Usijaribu kukaa na ndugu zako kwenye familia yako, utajuta!

Usijaribu kukaa na ndugu zako kwenye familia yako, utajuta!

Nilikashtaki kakatoa milioni tano akachukua baba mtu na mimba wakatoa nikajua watamsomesha kwa ile pesa ila waliitafuna tu binti akawa analia tena arudi nimsomeshe ila mm nimeshafuta napambana na wanangu
Duh watu kwa pesa sasa kwanini walishiriki ukatili huo kumtoa mimba kisha wanagoma kumsomesha!
 
Waswahili wanasema kuishi na watu Kazi.

Lakini pia, 'Limwambwata' likikolea Ndugu,Jamaa na Mrafiki wote unaweza kuwaona Kima tu😉

Kingine Mkeo, huyo 'mama P' wako, -Ni rafiki tu,
Anaweza akaja kukoroga mkaachana usiamini kuwa ni yeye, sasa usije ukawakosea Adabu Damu yako yako,
Kwa nguvu ya uliekutana nae ukubwani.
 
Tumelelewa na mama kwa muda mrefu,mimi ndiyo first born,baada ya kumaliza masomo na kuanza kujitegemea,mama alishauri niwachukue wadogo zangu ili nimpungie mzigo,
Nilikataa bila kupepesa macho nilimwambia awalee tu mpaka na wao wafike umri wa kujitegemea nitamsaidia kwa kila kitu ila wakiwa hapo nyumbani na siyo kuishi nao maana najua changamoto za kuishi na ndugu hasa ndoa ikiwa changa,
Mwaka jana mama alikuja kunitembelea ninapoishi,alinipongeza kwa msimamo wangu,akasema kwanza imewapa hamasa ya kuboresha nyumbani kwa kile unachowasapoti,na wamekuwa na ushindani wa kunisaidia mama yao ili wasionekane wamebweteka na kumwachaniza kaka yao.Pili kuna changamoto za hapa na pale kwa maisha yenu ya mjini msingewezana na wadogo zako.

NB:Saidia wakiwa kule kule na siyo kila shida usaidie shughulika na zilizo nje na uwezo wao.
Mke wa pia hauitaji bro?
 
Nakubali. Kuishi na ndugu hata uwe mwema kama malaika, maneno hayatakosa.

Mimi kaka yangu kosa alilolifanya ni kuruhusu mama aishi kwake. Japo maza naye ana kwake. Ila kwa kuwa walitengana na mzee kabla ya mzee kufariki, na hata baada ya kufariki mzee alikua na upweke sana. Kuumwa mara kwa mara. Mkienda hosp hakuna kitu. Etc. Ila tangu aliivoanza kuishi kwa bro, haumwi umwi tena. Wajukuu wamemzunguka muda wote anacheza nao. Mjukuu mwingine yeye daily anataka kulala chumbani kwa bibi yake. Basi raha mustarehe na mama haumwi umwi tena.


Sasa nakuja kusikia maneno kila kukicha huku na kule kuwa bro namnyanyasa na hamjali maza. Masista ndio kila kukicha.

Mara bro kashikwa akili na mke wake. Mara msichana wa kazi wa bro ana mdharau mama.

Hapo, maza kuna vyakula hali kwsbb za kiafya. Basi daily anaulizwa leo utakula nini na wanampikia anachotaka. Sasa maneno yameibuka mara mama hapewi hela ya chakula chake maalum, mara anawapigia simu ndugu kuomba hela na lawama zinarudi kwa bro.

Juzi kati nimewabalasa masista walivoniletea hizo mada. Nikawambia anayeona bro hamjali mama aende akamchukue akae naye. Na pia kama ni hela kila mtu atume hela kwa mama yake kadri anavyoona inafaa..

Bro kuna siku alisikia maneno yanayosemwa juu ya yeye kumnyanyasa maza amkuwa disappointed sana. Kifupi mimi ndio nimekua kimbilio lake. Namwambia asijali ndio maisha. Maneno yapo tu.
Una akili nyingi jomba
 
Kwa sasa nimepanga kuwa na roho mbaya sanaa sijui mtoto wa kaka sijui nani piga chini kmk

Tunajinyima halafu bado wanatuona tuna roho ya korosho
Kila MTU alee shahawa zake
Mkuu ni shida nmeshindwa hata kumaliza jengo langu mwaka uliopita sababu ya hizi mambo.Alafu wakijua una ka kitengo flani ktk gvt ,hata ndugu wengine Hawa waambii.wanakulundikia mizigo usiyo weza kuibeba.Nmenyonyoka manyoya January-feb Sina hamu apa .Nashkuru wanahitimu A-level wote mwaka huu
 
Be principled, tell them what you believe it is true, build your own culture to be known and followed by everyone regardless of pettytalks from anywhere.
Hiki ndicho ninachokifanya,kwa pande zote mbili yani kwangu na kwa mke wangu.i don't have bias..
 
Nadhani siyo ndugu wote wabaya kukaa nao ambae mnashindwana unamwambia tu kiustaraabu anafuata njia yake.kusema watu tusiishi kabisa na ndugu naona kama itakua ngumu.
 
Nadhani siyo ndugu wote wabaya kukaa nao ambae mnashindwana unamwambia tu kiustaraabu anafuata njia yake.kusema watu tusiishi kabisa na ndugu naona kama itakua ngumu.
Jamaa alikuwa anatema nyongo baada ya kuudhiwa na ndugu zake.
 
Ndugu wanawaweza kukugeuza mkatili sio mchezo.
Yaani wanaweza tengeneza image nje huko ukaonekana mbaya si mchezo

Bahati mbaya mume wangu anawasikiliza sana ndugu zake.yaani ni wazembe wadogo zake na mmoja ana tabia ya wizi,,
Kaka yake anamkania mwaka jana kaiba bajaj mpyaaa...tumejua mwaka huu..kaka yake ndo akili imeanza kumjia yaani mdogo wake ana mtia aibu hapa mtaani balaa.
Yaani ni stor ndefu inahitaji uzi.
Ila ukiambiwa jambo either na mkeo au na wananzengo kuhusu nduguzo..FANYA UCHUNGUZI kimya kimya sio kila mara ni chuki
 
Dogo amekua kituko mtaani lakini ni malezi ya kaka ake..ashanipigia mahusgel wangu vibao ameshawatukana yaan tafrani..sasa kaka ndo anaisoma namba
 
Back
Top Bottom