We dada unaonekana ni moto wa kuotea mbali! Ni mbabe, mkaidi, na kiburi! Unayoyaandika ndio yanavyoakisi mtazamo hayo...haya ndio haswaa yana m'put-off' mwanaume yeyote anayejitambua!
Mtu ukikosea 'logically' unatakiwa kuwa na 'remorse'
Unatarajiwa kujutia hilo kosa na kuelewa madhira apitiayo uliyemkosea! Kujutia huko huenda sambamba ya unyenyekevu, na pia uvumilivu kwa 'reaction' anayoweza kuchukua mtendwa! Lakini majibu yako hayaakisi hayo yote!
Ndio maana reactions za wachangiaji zimekuita majina yote mabaya! Jitafakari, chukua hatua! Kama ni nguvu za giza nenda kaombewe!
Naomba kama nimekukwaza unisamehe! Hivyo tu!
Wanaume wa jf huwa wanatabia ya ku bully wanawake
Yani ilitakiwa jana nimkalie kimya ndio nionekane sina kiburi na tabia njema[emoji28][emoji28]
Kama umefatilia huyo alikuwa anani attack kwasababu ya post niliomba ushauri mwaka jana,Hebu nikuulize wewe uliekeleketwa na tabia yangu unataka kuniambia jf ni wanaume tu wanaruhusiwa kuomba ushauri,yani niogope kuomba ushauri au kuchangia kuogopa tu nitashambuliwa kwa maisha yangu ya nyuma??
Nipo jf kwa muda mrefu sana kuliko hii ID humu nimekutana na watu wengi wakubwa kwa wadogo na tuna heshimiana sana,nimekutana na vichaa ambao wanapenda kupandia watu vichwa kama hao wachache kwenye huu uzi
Huwa sina muda wa kujibu jibu watu hovyo jana nilitaka kwenda sambamba na watu wanaodhani kila mwanamke ni wa kumuonea,mimi hunionei kirahisi na Kama hicho ni kiburi basi naomba kikolee zaidi na zaidi
Naweza kuwa submissive kwa mume wangu tu,wengine nyie nina nafasi ya kuwaheshimu tu sasa msifikiri kama mnapambana na wake zenu huko majumbani basi hadi huku jf mtawapandia vichwa kila mwanamke
Hayo majina mbaya sijajua yamenipunguzia nini,labda uniambie wewe kuna lipi nitalikosa kwa majina walioniita
Nirudi kwako wewe ulieingilia usiyo yajua na kutoa ushauri juu,sijajua unajipa nafasi gani kwenye maisha yangu na unajiamini nini
Sidhani kama nimewahi kukupangia maisha humu ndani,au Kuna ninacho kutegemea hebu kiseme hapa ueleweke
Mwisho ushauri peleka kwa ndugu zako naamini lazima kuna watu wako wa karibu wanahitaji sana uwaongoze usijikute mshauri wa mitandaoni kushauri usio wajua
Huwa sikwazwi kwa vitu vidogo vidogo vya mitandaoni haswa cyber bullying
Nakwazwa na watu wa karibu zaidi kuliko nisio wajua so bila samahani
Haya siku njema