Ushauri: JKT kwa Mujibu wa sheria ifutwe, badala yake vijana wapelekwe VETA miezi 3 au 6

Ushauri: JKT kwa Mujibu wa sheria ifutwe, badala yake vijana wapelekwe VETA miezi 3 au 6

Kule ujerumani, kabla ya kuingia chuo kikuu ni lazima kwanza ukapate elimu ya ufundi, hata kama unaenda kusomea sheria au udaktari, ni lazima uwe na elimu ya ufundi kwanza, iwe ufundi mekanika, umeme nk., vinginevyo hudahiliwi chuo kikuu.

Inabidi kutumika sasa huku kwetu
 
Mi wazo langu tofauti kwa kuwa vyuo vya VETA vichache na havina walimu wa kutosha,hukohuko kwenye makambi ya JKT ufundi ufundishwe kwa sana na makambi yapewe vifaa vya ufundi kama umeme,welding,uashi, rangi, upishi, udereva, mambo ya kwata yawe kiasi.
 
Suala muhimu ni kuboresha mfumo wa JKT na kuacha kuchanganya na siasa. Maana hata wakienda VETA siasa ikiingia tu basi Qwishney
Watanzania ni watu wa porojo porojo tu na si vitendo,yoote haya ni porojo TU!
 
Habari zenu wanajukwaa?

Ngoja nijikite kwenye lengo la uzi. Naishauri Serikali sasa wabadili mwelekeo katika kuelekea Serikali ya viwanda.

Vijana wanaomaliza kidato cha sita wapelekwe VETA kwa miezi 3 ili wakapate mafunzo ya awali (basic) ya ufundi mbalimbali.

Kwa kufanya hivi itasaidia kuwaandaa vijana wenye ujuzi mbalimbali mitaani. Kuna kozi nyingi tu ambazo kijana akizipata kwa miezi 3 anaweza kuamka na kujiajiri au hata kuajirika as general helper au fundi mwanafunzi.

Binafsi nimepitia JKT Mujibu wa sheria Ruvu na nilibahatika kupata ajira kupitia gamba la JKT ila wenzangu wengi wamemaliza digrii na hawana kazi mitaani.

Serikali inatumia kiasi kikubwa sana kumrecruit kijana mmoja wa jkt kwa miezi 3 au 6. Ile fedha ingetosha kumlipia ada VETA na akimaliza miezi 3 akapewa kamtaji.

Viongozi natumaini mtalitendea kazi suala hili.
Tambua lengo la JKT siyo kuinua viwanda, ni kuandaa waru watiifu kwa serikali
 
Habari zenu wanajukwaa?

Ngoja nijikite kwenye lengo la uzi. Naishauri Serikali sasa wabadili mwelekeo katika kuelekea Serikali ya viwanda.

Vijana wanaomaliza kidato cha sita wapelekwe VETA kwa miezi 3 ili wakapate mafunzo ya awali (basic) ya ufundi mbalimbali.

Kwa kufanya hivi itasaidia kuwaandaa vijana wenye ujuzi mbalimbali mitaani. Kuna kozi nyingi tu ambazo kijana akizipata kwa miezi 3 anaweza kuamka na kujiajiri au hata kuajirika as general helper au fundi mwanafunzi.

Binafsi nimepitia JKT Mujibu wa sheria Ruvu na nilibahatika kupata ajira kupitia gamba la JKT ila wenzangu wengi wamemaliza digrii na hawana kazi mitaani.

Serikali inatumia kiasi kikubwa sana kumrecruit kijana mmoja wa jkt kwa miezi 3 au 6. Ile fedha ni na JKT b
Viongozi natumaini mtalitendea kazi suala hili.
Kuna tatizo kubwa sana la uelewa kwa wengi wa vijana wetu kuelewa VETA vijana wanakwenda kusomea nini na bdae kulisaidia taifa na JKT wanakwenda jifunza nini na bdae wakalisaidie taifa kuwa na vijana wamoja,wazalendo na wanao pendana! Nimuombe mleta hoja atofautishe JKT na VETA na taasisi nyingine. Hizi ni taasisi zinazo pokea vijana tofauti sana na malengo tofauti!
 
Tulioenda veta miaka hiyo tulionekana tumefeli maisha sasa mambo yamekuwa mambo kila MTU anaona veta ni mkombozi.asante veta-chang'ombe kwa kunitunuku gamba langu LA electrical installation sasa napatapata vijihela
 
Niwazo zuri lakini ufundi Ni utashi wa mtu
Mambo yakibana utashi huwaga unakuja tu. Vijana sasa hivi wengi wana penda kilimo ila kama ungewauliza wakati wapo Secondary au vyuoni wange kwambia kilimo siyo utashi wao.

"Ubishoo huwaga unaenda uki isha kadri umri na majukumu yanavyo ongezeka"
 
Kule ujerumani, kabla ya kuingia chuo kikuu ni lazima kwanza ukapate elimu ya ufundi, hata kama unaenda kusomea sheria au udaktari, ni lazima uwe na elimu ya ufundi kwanza, iwe ufundi mekanika, umeme nk., vinginevyo hudahiliwi chuo kikuu.
Nilikuwa sijaipata hiyo, so my thought gone far away. Mpaka wazungu hufanya hivi!!!
 
JKT kwa mujibu ifutwe kabisa au taasisi zote za serikali ziwe chini ya Jeshi, ni ngumu sana askari nusu kuongozwa na raia, ni bora wahitimu wa kidato cha nne na sita wapitie VETA kwa mujibu na huko wapewe mafunzo kidogo ya ukakamavu.
 
Back
Top Bottom