Usinunue kiwanja au shamba lenye mbuyu mkubwa kama huna uwezo wa kukabiliana na changamoto zake

changamoto ni zipi?
We mtu akikubomolea nyumba yako bila mapatano au ridhaa yako utakubali.
Hata madini yana namna yake ya kuchimba bila ushirikina maana ushirikina ni lazima mbeleni ukuletee madhara utake usitake. Tafuta mali kihalali kwa kuzijua siri za utafutaji pasipo kumkufuru Mungu wako
 
Mbona Masaki kuna nyumba zina hayo maiti makuubwa na watu wanaishi freshi tu?????!!!!!
 
Kama unasulubika huku unasali bado umjui Mungu,we ni mshirika tu wa nyumba ya ibada
Ukimjua Mungu huwezi kuwa masikini.
 
Kuna mti Mimi nimezaliwa nimekuta Hadi Leo Nina miaka mingi,watoto,lakini huo mti Kijiji kizima hakuna wa kuukata,
Kuna mwaka walijaribu kuukata ukaanza kuvuja damu

Mtu mzima na akili zake unakuta anaamini hii tu. Smh

Mitanganyika Bure kabisa. Kwa akili hizi bora mtawaliwe tena.
 

Mungu wenu anataka muwe maskini? Sasa mnamuamini wa nini?
 

Nawewe unaamini hizi story? This is too low, I held you in high regard.
 
Mshana Jr
 
Ndugu, acha kutumia maneno makali na kejeli.Wajinga na mazwazwa siyo lugha nzuri na yenye staha.Halafu bado hujaijuwa dunia na siri zake.Hicho unachokifahamu wewe ni sehemu ndogo sana.Waliosema elimu ni bahari siyo wajinga.Acha dharau na kejeli kwa vitu ambavyo huna elimu wala ujuzi nao. Penda kujifunza na kuacha ubishi na ujuaji wa kishamba.

Nb: Dunia hii ni pana sana na bado hujaifamu na hutakuja kuifahamu mpaka unakufa.Omba Mungu akupe hekima na busara.
 
Pengine hilo lenyewe ndilo lishirikina likuu la vilinge vya hiyo mibuyu, so linajitutumua hapa kupumbaza Watu hapa JF [emoji23]

Jamani muelewe hata hapa JF pia tunachati na mawakala wa shetani (mizimu, mapepo, majini, wanga/wachawi/washirikina na waganga wa kienyeji) maana shetani ni roho mchafu awezaye kuingia popote pale pasipo na uwepo wa Mcha Mungu haswaa [emoji16]
 
Sasa umeijuwa kweli, na watu kama hao usishangae gari yake kukuta zile sticker "This car is protected by blood of Jesus" kumbe ni washirikina hatari, wanaishi kwa makafara tena wengine ni wachungaji kabisa wa haya makanisa ya kisasa.

Wanakwambia devil is a lier huku wao ndio washirika wakuu.😄😄
 
Nani?
 
kwahiyo unatafuta kazi?Hujaeleza madhara zaidi kama kukata hata sisi twapiga 2hini
 
Nakuelewa sana Chifu, ndiyomaana hata Maandiko Matakatifu yametutahadharisha Watu kama hao....... [emoji116]

2 WAKORINTHO 11:14-15.

"Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.

Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao."
 
niliwahi kuambiwa na mzee mmoja kwamba miti mikubwa, mapango, mabwawa, maziwa na mito ni makazi ya majini(spiritual beings).

ndio maana wahandisi wa masuala ya ujenzi hutumia maarifa mengi ya kisayansi na pia maarifa ya kimila wanapofanya kazi za ujenzi kwenye maeneo kama hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…