Dada Maya, sijui kwa nini una hasira na uchungu hivyo!
Mleta maada alitaka kutoa ushauri kwa mambo 'sensitive' sana kwa wanandoa wa kiume...hasa akigusia jambo gumu kumeza kuliko yote yanayoweza tokea kwenye ndoa na namna ya kukabiriana nalo! Majibu ulioyatoa ndio yaliyoshtua wengi! Wewe ndio umeonyesha huo ubabe dhidi ya huyo uliyemtendea kana kwamba alikutuma ufanye hivyo na kwa ukaidi na bila haya unaahidi kumtesa zaidi kama hatakusamehe na kusahau kwa muda wako uliojiwekea! Wakati huohuo unajigamba unamuheshimu mumeo huyohuyo unayemvunjia heshima na kuahidi kumkomesha zaidi asipokusamehe kwa wakati...huu ni utani! Heshima ni heshima tu kama humuheshimu mtu mwingine hata uliyenaye ndani...huyo mumeo kama kweli umeolewa huwezi muheshimu!
Humu mitandaoni kuna wengi wanapita na wengine hutumia maoni ya watu kutekeleza wanayotekeleza...hivyo tunapaswa kuwa waangalifu kwa tunayoyaandika ili yawajenge wengine!
"Kama umefatilia huyo alikuwa anani attack kwasababu ya post niliomba ushauri mwaka jana,Hebu nikuulize wewe uliekeleketwa na tabia yangu unataka kuniambia jf ni wanaume tu wanaruhusiwa kuomba ushauri,yani niogope kuomba ushauri au kuchangia kuogopa tu nitashambuliwa kwa maisha yangu ya nyuma?"
Toa ushauri unaojenga...badala ya kutibua na kutokubali matokeo ya utibuaji wako ni bora usitibue, baki nyia kuu...ukichepuka huwezi ukasimama na mishipa ukiitoa nje eti unamuheshimu huyo mumeo/mkeo! Itabidi ukapimwe akili! Huwezi mlazimisha mtu uliyemuumiza namna ya ku'react'! Maana kufanya hivyo unaweza sababisha makubwa zaidi!
Wanandoa, tujitahidi sana kuenzi viapo vyetu, tubaki njia kuu, ili tusijikute ktk mazingira magumu! Ukiacha mambo mengine kuna corona unaweza ambikizwa ikakugwarimu maisha yako na familia!
"
Nirudi kwako wewe ulieingilia usiyo yajua na kutoa ushauri juu,sijajua unajipa nafasi gani kwenye maisha yangu na unajiamini nini
Sidhani kama nimewahi kukupangia maisha humu ndani,au Kuna ninacho kutegemea hebu kiseme hapa ueleweke
Mwisho ushauri peleka kwa ndugu zako naamini lazima kuna watu wako wa karibu wanahitaji sana uwaongoze usijikute mshauri wa mitandaoni kushauri usio wajua"
Hukumbuki kuwa ww mwenyewe umekuwa mnufaika wa ushauri kutoka kwa watu usiowajua kama mwenyewe unavyoshuhudia[emoji848]! Leo hii hutaki nikashauri kwa jambo lilopindika kama hili...huoni na wewe unakuwa cyber bully[emoji848]! Ok, ok, samahani kwa kukushauri!
Ila maombi ni muhimu aiseeh!