Suala la kwenda CAS si la lazima ni la kimaamuzi la yeye na wanasheria wake, iwapo wanaamini kuwa hakuna umuhimu wa kwenda hawatokwenda.
Hayo masuala ya mshahara ni masuala ya mkataba. Tatizo ni kuwa hapa nchini Club wakitaka kuachana na mchezaji wanamlipa na wanamuacha, mchezaji hawezi kulazimisha kubaki kambini, labda aseme amelipwa pungufu atafungua madai akiwa nje ya kambi na madai yatakuwa wazi na akishinda analipwa.
Upande wa pili wa shilingi sasa.
Yanga imwambie Fei ili kuondoka bila timu kutaka kukununua fanya moja, mbili, tatu ashindwe mwenyewe. Mpira ni burudani, sio biashara ya utumwa. Mchezaji anataka kuondoka mwenyewe aambiwe afanye nn aondoke. Aambiwe wazi wazi tulipe kiasi kadhaa uondoke.