hicho ni kiwango cha kawaida tu kwa kampuni kama Abood. Hata alipoingiza hizi zilizopo sasa ni hivyohivyo tu. Ninakumbuka ilikuwa sherehe pale Msamvu, misele ya kufa mtu roundabout wakipokewa na bodaboda.

Ninafikiri kwetu wateja, muhimu sasa ni kuletewa basi zilizo comfortable na rafiki kimatumizi. Yutong tunazoletewa ni za kikuda sana. Pot za kuchajia zinadumu miezi,hazifiki mwaka. AC halikadhalika—ikishabuma mtakoma humo kwenye basi. Siti pia ni ndogoo,ukiwa mrefu ama kibonge imekula kwako.

Ninajua haya ndo huchangia kushusha bei ya basi huko sokoni uchina. Lakini,kwakuwa kampuni ina uwezo, ingia dau kubwa, lete chache za ukweli wenye uwezo wapande kwa bei elekezi. Wateja wapo. Tunaona BM ana zile zenye daraja la kwanza na la pili. Kila siku daraja la kwanza zinajaa fasta.

Halafu Abood kama mnanisoma acheni ubahili. Katikati ya Dar na Moro jengeni kahoteli uchwara ka kupata bites na kujisaidia. Mnahama vihoteli, mnapeleka abiria vihoteli vinanuka choo utasema vyoo vya stend. Bites za kiwango cha chiiini.

Safari ni starehe jamani.
Kali kuliko vyote ni seat, visiti vimebanana hadi kero, ukiegemea hauwi comfortable
 
Humjui abood wewe,utakuwa umezaliwa juzi,kila nusu saa kuna gari inatoka msamvu kuja dar na dar kwenda moro,bado route za mikoa bado yanayokodishwa,reserve na yaliyo service
Kazi yenu kusifia wanaume wengine, tengeneza vyako ujisifie.
 
Katika wasafirishaji wa Abiria Dar/Moro ni Alsaed,Sadiq,Islam,Hood na Abood hawa ndio walikua na basi nyingi sana!!...Kwa sasa ndio BM ambae wakati huo alikua Route ya Turiani na New Force huyu naona basi zake mbovu ndio kazipa route hii fupi!!!
Nikaingia kwenye website ya abood, kumbe biashara imeanza 1941 na baba yao

Usafirishah abiria walianza 1986

Watu wapo kitambo kwenye game
 
Back
Top Bottom