Ushauri: JKT kwa Mujibu wa sheria ifutwe, badala yake vijana wapelekwe VETA miezi 3 au 6

Ushauri: JKT kwa Mujibu wa sheria ifutwe, badala yake vijana wapelekwe VETA miezi 3 au 6

Waliorudisha huu utaratibu wa JKT kwa mujibu wa sheria hawakukurupuka.
Jeshi lina nafasi kubwa katika ustawi wa nchi.
Kule tunasema vijana wanajifunza uzalendo, hiyo ni lugha rahisi tu ya kutuaminisha wananchi, lakini JKT ina umuhimu mkubwa zaidi ya huo uzalendo.
Kuna mambo yanaendelea kwa wachache baada ya ile miezi mitatu kuisha.
Kupitia JKT kuna mambo makubwa yanafanyika kimya kimya ambayo matokea yake yatakuja kuonekana baadaye sana.
Nchi kubwa kama Korea, US na China wanautaratibu unaofanana na huu.

Hesabu inayofanyika kule ni: ELIMU+ JESHI+JAMII= ( ).


Elimu ya ufundi nayo ni muhimu sana, ingependeza kila mzazi awe anapeleka kijana wake kusoma ufundi mfano anapomaliza form 4 maana pale ndio kuna muda mrefu mtoto anakaa nyumbani.
 
Kila mahala JKT na VETA kuna malengo/makusudi yake mpaka serikali ikaamua kuziweka taasisi hizi Mbili tofauti...
wazo lako ni zuri sana ila kubalance ulitakiwa kushauri kwamba kuwepo na chagua wanaotaka kwenda veta na wanaotaka kuniunga na jkt yaani liwe chagua la muhitimi wa form six.
 
Nakubaliana nawe mkuu. maana binadamu lazima azifuate nyakati na siyo nyakati zimfuate binadamu. zama za ukakamavu zimekwisha kwa sasa katika bara letu la afrika na hivyo zama zinazoitajika na mapinduzi ya kitaalamu. kama vijana wote watakwenda veda hata kwa miezi 6 basi tanzania itakuwa na family industry( viwanda vya kifamilia) nyingi sana. kama china walivofanya mapinduzi.
 
Kila mahala JKT na VETA kuna malengo/makusudi yake mpaka serikali ikaamua kuziweka taasisi hizi Mbili tofauti...
wazo lako ni zuri sana ila kubalance ulitakiwa kushauri kwamba kuwepo na chagua wanaotaka kwenda veta na wanaotaka kuniunga na jkt yaani liwe chagua la muhitimi wa form six.
ok. lakini jkt bado ina watu wa kujitolea. hivyo ni heri washeria wakawekwa veta.
 
Mawazo yangu:-

JKT bado ni muhimu, vijana wajifunze UTII, UVUMILIVU, UKAKAMAVU, Mbinu za medani kiasi kisha watumikie kujenga Taifa kwa cheo cha 'Service Man / Woman' kwa muda huo wa miezi mitatu au sita kwenye hizo fani za VETA. (Labour Camps)

Tuna kizazi legelege sana wasiojuwa hata uzalendo.

Niishie hapa kwanza.
Me niliyepitia huko, nilijifunza Utoro, Matusi n.k..
 
Wewe umenena sana, kwa maana ile likizo ya kidato cha 4 ni ndefu sanaaa.. Vijana huwa wanishiaga kupeana mimba tuu.. bora huo muda ungekuwa wa kwenda VETA kwa ajili ya basic technical skills
JKT Bado inaumuhimu wake Mkuu bora ingekuwa ukimaliza form four unaenda veta kupata technical skills haijalishi ulisoma mchepuo gani yaani hii iwe ni (Basics).

Alafu form six waende JKT sasa.

Then chuo kikuu ukimaliza nenda katumie ujuzi uliuopata kujiajiri au kuajiriwa.

Nawasilisha
 
JKT Bado inaumuhimu wake Mkuu bora ingekuwa ukimaliza form four unaenda veta kupata technical skills haijalishi ulisoma mchepuo gani yaani hii iwe ni (Basics).

