La pili : Soko nimepata nasikia Kibaha kwa wachina ukipeleka ni fasta tu na malipo ni siku 3 mpk 5 je ni kweli na je kuna changamoto yoyote?
Sawa kiongoz nshapata muhusika wa pale na very soon naenda kuwacheki nijue utaratbuKwangu ni hayo tu.
- Biashara haifanyiki kwa kusikia
- Bali biashara hufanyika kwa utafiti usio na shaka kuhusu soko husika.
- Kama kweli unania, Hakikisha umefika hapo kibaha, kwa utafiti wa kina na uliokamilika kwa kuona ahaswaa na wahusika na kufanya nao mazungumzo.
- Hata kama itakughjarimu fedha na muda kufika manufaa utakayopata ni makubwa.
Ushauri wa maana sana huuMm sikushauri uchukue mkopo kwa ajili ya kuanza biashara ambayo hauna uelewa nao vizuri.Asante
Hio kazi mimi ndo naifanya , nimeongea kwa uzoefu niliokuwa nao kuhusu hio biashara.Umeongea mengi ila hapo hakuna litakalofanya afanikiwe kwenye hio biashara.
Atafute wafanyabiashara wa hio kazi akae nao awafanyie kazi hata miezi miwili, atakuwa ashaelewa kila kitu
VP umeshapata abc ktk hili au bdos
Sawa kiongoz niko tayar kufanya hivyo labd n dodoma sehem gani
hapana bado sjapew nimeamua kuchkulua singidaVP umeshapata abc ktk hili au bdo
Kwanini uliacha.Mimi ndiye Alwatan wa hii biashara, mwakani naingia tena baada ya kuiacha kwa muda nikiwa full equipped.
No reform, no business.Kwanini uliacha.
Yaan unamwaga 30 mil kwa utafiti wa kusikia. Kifupi hakuna information yoyote uliyo nayo kuhusu hiyo biashara.kusema umepata saoko kwa kusikia maongezi ya vijiweni utalia baadae. Chukua hiyo hela nenda kaweke utt wakati unajifikiriaHabar mimi naishi Dar nataka niombe mkopo wa million 30 kwajili ya biashara ya mahindi, nikachkue vijijini tani 32 nilete Dar kuuza kwani kwenye tani nyingi ndo faida ilipo. Mnashaurije wadau? Hilo la kwanza.
La pili : Soko nimepata nasikia Kibaha kwa wachina ukipeleka ni fasta tu na malipo ni siku 3 mpk 5 je ni kweli na je kuna changamoto yoyote?
La Tatu: Ninachoogopa mimi ni upande wa Quality nasikia kuna quality inayohitajika kwa mahindi ya zamani na mapya kuhusu unyevunyevu au moisture, sasa nitajuaje hiyo quality nasikia kuna kile kifaa je nitaweza kupima tani 32 kwa haraka haraka na kule kwenye soko je wanakata bei wakiona quality yako ndogo?
KAMA KUNA MTU ANAYEHUSIKA ANAYEFAHAMU ZAIDI JUU YA HILI ANICHEKI MSAADA WAKO MUHIMU
Fafanua mkuuNo reform, no business.
Km umeshafanya uamuzi sio mbaya ila Kuna jamaa yangu yupo kibaigwa naweza kukuunganisha nae ili uangalie unafuuhapana bado sjapew nimeamua kuchkulua singida
Kama huyo Jamaa (anayetaka kuchukua mkopo wa 30m) Kabila lake ni Mkinga aendelee na mchakato wa kukopa na kwenda kuchukua mzigo Sumbawanga then kuupeleka kwa Wachina. Vinginevyo aache.Bwashee, watu wanachukua mkopo kuendeleza biashara! Wewe unataka kurisk pesa yote hiyo halafu bado huna abc za hiyo biashara? Nakushauri komaa upate hela walau ya tani 3-6 kwanza anza mdogo mdogo , ukiona mwanga ndo uwaze kukopa sasa !
Anza na milioni 5 ya mfukoni kutest kitambo, usije kuwa mkimbizi uzeeni wa madeni kama jamaa zanguHabar mimi naishi Dar nataka niombe mkopo wa million 30 kwajili ya biashara ya mahindi, nikachkue vijijini tani 32 nilete Dar kuuza kwani kwenye tani nyingi ndo faida ilipo. Mnashaurije wadau? Hilo la kwanza.
La pili : Soko nimepata nasikia Kibaha kwa wachina ukipeleka ni fasta tu na malipo ni siku 3 mpk 5 je ni kweli na je kuna changamoto yoyote?
