USHAURI: Rais Samia suluhisho pekee kwa Bandari Tanzania ni hili

Kwa haraka sana, Ijengwe Bandari ya Bagamoyo ambayo iwe na Gati zisizopungua 40. Bandari hii iendeshwe na Private sector with exception kwenye masuala ya Ulinzi, Usalama na Kodi
Hapa ndipo panapolengwa, mnaanzia mbaaaali ili mradi tu mfikie hapa.

Haridhishwi na kitu gani? Amesema madhaifu yoyote?
 
Bandari bila reli ni kazi bure, kazi bure bureshi
 
Maendeleo ni process! Roma haikujengwa kwa siku moja! Kikubwa ni kufanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi
Na watanzania tulivyo……tunashabikia viongozi dhaifu tulionao na hata kufikia kutetea kasi ndogo ya maendeleo yetu!
 
Serikali yenyewe imeitelekeza bandari ya Dar huyo DG ataweza nini? Mkataba wa TICS ni kandamizi na TICS hawaperform na hawajawahi kuperform. Bandari haina miundombinu itakuwaje efficient? Yaani hata hivi vidaraja hicho cha Tazara na hicho kingine kinachojengwa cha Uhasibu vyote vimeigonore route ya Bandari ambayo ilipaswa kuwa kipaumbele. Yaani mzigo wa bandari unaweza kutumia masaa ma3 kutoka bandari mpk Ubungo ambapo ni chini km 15 halafu tunatafuta efficiency toka kwa DG kweli huku si kumuonea tuuuu? Dry port ya Kwala imekwama zaidi ya miaka 7, are we really serious au ndiyo tunapiga siasa kama kawaida yetu?
 
Kuna watu wananufaika na hiyo Bandari na ndio wanasabisha yote hayo yasifanyike,Hii nchi kuna watu wanahujumu miradi kwa sababu ya matumbo yao binafsi....Nasikia kuna watu wakisikia mradi wa Reli unafanikiwa matumbo yanawauma!!! Ubinafsi umewajaaa...
 
Barabara ya Mandela Road haifai! kuna muda ukifika kule Bandarini unaweza kuacha gari ukaamua kuchukua pikipiki! Maroli yanaziba njia na kuweka foleni ya hatari sana!

Bila kujenga Bandari ya Bagamoyo na kurekebisha miundombinu hatuwezi ona ufanisi kwenye sekta ya Bandari kamwe
 
Kuna watu wananufaika na hiyo Bandari na ndio wanasabisha yote hayo yasifanyike,Hii nchi kuna watu wanahujumu miradi kwa sababu ya matumbo yao binafsi....Nasikia kuna watu wakisikia mradi wa Reli unafanikiwa matumbo yanawauma!!! Ubinafsi umewajaaa...
Dawa ni kuwapa private sector wajenge hizo reli na hiyo miundombinu as long as watakuwa wametoa hela zao na kukopa lazima watataka zijiendeshe kwa faida! Obvious hutaona kukwama au kuchelewa kwa mizigo na mifumo bandarini. Serikali tukusanye kodi na kusimamia ulinzi na usalama tu! Uendeshaji wafanye private sector
 
TICS kuna malalamiko sana juu ya mkataba wao! it's high time huo mkataba uwe renegotiated au otherwise watolewe Alltwen muwekezaji mwingine mwenye uwezo
 
Bandarini kumeoza kweli kweli. Mwezi uliopita nilikuwa nimetokea zangu huku Dk Mwinyi na kuna machine flani flani used nilikuwa nimenunua. Hivo nikalazimika kusafiri na meli ya mizigo ili nikifika nitoea kabisa mzigo wangu. Baada ya meli kufunga gati nilikaa kwa muda wa masaa matatu nikisubiri mtu wa kuja kukadiria CBM ya mzigo wangu. Baada ya makadirio nilipewa control number ya kwenda kulipia, ili kuokoa muda nikamtafuta potter mmoja nikamkabidhi kazi ya kwenda kulipia na mimi nikatoka nje kutafuta gari. Baada ya kurudi na gari na tayari potter ameshalipia wafage na sms ninayo kwenye simu yangu, walinzi wakagoma kuruhusu gari kupita getini. Nikamwuliza dereva shida ni nini akasema wanataka tuwape elfu 20 ili waruhusu gari. Nikamwita yule mlinzi nikamwuliza tatizo ni nini akabaki anajiuma jiuma tu, nikamwambia nina haraka nimetoka kazini Zanzibar natakiwe nifikishe huu mzigo nyumbani na nirudi zanzibar, akaanza kuniuliza wewe unafanya kazi gani nikamwambia siyo juumu lako. Na kama unataka nikupe hiyo elfu 20 nipe control number na nikamwambia dereva usiondoe gari hapa acha tuweke foleni.