Alafu form six waende JKT sasa.

Then chuo kikuu ukimaliza nenda katumie ujuzi uliuopata kujiajiri au kuajiriwa.

Nawasilisha
Hili wazo litumike kipindi vijana wameshamaliza shule na wanasubiri matokeo yao, wazo litanoga sana.
 
Mdau katoa mada nzuri,Ila sasa mimi ningeshauri hili swala lingeenda kwa form 4 kwani wapo wengi mtaani alafu bado ni vijana wadogo ambao wanamaliza wakiwa wengi wao hawana mwelekeo na kwa wachache wao hawana msaada wa kujiendeleza kwenye shule za private ,Lakini pia hakuna mtu ambaye hajui wingi wa vijana hawa kwenye jamii tunayoishi.
Kwa serikali kutekeleza haya lazima izingatie yafuatayo
1. Sera ya nchi.sera nchi yetu ni Tanzania ya viwanda.lazima uzalishe vijana watakaosadia kufikia lengo hilo,na ifahamike kuwa hata nchi zilizoendelea kama china wanatumia vijana wa kila aina alimradi mtu kabobea kutengeneza kitu fulani bila kujali elimu aliyonayo.
2.Gharama ni kubwa ila serikali ikiamua itafanya kwani mapato ya nchi yetu ni makubwa.
3.kwa kidato cha sita kwenda jkt waendelee kwenda ila waboreshe mafunzo yanayotolewa kule yawe yanafaida /ifanane na sera ya nchi.
Kwa kufanya haya utakuwa umetengeneza ajira kwa vijana wengi baada ya muda mfupi alafu alafu lengo la serikali itakuwa imefanikiwa.
 
Ni wazo zuri ulilowaza lakini utekelezaji wake ni kazi kubwa Sana na mzigo mkubwa. Kuwafundisha wanafunzi JKT costs less than kuwafundisha wanafunzi VETA.

Miundombinu ya Jkt ni michache na haihitaji gharama kubwa ukilinganisha na Veta,

Jambo jingine ni kwamba wakati vijana wako Jkt wanashiriki katika kilimo hivyo Chakula kinachotumika kinapatikana kupitia wao wenyewe unlikely Kama wangekuwa Veta ambapo watakuwa wanakula wasichozalisha. Hii itaongeza gharama ya mafunzo.

Zaidi ni kwamba vyuo vingi vya Veta havina miundombinu ya kutosha kuwahost walengwa Kama ilivyo kwa Jkt ambapo unaweza shuhudia wanafunzi hata zaidi ya 1000 kwenye kambi moja.
 
sema tatizo muda ..utamfundisha kwa muda upi utakaotosha ku master skill hyo utakayompa kabla ya kuendelea na masomo?
 
Naunga mkono hoja, ila VETA itabidi waunde crash programme maalum kwa wanafunzi wa muda mfupi ambao hawatapata academic certicates ila watapata vyeti vya utambulisho wa kushiriki kambi maalum ya mafunzo.
 
Mi huwa najiulizaga, hivi wana JF wote tungekuwa tunatoa hoja zenye mashiko na zenye kulenga kuboresha maisha hii nchi si tungekuwa mbali sana, nichukue nafasi hii kumpongeza mtoa mada, maana thread kama hizi ni ngumu kuzipata humu, zimejaa thread za ujinga ujinga tu..
 
Chief umetoa kitu ambacho serikali inaweza kukiangalia upya. Faida vijana watakuwa na ujuzi mbali mbali ambao wengine wanaweza anza tumia kama mtaji chuoni.
Kule ujerumani, kabla ya kuingia chuo kikuu ni lazima kwanza ukapate elimu ya ufundi, hata kama unaenda kusomea sheria au udaktari, ni lazima uwe na elimu ya ufundi kwanza, iwe ufundi mekanika, umeme nk., vinginevyo hudahiliwi chuo kikuu.
 
Back
Top Bottom