Huu ni Ushauri wa Bure kwa Rais Samia kwenye mabadiliko tarajiwa ya cabinet kufuatia Ripoti ya CAG, namshauri Rais Samia, asibabaike sana na kuangalia ma vyeti ya usomi kwenye uteuzi wa cabinet yake, atumie watu wenye uzoefu, mfano Waziri wa Fedha wa sasa Dr. Mwigulu Mnchemba ni msomi mzuri wa uchumi, ana 1st Class ya degree ya uchumi kutoka UDSM, lakini sio mtu wa ki fedha fedha!. Hajawahi kushika na B na ma B na ma B mikononi mwake kama Dr. Charles Kimei alipokuwa CRDB, hivyo Wizara ya Fedha akimpa Dr. Kimei, fedha zitakuwa zimefika kwenyewe.
Kwenye biashara na uwekezaji, kuna wasomi wawili, madaktari wa PH.D, je, wanewahi kufanya chochote hata kuuza nyanya tu? Kwenye Biashara Uwekezaji ampe Deo Mwanyika, kina Sumri, kina Shabiby, Abood etc, watu wenye uzoefu wa kufanya biashara.
Aunde Baraza dogo lenye mawaziri wenye uzoefu, ukiwa na mtu mwenye uzoefu, hawezi kupigwa kirahisi kama msomi mwenye vyeti lakini hajawahi kuuza hata toothpicks!
Ni ushauri tu.
Paskali
Umemtaja pia Deo Mwanyika.
Ni mtu muungwana sana.
Na Barrick Gold walimuamini sana wakamteua kuwa Vice President wa Afrika anayeshughulikia Mahusiano na Serikali.
Tatizo langu siyo Deo Mwanyika.
Tatizo langu ni Sekta ya Madini.
Kwa nini Tanzania tunakosa au tunapungukiwa USD/Euro wakati Tani za Dhahabu zinasafirishwa kwenda nje ya Nchi kila mwaka?
Sote tunajua kuwa Nchi yenye 'Gold Reserve' haipati shida ya FOREX!
Dhahabu zinazochimbwa na hawa Wachimbaji Wakubwa, ie Geita Gold Mine, Barrick Gold, etc etc, zinasafirishwa kama mzigo wa nguo za mtu binafsi mpaka huko Canada, UK na kadhalika.
Baada ya kufika huko, ndipo zinauzwa.
Kwa hiyo, wanaopata FOREX ni hizo Nchi zinazouza Dhahabu iliyochimbwa Tanzania.
Tunachopata Tanzania ni MRABAHA tu.
Katika mazingira haya, Mhe. Deo Mwanyika ambaye ameitumikia Barrick Gold, haleti matumaini ya kukuza UWEKEZAJI Tanzania.
Barrick Gold, na Migodi yote mikubwa Tanzania siyo Wawekezaji.
Ni WAVUNAJI.
Wanakuja na 'Combine Harvesters' kuvuna Ngano ambayo hawakushiriki kuipanda.
Ningekuwa na uwezo, UAMUZI wangu ungekuwa MADINI YOTE YACHIMBWE NA WAZAWA PEKEE.
Dhahabu zote zingekuwa zinauziwa Tanzania na Benki Kuu ya Tanzania ingekuwa imejaa Dola za Kimarekani na Euro za Ulaya na Fedha za Mataifa mengi ya Nje.