Kinyonge saana akaruhusu gari kwende mbele tena kuna geti lingine kwenye kona kushoto nako wanataka hela ili gari kupita nikawambia wasubiri nirudi, kifupi kila mahali na kila mtu anataka hela. Huo ni mzigo tu mdogo ambao umetokea ZNZ vipi mizigo mikubwa? Bandarini kuna laana hata huyu aliyechukuwa nafasi naye atafurushwa tu kwa sababu Tanzania tunaanza kufundisha rushwa vijana wetu wakiwa wadogo. Kwa nini utakuta kijana anafuatilia cheti cha kuzaliwa anakwenda ofisi ya serikali anaambiwa kama unataka cheti ndani ya wiki moja toa elfu 50, ila kama hauna haraka lipia hiyo serikali ambayo nadhani ni elfu 10, unajiuliza mtu huyu huyu anauwezo wa kufanya hiyo kazi kwa siku chache lakini anataka rushwa kwanza.

Niseme tu kuwa hakuwezi kuwa na efficiency bandarini kwa sababu kinachofanyika ni miradi ya watu kupiga hela
 
Bandari imeshatushinda kuiendesha, bado tuna akili za kitoto kwenye uendeshaji wa biashara na usimamizi, we are not matured enough to run these show.

Watu wetu wengi kwenye management and control ni zero na sio wakutegemea kabisa.
Tuna jamii ya watu wavivu, wezi, walevi, wazinzi na wasiojali chochote.
Hayo yote yameletwa na malezi mabaya kuanzia ngazi za familia, mfumo mbaya na mbovu wa elimu, jamii kuishi kwa kudekezana, Serikali kudekeza watu wake nk.

NINI KIFANYIKE PALE BANDARINI? naelezea chini kwa kirefu.
 
NINI KIFANYIKE?

Kwasasa serikali ipige hesabu zake, kiasi gani cha fedha bandari kila mwezi inaingiza kwenye Hazinia yetu, kuanzia Kodi na mapato mengine. Tukishapata figure kamili ya kiasi cha fedha kwa mwezi kama mapato yetu, twende stage ya pili.

Tutafute muwekezaji mwenye jina kubwa kwenye operations za bandari kama MSC au MAERSKY nk, tubinafsishe bandari na operations zake kwa makubaliano ya yeye kutulipa kiasi kile cha fedha kulingana na hesabu zetu.
Tumpe kwa kuanzia miaka 10 afanye kuanzia management na operation kwa hiyo miaka 10.

Muwekezaji apewe mamlaka ya kuajiri kwa kuleta watu wenye uwezo kwenye utawala na uendeshaji.
Watanzania wabaki waajiriwa kwa muwekezaji na serikali iachane kabisa kudeal na uendeshaji wa bandari.
Serikali iwe na joint forces na muwekezaji kwa ajiri ya kumonitor mapato na malipo kwa serikali, kwenye joint force kuwe na watu wetu wa system wenye akili timamu wajaribu kuona in 10yrs muwekezaji anaingiza kiasi gani.
Serikali iwe haina mwajiriwa hata mmoja bali waajiriwa wote wawawe wameajiriwa na mwekezaji na mamlaka ya kuhire,kufire na kulipa mishahara ibaki chini yake muwekezaji.
 
Jambo muhimu ambalo linaweza kuwa na msaada maeneo mengine.

Serikali iache kutoa ajira za kudumu kwa wafanyakazi wake, Serikali ianze kupima waajiriwa wake kulinagana na utendaji kazi wao, Serikali ianze utaratibu kwa kuongeza mishahara na kupandisha vyeo kutokana na utendaji wa mhusika. Serikali isisite kufukuza kazi watendaji wazembe kila uzembe unapotokea.
 
WAZO ZURI SANA SIJAJUA KUNA WATU WANA AKIKLI HIVI. TATIZO NCHI HII VIONGOZI WAMEKARIRI KILA KITU DAR ES SALAAM KANDA ZINGINE ZITAENDELEAJE KWA MTINDO HUU. HALAFU NJIA YA USAFIRISHAJI ILIEILE. WABORESHE BARABARA KWA MFANO KWA MIZIGO KUTOKEA TANGA WAJENGE BARABARA YA LAMI KUTOKEA KARATU-MEATU-MASWA MIZIGO YOTE YA KANDA YA ZIWA ITAPITIA KULE PAMOJA NA YA NCHI JIRANI ZA RWANDA, UGANDA. JAMANI KWANINI KILA KITU DAR? NDIO MAANA WATU WAMEJAZANA HUKO KWASABABU MAENEO MENGIE MMEWANYIMA FURSA WANAKIMBILIA DAR. MUNGU AWAFUNGUE AKILI VIONGOZI WETU.
 
Umetoa madini sana ndugu yangu. Asante sana

Uendeshaji wote apewe muwekezaji ambae awe na mamlaka ya kuhire and fire. Kwa mfumo wetu wa malezi unaowafanya watu waishi kuwaza kupiga na kupata utajiri wa fasta kamwe hatuwezi kupata ufanisi kwenye Bandari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…