La Tatu: Ninachoogopa mimi ni upande wa Quality nasikia kuna quality inayohitajika kwa mahindi ya zamani na mapya kuhusu unyevunyevu au moisture, sasa nitajuaje hiyo quality nasikia kuna kile kifaa je nitaweza kupima tani 32 kwa haraka haraka na kule kwenye soko je wanakata bei wakiona quality yako ndogo?
KAMA KUNA MTU ANAYEHUSIKA ANAYEFAHAMU ZAIDI JUU YA HILI ANICHEKI MSAADA WAKO MUHIMU
Pata muda ujue msimu mzuri wa ununuzi wa mahind iwe shambani zaidi kwakujikita kuandaa vituo vya ukusanyaji kwa bei ya ulanguzi,, ukipata uhakika hakikisha unaweka mashalt yako kwamba unahitaji mahindi yenye ubora upi? Kwa bei yako ya kibiashara, ukumbuke kwamba ukitangaza donge nono kwa mkulima utapata mahindi safiii yaliyo safishwa kabisaaaa, pia hutakiwi kukurupuka, mara nyingi msimu wa mavuno wakulima wanakuwa na uhitaji wa pesa ya haraka huo ndio muda wako, jitahid kucheza na gape, walanguzi wakisha zidi kwa lengo la kupandisha bei kwa wakulima usipani hapo inatakiwa utulie na mzigo wa kwanza yaaan kuwa mpole kusoma mchezo, walanguzi wakubwa wakisha pita wakulima watashusha tena! Mzigo wako unapokuwa umehifadhi gharani ingia sokoni ukiwa na options 2." option ya 1 ingia kwa Hao wachina kibaha nadhani wapo mail moja maeneo ya loliondo ulizia bei zao, na ujue ubora wa mahind wanayo hitaji pia zipo company nyingi za kusagisha Unga cheza nao.
Option 2 kodi mashine, andaa logo yako upate mifuko kg tofauti, nunua mashine ya kufungua mifuko sajil campun kisela sagisha Unga sambaza. Watu wanakula kila siku mzee wangu pambana idea ni nzuri Sana hutakiwi kuogopa muhim jipange na uwe mjanja
shukran brother nimekuelewa.... nitavi note nifanyie kazi , Swez kurudi nyuma ila ntazingatia ushaur na kwa wachina nshaenda pale na nimepewa utaratbu wote na wiki hii naeza kwenda sumbawangaKwan uzoefu wangu zingatia mambo yafuatayo :
- Hakikisha unaenda kwanza kwa hao wachina iliupate utaratibu wao na vigezo wanavyotaka.
- Moisture content
Ndo Kila kitu ila kwa mahindi mengi ya sasa ni ngumu kupata ambayo moisture content ipo chini ya 14 , hivyo unaweza ukatafuta location ambazo mvua za masika zinawahi kukata au au ukakusanya hivyo hivyo faida inaweza kuwa ndogo ila ukawa na mzunguko.
- Usafiri
Zingatia unapotoa mahindi kama utakuwa unayatoa ndani sana na ujaweka logistics zako vizuri unaweza kupata hasara au faida kupungua. ( Wastani wa kisafirisha 1 Tani moja kutoka Sumbawaga, Mbozi, Mbeya inacheza 80k - 100k mzigo ukiwa karibu na barabara kuu)
- Upimaji
Viwanda na wachina wananunua kwa kilo na sio kwa debe , hivyo lazma uzingatia wastani wakilo unazopata kwa kila gunia , kuwa makini na Upimaji mashambani ikibidi uwepo site kabisa iliusipate hasara na upate mahindi yenye ubora.
- Ufungaji wa mzigo
Hakikisha mahindi unayonunua funga kwenye mifuko imara na ujazo unaoendana iliusipate shida kwenye ukaguzi wa mzigo kiwandani .
- Ulipaji wa pesa wakati wa kukusanya mzigo.
Hapa ndo wengi huwa wanapigwa . Usikubali kuwapa madalali au kuamini watu kukusanyia , malipo yote fanya mwenyew baada ya kukagua mzigo unaoletewa. Pia usitembee na cash nyingi utalia..
Kwan sasa hivyo vitakusaidia....
Ushauri wangu hii biashara inafaida sana kama ukijua jinsi ya kuifanya . Pia kupata hasara ni jambo la dakika mbili , kwa wastani faida kwa Tani 32 ukifanikiwa kufikisha na ukitoka gharama zote faida inacheza 2m hadi 3m kutegemea na demand na ubora wa mahindi .
Hivyo kwasababu ww n mgeni kwenye soko anza na kusafirisha tani 10 kwanza , then utaongeza unavyozidi kupata uzoefu...
Wasikukatishe tamaa hii biashara inapesa sana , kama unania nayo itakutoa kimaisha .